Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,357
- 40,245
Ulimwengu wa sasa mapenzi yamekuwa ni biashara, mtu atajitokeza kuwa na wewe kwa sababu atanufaika na kitu fulani. Na hicho kitu kilichomvutia kikiisha au kupotea, uhusiano au mapenzi nayo yanakufa.
Atakayebaki na wewe katika majuto yako ya pesa, wadhifa, au umaarufu wako pale utakapoisha; ni mkeo/mumeo ambaye mmezaa naye watoto. Wale wengine wapembeni wataenda sehemu nyingine kupata wanachokitaka, huku wakikutazama wewe kama zoba.
Wapo wengi hasa wanawake walionufaika kwa kuzurumu familia za watu; wapo waliojengewa nyumba za makazi na za biashara, kufunguliwa biashara, kupewa pesa lukuki, kupewa nafasi sehemu fulani, kununulia vyombo vya usafiri n.k. Wakati mwingine wanaume wanaowawezesha hao, wanajisahau hata kujijali wao wenyewe pamoja na familia zao. Mwisho wa siku wanabaki na matatizo yao pale pesa au nafasi inapoisha muda wake.
Mbaya zaidi ukiingia kwenye mahusiano na aliyeshindikana, ambaye amekuendea kwa babu..kuchomoka hapo mpaka yeye akuhurumie, ahakikishe pesa yote imekata. Kuja kushtuka ata kibanda cha kufugia mbuzi huna.