Usisahau kuwa sio kila Kondakta anaweza kuwa Dereva mzuri

MenukaJr

Member
Apr 24, 2021
50
128
Rafiki. Nakusimulia hadithi niliyopata kusimuliwa miaka mingi kidogo iliyopita. Kwamba, hapo zamani palitokea safari ya wana-familia, kutoka Da'slama kwenda Dodoma. Kama kawaida ya safari zote, safari ilianza kwa furaha na matumaini makubwa. Halafu ikatokea bahati mbaya kwao safari ikamalizika kwa maumivu na majuto makubwa. Safari ikaacha vifo, maiti, mauti, vilema, machozi, visasi na risasi!!

Siku ya safari kulipambazuka vizuri hali ya hewa iliruhusu kila jambo. Utukufu wa Mungu ulikua hadharani licha ya mawingu kidogo yaliyokuwa yakijiliwaza huku na huko angani. Safari ilikua ni kwa gari dogo aina ya Coaster, si jipya sana na wala si chakavu. Gari la umri wa kati lakini lililotunzwa likatunzika, kila kitu chake kilikua bado kwenye nafasi yake. Wenyewe walikua wanapenda kuliita Coaster Mayai. Watu ishirini na tano na ushehe ndani ya gari, familia nzima Dereva pamoja na Kondakta. Ndani ya gari kulibebwa chakula kizuri, mvinyo na vinywaji aina aina. Ilikua ni full shangwe!!

Safari ikaanza alfajiri na mapema kwa furaha na amani kama nilivyokusimulia hapo juu. Dereva wa gari ketwa Mr. John na Kondakta wake nimesahau jina lake. Haki sawa, safari na muziki. Gari ikala rami na rami ikakubali kuliwa na gari kisawasawa. Katika wakati wote wa safari, Dereva alikua makini sana kama ujuavyo kubeba familia nzima kwenye chombo kimoja yataka umakinike zaidi. Ilikua ni kazi tu, kwenye 50 Dereva alikwenda 50, kwenye matuta alipunguza mwendo na penye 80 alikwenda vivyohivyo. Rafiki. Ilikua ni safari nzuri kusema ukweli!!

Safari ilipokwenda zaidi karibia nusu yake ikaja bahati mbaya kwa Dereva. Akapata mshtuko wa moyo, mapigo ya moyo yakaongezeka, umeme ukakatika ghafla presha ikapanda. Akaweka gari pembeni kidogo. Porini katikati, kama ni mwenyeji wa Kibaigwa ya mwisho unaweza kuona utupu ule wa ardhi. Hapakua na msaada wowote kwa wakati huo, nyumba moja moja na barabara tulivu. Hali ya dereva ikaendelea kuwa mbaya zaidi. La haula!! Kabla hawakujua la kuchukua, Dereva akafariki. Hapakua na njia nyingine zaidi ya Kondakta kuchukua usukani ili safari iendelee. Huko mbele, mwisho, mambo mengine ya kutafuta Dereva mwingine yangalifanyika kama ingalihitajika.

Rafiki. Nikwambie tu ukweli wa moyo wangu, sio kila Kondakta anafaa kuwa Dereva. Wana-familia hofu ikaanza kuwatawala. Wanafahamu, Dereva ndie mtaalam wa mambo ya kuendesha gari na Kondakta ni msaidizi wake katika shughuli zingine ndani ya gari. Sasa Kondakta ameshika usukani ili safari ifike mwisho. Walijiuliza kama safari itafika mwisho salama, kila mtu alimuachia Mungu!! Rafiki, kama umewahi kuendeshwa na mtu usiyemuamini unaweza kuhisi hofu waliyokuwa nayo wana-familia. Gari lote kimya, safari ameachiwa Dereva-Kondakta.

Wala safari haikua imeenda mbali zaidi, hofu ikabadilika kuwa kweli na hakika. Dereva-kondakta gari likamshinda nguvu, likapinduka mara nane hadi katika mtaro. Ilikua ajali mbaya sana, kama ungafanikiwa kuiona ungeweza kuamini kuwa sio kila Kondakta anafaa kuwa Dereva. Marehemu Dereva akafa tena kwa sababu hakuweza kujitetea na ajali kama wengine. Wana-familia wakaumia, wakavunjika vunjika vibaya. Gari likaharibika nyang'anyang'a!! Mashuhuda wanasema ni Mungu tu mwenye rehema. Wanasema Dereva-Kondakta alifanikiwa kuruka dirishani. Huo ndio ukawa mwisho wa safari njema iliyoanza kwa furaha, amani na matumaini makubwa. Ikazimika!!

FUNZO: Sio kila Kondakta anaweza kuwa Dereva mzuri. Rafiki. Hili ndilo funzo nililolipata mimi katika hadithi hii japo hata wewe unaweza kujifunza itakavyokupendeza. Mwenye hadithi anasema vyovyote utakavyojifunza, usisahau kuwa sio kila Kondakta anaweza kuwa Dereva mzuri.
#Nenda kwa usalama, ajali zinaua!!
MenukaJr,
Jamii Forum.
 
Tatizo lilianzia pale mlipompa John udereva wakati mnajua kabisa kwenye moyo wake pamefungwa Magneto!!

Konda atatufikisha salama tu, John alikua na rafu nyingi ila nyinyi mlishakunywa Pombe mkaweka Kufuli kwenye vichwa vyenu mkawa hamuoni rafu zake maana aliwagai ganji!
 
Tutaelewana tu. Na huyo dereva keshakuwa chakula cha funza. harudi ng'o
 
Madereva wa kike wako makini barabarani kuliko wale wa kiume.

Na umakini wao unaongezeka zaidi kama hapo mwanzo waliwahi kuwa makondakta.
 
kosa la deleva alikua mroho wa madaraka na ndio maana kamchagua kondakta ambae ana uzoefu wa gali ili anapocheza lafu asiwe anamuhoje tumlaana kw a uloho wa madalaka
 
Back
Top Bottom