Usitumie mapenzi kuzurumu haki ya familia ya mpenzi wako

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
15,181
2,000
Ulimwengu wa sasa mapenzi yamekuwa ni biashara, mtu atajitokeza kuwa na wewe kwa sababu atanufaika na kitu fulani. Na hicho kitu kilichomvutia kikiisha au kupotea, uhusiano au mapenzi nayo yanakufa.

Atakayebaki na wewe katika majuto yako ya pesa, wadhifa, au umaarufu wako pale utakapoisha; ni mkeo/mumeo ambaye mmezaa naye watoto. Wale wengine wapembeni wataenda sehemu nyingine kupata wanachokitaka, huku wakikutazama wewe kama zoba.

Wapo wengi hasa wanawake walionufaika kwa kuzurumu familia za watu; wapo waliojengewa nyumba za makazi na za biashara, kufunguliwa biashara, kupewa pesa lukuki, kupewa nafasi sehemu fulani, kununulia vyombo vya usafiri n.k. Wakati mwingine wanaume wanaowawezesha hao, wanajisahau hata kujijali wao wenyewe pamoja na familia zao. Mwisho wa siku wanabaki na matatizo yao pale pesa au nafasi inapoisha muda wake.

Mbaya zaidi ukiingia kwenye mahusiano na aliyeshindikana, ambaye amekuendea kwa babu..kuchomoka hapo mpaka yeye akuhurumie, ahakikishe pesa yote imekata. Kuja kushtuka ata kibanda cha kufugia mbuzi huna.
 

Haya_Land

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
5,656
2,000
Mapenzi sio pesa , Watu hatuna Pesa ila namba D zote hazikatizi.

mkitongoza wazee wa 25+ usitegemee huruma .
 

Cryptographer

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
288
500
Kama wanaume tunavyopenda wanawake kwa sababu ya tako.
Akijikwaa kwenye tope bahati mbaya au akiugua kuharisha mfululizo tako kwisha na mapenzi kwishnei.
Kwa hiyo Ngoma Droo!!!!.
 

joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
8,836
2,000
Kuna wanawake wengine wakiingia kwenye ndoa wanataka kila kitu wacontrol wao, itakuta kakukuta labda unasomesha wadogo zako na yeye unamtimizia kila kitu still anakasirika ukiwasaidia ndugu zako.

Kuna familia nyingine mzazi anakuendeleza kwa tabu sana ili baadaye uje kuwasaidia wadogo zako, sasa yy akiingia anakata kila kitu. Utakuta mzazi mwenyewe ni mjasiriamali mdogo mdogo mtaji wa kuungaunga, still anakasirika ukimsaidia mpaka mzazi wako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom