Usirogwe Kujiunga na Kifurushi cha Airtel. Utajuta kupoteza pesa mbayo ungempa Maskini angekuombea Kheri.

airtel ilikuwa poa ila hapa katikati walipata shida network ilikuwa hovyo hata hivyo haijatengemaa ila kuna baadhi ya watu wanapata net vizuri na baadhi haifanyi kazi kabisa na wengine wanapata usiku tu ikifika asubuhi kimya





Usirogwe Kujiunga na Kifurushi cha Airtel. Utajuta kupoteza pesa mbayo ungempa Maskini angekuombea Kheri. au ni bora ununue maziwa unywe. ni bora ununue juice unywe. airtel wamekuwa wahuni wezi na watu wa hovyo. kifurushi chao kwenye simu hakifungui hata google. kita search kwa muda mrefu sana na kikija kukubali kitakwambia page not found. kimekuwa cha hovyo sana.

huwezi kudownload au ku update.kiuhalisia wamekuwa wezi na wizi wao naona kama umehalalishwa maana wanaendelea kutuibia huku nasi tunangaalia. kwa sasa naona mtandano ambayo speed yake si haba umekuwa ni tigo mimi ndo hunisaidia. NIMEJARIBU KUTUMIA AIRTEL NIKIWA POSTA, NIKIWA MWENGE,NIKIWA KIJITONYAMA,NIKIWA TABATA KOTE ninafail sana. kila wakati mtandao hauwezi kufungua JF,hauwezi ku upload au hata kufungua FB ,hauwezi hata kutafuta kitu Google.

najiuliza nini tatizo? maana before nlidhan ni simu nimenunua simu nyingine bado hali ni ileile. hizi pesa zangu walizochukua ntarudishiwa vipi au nijirudishie vipi?
 
mm niliweka bundle airtel one day aisee nilijutaaa mpk line nikavunja ila zamani walikua vizuri sana mwaka 2014 walikua wanatoa mb 800 kwa tsh 1000 mwez nzima
 
Mkuu umesema neno,naunga mkono hoja na kama wahusika wako na huku wajirekebishe tangu juzi play store imegoma,Google ndio kabisaaaaa,YouTube hali kadhalika wanafanya makusudi hawa jamaa tena wanafanya mambo yasiyojulikana....mfyuuuu zao nonsense.
 
Duh! Aisee, mimi kwa hapa nilipo airtel ndo msaada mkubwa sana aisee, na ipo vizuri sana.. voda na tigo wote hamna kitu..
 
Hao ndio wezi squared
Ingawa wako fast hasa Usiku ila na doubt kama MB wanazotoa ni kweli kulingana na pesa , utakuta kifurushi cha 4Gb una download movie 2 tena za labda 1.4GB unaambiwa kifurushi kimekwisha.ILA tukizungumzia ufanisi na kasi hakuna kama VODACOM 4G
 
Umegenerelize sana, I am using airtel na sijaona sababu yakuhama bado, hayo matatizo hayajawai kunikuta, I guess tatizo ni simu yako au eneo ila sio tatizo la kila mtumiaji wa airtel.
 
Mimi nadhani inategemea na location uliyopo, kwangu mimi apa Airtel ipo vyema ila nnafkiria kuhamia voda au ttcl.
 
Uko sahihi kabisa mkuu hakuna mtandao wowote unaouzidi vodacom kwa ufanisi, kasi na uko reliable kuliko mtandao wowote Tanzania by far hiyo nazungumzia kiujumla ingawa mapungufu ya hapa na pale yapo pia mkonga wa net ukikata wana backup ya satelite spidi itakuwa ndogo lakini net huwa inakuwepo na kumaintain mambo kama hayo ni gharama ndio maana gharama zao ni juu
Ingawa wako fast hasa Usiku ila na doubt kama MB wanazotoa ni kweli kulingana na pesa , utakuta kifurushi cha 4Gb una download movie 2 tena za labda 1.4GB unaambiwa kifurushi kimekwisha.ILA tukizungumzia ufanisi na kasi hakuna kama VODACOM 4G
 
Back
Top Bottom