Usitoe kafara kupita kiasi utaishia kuwa sugu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
Wataalam wetu matatibu na walozi wa mambo ya Giza ni mahiri sana wa kujifanya wanajua kila kitu..Yaani wao ni maprofesa wa mambo ya Giza! Hawashindwi kitu...Lakini naomba nikwambie mpendwa wengi ni waongo kwakuwa kaliba ya ushirikina nayo ina madaraja yake na specialization zake Kwamba.

Kuna manguli wa vitabu tu
Kuna manguli wa majini tu
Kuna manguli wa mapepo tu
Kuna manguli wa hirizi na kuchanja tu
Kuna manguli wa mimea tuu
Kuna wasoma nyota viganja na majina
Kuna wapiga ramli na wazee wa tv asilia
Kuna manguli wa kafara tuu
Kuna wapandisha mzuka na mashetanj
Halafu kuna wenye uwezo wa kumiliki fani tatu au nne LAKINI KAMWE SIO ZOTE

Wakweli ambao ni wachache mno wanakuambia ukweli kwamba hii sio kaliba yangu ama hii sio saizi yangu...Nina mzee wangu pale Makanya yeye anakupasulia wazi kwamba fani yake yeye aliyobobea ni KUUA TUUU..Na hana kificho kwenye hilo....

Sasa ndugu zetu hawa waganga njaa wengi si wakweli...tatizo si kaliba yake yeye ata force, ama tatizo si saizi yake Lakini atataka kujaribu tuu ili apate mboga pesa na vitenge...na kwakuwa wewe ni mgonjwa na ni mhitaji na umeaminishwa na mtu unayemuamini sana basi unaingia mzima mzima

Ndugu yangu hizi kafara za kuku zinatibu mambo madogo madogo tu ya mahusiano ajira za kawaida na kupata Kiula yako tuu...roho na damu ya kuku ni vidogo na hafifu mno kulinganisha na roho yako na damu yako... kile kinachotokea ni kwamba asilimia 90 ya waganga hawatakukatisha tamaa...Mwisho wa siku maisha yako kiroho yanakuwa yamezingwa na maroho ya kuku na damu zao ...kumbuka vifo vyao vimetokana nawe

Madhara yake ninini?
Mosi unajiweka kwenye nafasi mbaya kiroho kutokana na roho zisizo na hatia ulizoziangamiza...zitakuandama
Pili kiroho utakuwa umejaa damu ya wafu hivyo kuyakaribisha mapepo machafu kufanya kikao kwako kwakuwa sasa yatakuwa na uhakika wa kula.

Tatu, mambo yako hayatafanikiwa na utazidi kudidimia kwakuwa sasa utakuwa umeongeza maadui, adui wa kwanza akiwa ni yule aliyekusababishia madhila na adui wa Pili akiwa ni haya mapepo yanayopata free meals kutokana na makafara unayofanya daily...yatahakikisha hufanikiwi shida yako ili waendelee kula bata

Maisha ya mafanikio ni mapambano magumu sana yasiyo na huruma wala simile...ni mapambano yaliyojaa ukatili mwingi tuu...hao waliofanikiwa waone hivi hivi....hivyo basi makafara hayaepukiki, huwezi kukwepa kutoa kafara kwenye njia ya mafanikio...lakini basi punguza athari za makafara kwa kutoa kafara sahihi kwenye tatizo sahihi na kwa kutumia mtu sahihi....ogopa sana wale wanaodai malipo kabla hasa pesa ya kianzio cha kazi na vifaa

Malipo halali ni mawili au matatu kulingana na kaliba ya mtaalam
Kiingilio cha madhabahu yaani commitment yako mwenyewe...hii kiuhalisia ni usajili wa kuzimu
Pesa ya vifaa..kutegemeana na tatizo na kaliba
Mwisho ni shukrani na hii hutolewa baada ya kufanikiwa jambo lako na hushurutishwi na yeyote kutoa

Pesa ya kiingilio si kubwa hivyo wengi hawahangaiki nayo...wahanga wengi hupigwa kwenye vifaa hasa hawa wazugaji na matapeli na pia kujilinda na utapeli wao huwapa watu masharti magumu mno
Kumbuka zaidi wanaojitangaza mitandaoni na kwenye mabango na vyombo vya habari hawana tofauti na manabii na mitume wa uongo....Asili yao ni moja....UPIGAJI
 
Saa 04:00am ndio post imepanda hewani, mida mibaya sana hii kwa nyie wazee wa vilinge

Tumenusurika kupinduka angani mida ya saa nane na dakika 46 hivi
giphy.gif

Shambulizi lilikuwa la kustukiza halafu kali
 
Kuna manguli wa vitabu tuu
Kuna manguli wa majini tuu
Kuna manguli wa mapepo tuu
Kuna manguli wa hirizi na kuchanja tuu
Kuna manguli wa mimea tuu
Kuna wasoma nyota viganja na majina
Kuna wapiga ramli na wazee wa tv asilia
Kuna manguli wa kafara tuu
Kuna wapandisha mzuka na mashetanj
Halafu kuna wenye uwezo wa kumiliki fani tatu au nne LAKINI KAMWE SIO ZOTE


Mkuu Mshana, wewe ni nguli katika upande upi??
 
@Mokaze kaka Mimi story tuu kaka labda na kupiga zongo kidogo


Usitufiche mkuu, katika jamii kama hii ya jf watu wa aina hiyo wanahitajika ili kuweka mambo sawa kwa wanajamii (jf), watu wanataka kuja Pm kupata walau ushauri nasaha, funguka mkuu.🤣
 
Back
Top Bottom