Usithubutu kuangalia mpira na girlfriend / mke wako utajuta

mkali kwanza

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,301
1,180
USITHUBUTU

*KUTIZAMA MPIRA UKIWA NA MWANAMKE NI QUESTION QUESTION STRESS TUPU*

*Mke:* _Honey timu gani zinacheza leo?_

*Mume:* ```Arsenal vs Manchester Utd```

*Mke:* _oooh safi sana, ninaipenda Arsenal._

*Mume:* ```Safi hiyo timu nzuri sana, hujakosea Darling.```

*Mke:* _Drogba anacheza?_

*Mume: ```Drogba hachezei timu yoyote kati ya hizi zinazocheza hapa.```

*Mke:* _Okey sweety. Oh huyo ni Chriss Brown?_

*Mume:* [akiwa ameboreka]
```Hapana huyo ni Theo Walcott.```

*Mke:* _Ahaa ila wanafanana sana. Hiyo kadi ya njano aliyoonyeshwa huyo mchezaji n ya nin?_

*Mume:* ```Hilo ni onyo kwa mchezaji aliyeonesha utovu wa nidhamu kwenye mchezo.```

_*```Baada ya dakika chache Wayne Rooney akafunga gori la kwanza kwa Manchester utd```*_

*Mke:* [Huku akishangilia pasina kujua timu yake ndiyo iliyofungwa]
_Oh oh Mume wangu Huyo ni walcot ndio amefunga goli ee?_

*Mume:* [akiwa mpolee baada ya kufungwa]
```Hapana sio Walcott ni Rooney ndio ameifunga Arsenal.```

*Mke:* [akiwa amefura hasira]
_Kwanini? Ilitakiwa Arsenal ndio ashinde._

*Mume:* [kimya]

*Mke:* _Hiyo kadi nyekundu aliyoonyeshwa huyo mwenye kiduku ni ya nini?_

*Mume:* [akiwa ameboreka kweli kweli]
```Hiyo kadi nyekundu inamaanisha kwamba mchezaji atoke nje kutokana na kufanya madhambi uwanjani.```

*Mke:* _Kwaio akitoka nje anaenda kuwa kocha?_

*Mume:* [akiwa amechoshwa na maswali ya mkewe huku akiwa hana utayari wa kujibu]
```Aaaaaaaa Hapana wife. Anatoka nje kabisa hatakiwi kuonekana hata kwenye benchi la ufundi.```

*Mke:* _kwaio kadi nyekundu ni kama taa za barabarani._
*Njano=Onyo*
*Nyekundu=Hatari*

*Mume:* [akijibu tu ilimradi yaishe]
```Haswaaa mke wangu, hivyo hivyo.```

*Mke:* _Vipi kuhusu kadi ya kijani_

*Mume:* ```mmmmmh hapana kitu kama hicho katika mpira wa miguu.```

*Mke:* _Nataka Arsenal ishinde kombe la Dunia_

*Mume:* [akaguna]
```Kombe la dunia ni mashindano ya mpira wa miguu baina ya nchi na nchi na Arsenal sio nchi ni klabu ya mpira. Inacheza kwenye ligi ya Uingereza```

*Mke:* _Ni nani huyo mbaba aliyesimama amevaa koti refu na anapua ndefu anaefanana na Mr. Bean?_

*Mume:* [akiwa ameboreka haswa]
```Huyo ni kocha wa Arsenal anaitwa Arsene Wenger.```

*Mke:* _Kwaio inamaanisha kwamba kocha wa hiyo timu pinzani anaitwa Machester Wenger?_

*Mume:* [akabadilisha channel na kuweka *TBC1 kipindi cha chereko*
 
Kwani hakuna wanawake wenye uelewa wa mpira wa miguu? Temna kuna wanaume wengi tu huwa wanauliza mwaswali kama haya. Story za facebook hizi umekopi.
 
Nilishawahi kuuliza kwa mr kama refa huwa anabeba idadi ngapi za kadi za njano na nyekundu mana nilijua ukipewa kadi ya njano au nyekundu unaondoka nayo......!!!
Vitu vingine si vya kufuatilia hasa ukiwa huna hobi navyo.
 
Nilishawahi kuuliza kwa mr kama refa huwa anabeba idadi ngapi za kadi za njano na nyekundu mana nilijua ukipewa kadi ya njano au nyekundu unaondoka nayo......!!!
Vitu vingine si vya kufuatilia hasa ukiwa huna hobi navyo.

Hehehehe!!
Bora kuwa kimya maana maswali ya kihivyo halafu timu anayoshabikia mumeo inapokea kichapo, aisei utakua keroooo...
 
Duu nimeipenda hii, huwa nakumbana na hii hali nikitazama movie yaani atakuja halafu halafu anaomba uanze mwanzo na baada ya dakika kumi na tano anaondoka akirudi utauliza masuala tele kama trafik aliekosa kosa la kukushitaki na kukubambikizia kesi
 
Back
Top Bottom