Usishindwe na ubaya bali uushinde ubaya kwa wema. Warumi 12:21

Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
“ USISHINDWE NA UBAYA, BALI UUSHINDE KWA WEMA” WARUMI 12:21
Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema ni somo ambalo liko very motive kwa wale ambao wako katika elimu ya kidunia wanajua ni jinsi gani wanatakiwa kufanya iliwaskate tama kufikia malengo yao.
Kabla ya yote embu tutazame ubaya ni nini? Ni vitu ambavyo hufanyika kinyume na mapenzi ya ya Mungu. Pengine kwa kunena au kwa kutenda, kama utakua umesoma agano la kale na agano jipya basi utakua shahidi umekutana na mistari inasema “linda kinywa chako, kwa maana mdomo ho huo utoao Baraka ndio utoao laana.” Mfano 1 KOR 6:10 “ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike, washerati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.” Then swali la kujiuliza tufanye nini basi tuweze kushinda? Jibu linakuja katika MATHAYO 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Kumbe kupo na njia tayari tumeshapewa kwa ajili ya kwenda mbinguni ndio maana WARUMI 10:8 Inasema “Lakini yanenaje? Lile neon li karibu nawe, katika moyo wako; yani lile neon la Imani tulihubirilo; kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa ni Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.” Lakini si swala la kuokoka tu ndio upate wokovumaana Mungu anasema anawajua walio wake katika kitabu cha 2 TIMOTHEO 2:19 “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.”
Basi uovu tunaushindaje? Kama Bwana anavyosema? Embu turudi katkia WARUMI 12:21 “Usishindwe na ubaya , bali uushinde ubaya kwa wema.” Kama kweli umeokoka na kuamini lazima ujue Mungu hawezi funga mlango bila njia ya kutokea. Ulikuwa mtenda dhambi ukaamua kumrudia yeye hapo tafsiri inakuja katika biblia kama isemavyo kila alitajeye jina la Bwana na auache uovu. Lakini hii sentensi ya kila ubaya tuushinde kwa wema inamaanisha nini? Kama ubaya ni mambo yasiyompendeza Mungu basi twajua Mungu kaweka mlango wa kutokea ambao ni Kristo kwa yeyote aaminiye atapata uzima wa milele. Ulikua mwizi unaokoka unaanza kufanya kazi za mikono yako Mungu anakubariki, kama kinywa chako kilikua kinatumika kusema uongo, kulaani na kutukana ukamrudia BWANA lazima kinywa chako kitakua kina bariki, kuomba na kunena habari zilizo njema ambayo ni Injili ya Yesu kuwa alikuja ili wenye dhambi wapate kusamehewa, walio na shida wapate kupumzika. Dhambi zote tuzifanyazo tunazifanya nje ya mwili isipo kuwa uzinzi twaufanya juu ya miili yetu wenyewe 1 KOR 6:18 inatupa ushahidi wa dhambi hii “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” Basi kama zinaa tunaitenda juu ya miili yetu wenyewe ipo njia moja tu Mungu alitupa ili tupate wokovu. MWANZO 1:27-28 “ Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhaikiendacho juu ya nchi.” Vile vile ukiendelea katika MWANZO 2:21-25 “Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kasha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Nao walikua uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona aibu.” Kumbe basi tunaona tangu mwanzo Mungu alivyojenga njia ya kujitenga na uzinzi. Kwa maana aliweka wawili wawe mwili mmoja na pasiwe na mtu wa kuwatenganisha. Ndio maana katika ule mstari wa MWANZO 2:25 unasema “ Nao walikua uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona aibu.” Lakini swali linakuja akina nani basi ambao watakua uchi na waone aibu? Ngoja tuangalie mfano mwingine katika MAMBO YA WALAWI 18:5-23 “Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi BWANA: Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndiye Bwana. Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake. Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako. Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue. Utupu wa binti ya mwanao mume, au wa binti ta binti yake, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ndio utupu wako mwenyewe. Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni umbu lako, usifunue utupu wake. Usifunue utupu wa umbu lake baba yako; maana, yeye ni jamaa aliye karibu. Usifunue utupu wa umbu la mama yako, maana, yeye ni jamaa ya mama yako ya karibu. Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo, yeye ni shangazi yako. Usifunue utupu wa mkweo mwanamke yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo. Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana ni utupu wa nduguyo. Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanawe mume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake, hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu. Wala usitwae mwanamke pamoja na nduguye, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, huyo wa pili atakapo kua yu hai. Nawe usimkaribie mwanamke kufunua utupu wake wakati wa kutengwa kwa ajili ya unajisi wake. Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. Nawe usitoe kizazi chako chochote na kumwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako mimi ndimi Bwana. Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye ni uchafuko.” Hivyo tunaona aibu kuu Mungu aliyoikataa ilikutuweka kuwa safi. Pia habari hizi utazipata katika MAMBO YA WALAWI 20 zikiwa zimeandikwa kwa lugha nyepesi ambayo waweza isoma na kuielewa kwa ufasaha. Lakini tumeanza kupata picha jinsi ya kuacha zinaa maana wote twajua mume na mke wakioana wote wanakua mwili mmoja na habari za kuachana hazikuwepo katika uumbaji wa Mungu. Embu tuangalie katika agano jipya ambalo Injili yake iko wazi imefunguliwa ili kila mmoja aelewe. Mungu ametuonya nini katika agano hili la pili? Ni swali ambalo lazima tujue kama kweli tuna taka kuushinda ubaya kwa wema. 1KOR6:15-20 “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala nyinyi si mali yenu wenyewe, maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Kumbe tumejua miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu tuliyepewa na Mungu ili aweze kutupa vipawa vya kumtumikia MUNGU. Basi twawezaje shinda ubaya huu wa zinaa kwa wema? Embu tusome katika 1 KOR 7:8-9 “Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tama.” Kumbe tunaambiwa kama hatuwezi kujizuia ni heri kuoa kuliko kuwaka tama, wewe kijana, ewe binti wapata faida gani hasa kuuharibu mwili wako mwenyewe kwa tama za siku moja au masaa kadhaa tu kasha siku nyingine wafanya vivyo hivyo? Tena siku hizi wnakwambia kabisa ni bora uwe na wanawake au wanaume wengi ili siku mmoja akizingua unachukua mwingine bila haya kabisa! Wengine wanasema wanatengeneza njia ya ndoa ili siku wakija kuoa au kuolewa wawe wameshayazoea bila aibu kabisa unabaki unajiuliza huyu anamwabudu Mungu yupi? Ambaye atampa uzima siku ya mwisho? Kwa maana Mungu kasema katika 1TIMOTHEO 5:14 anatoa ruhusa ili msije kumpa nafasi adui ya kumlaumu. Embu tuone anasema “ Basi napenda wajane ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kumlaumu.” Ukiuliza asilimia 70 ya watu wote wakupe sababu ya kwanini wanazini watakwambia ni kufaidi ujana wanasahau biblia inasema mkumbuke Bwana Mungu wako kabla hazijaja siku za hatari, kwa maana kila mmoja hujaribiwa kwa tama zake mwenyewe. YAKOBO 1:12-18 anasema “ Heri mtu Yule astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa atapokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na MUNGU; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tama yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tama ikiisha komaa kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha komaa huzaa mauti. Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neon la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake.” Lazima utakua umejiuliza kwa nini nimeongelea kuhusu kujaribiwa ? jibu ni kuwa kila mmoja wetu hjujaribiwa kwa kadiri ya tama zake mwenyewe huyo atajaribiwa hivi na huyu hivi lakini Mungu anasema usishindwe na ubaya bali, uushinde ubaya kwa wema. Ukipata nafasi soma 1KOR 7:1-40 lakini mimi nitakupa baadhi. 1KOR7:1-5 “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mu,me wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena; Shetani asije akawajaribu kwa kutokua na kiasi kwenu” vile vile Mungu hakua na mpango wa kuachana ndio maana 1KOR 7:10-11 anasema “ Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana mke asiachane na mumewe lakini , ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena asimwache mkewe.” Vivyo hivyo katika MATHAYO 5:32 ” Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa Yule aliyeachwa, azini” ukiendelea katika sura ya 19 katika MATHAYO mstari wa 3-9 anasema “Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu? Akajibum akawaambia Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu na mumee na mtu na mke, akasema kwa sababu ya hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe. Wakamwambia, jinsi gani basi Musa, aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha? Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Name nawaambia nyinyi, kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini, naye amwoaye Yule aliyeachwa azini.”
Kumbe tumeona mpango wa Mungu kabla dhambi haijaingia na mpango wa Mungu wakati dhambi imeingia. Yote hufanyika kwa ajili ya kutuokoa sisi ili tuweze kuushinda ubaya kwa wema. Lakini kuushinda ubaya kwa wema ni vigumu sana usipovaa silaha za Mungu. Lazima tuzijue silaha za Mungu ilitujue vita tunayopigana ni juu ya mamlaka gani? Silaha za Mungu utazipata katika WAEFESO6:11-18
Anasema “ Vaeni silaha zote za Mungu ,mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu war oho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimizia yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani, zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye motoya Yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neon la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.” Kumbe tukisha kuvaa au kutwaa silaha zote za mbinguni twaweza shinda ubaya kwa wema kwa maana MUNGU hafanyi uovu wala hajaribu mtu kwa uovu. Hivyo basi mwisho kabisa napenda kumalizia na LUKA 10:17-20 “ NDIPO WALE SABINI WALIPORUDI KWA FURAHA, WAKISEMA, BWANA HATA PEPO WANATUTII KWA JINA LAKO. AKAWAAMBIA, NILIMWONA SHETANI AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI KAMA UMEME. TAZAMA, NIMEWAPA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, WALA HAKUNA KITU KITAKACHOWADHURU. LAKINI MSIFURAHI KWA VILE PEPO WANAWATII, BALI FURAHINI KWA SABABU MASJINA YENU YAMEANDIKWA MBINGUNI.”
Ahsanteh! Kwa kusoma share na marafiki zako waweze kupata ujumbee huu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom