Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,182
Nafasi ya Uwaziri Mkuu haina mjadala na ya kuwa JK ambaye ni jemedari mpinga mabadiliko ataendelea na PM Pinda Mizengo ikiashiria ya kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya kikatiba kwa miaka mitano ijayo labda kama wanaharakati wataingia barabarani kwa maandamano na kuvumilia maji pilipili na mabomu ya machozi kudai mfumo mpya wa kuendesha nchi ubadilishwe ili kuzuia machafuko ambayo lazima uchaguzi ujao yatatokea kama mfumo wa uchaguzi utakuwa huu huu wa CCM, NEC na Idara ya mashushushu kutuchagulia mafisadi kututawala kinyume na misingi ya kidemokrasia...........
Wale wanaofikiri Pinda hana sifa hawaifahamu katiba yetu ambayo ipo wazi kuwa Mbunge yeyote mwenye jimbo anazo sifa za kuwa Waziri Mkuu na hakuna mahali ambapo wabunge ambao wamepita bila ya kupingwa wamebaguliwa hata kidogo..........
Ninaomba kuwakilisha................