Usiri wa wakaguzi & wapima mizigo na wamiliki wa mizigo hiyo katika viwanja vya ndege nchini tz... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usiri wa wakaguzi & wapima mizigo na wamiliki wa mizigo hiyo katika viwanja vya ndege nchini tz...

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TUJITEGEMEE, Nov 13, 2011.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,786
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Katika siku za karibuni nilibahatika kutembelea baadhi ya viwanja vya ndege. niliweza kushuhudia jinsi utaratibu wa ukaguzi na upimaji wa mizigo unavyofanyika. Kuna jambo moja lilinishtua katika eneo hili ambalo nimehisi nanyi wa JF kuwashirikisha kulifahamu(kama ulikuwa hulifahamu). Jambo lenyewe ni usiri unao kuwepo kati ya baadhi ya wamiliki wa mizigo na wapimaji/wakaguzi wa mizigo hiyo katika viwanja hivyo vya ndege. Usiri huo unatokea baada ya wakaguzi/wapimaji wa mizigo kumaliza kazi ya kukagua/kupima mizigo hiyo. Utawaona wahusika wanaitana pembeni na kupeana "vikaratasi" kwa uficho.

  Wasiwasi wangu juu ya USIRI huo ni kuwa kuna uwezekano wa ulaghai wa uzito halisi na uhalali wa mzigo unaosafirishwa, jambo ambalo linaweza kusababisha:

  1.0 upungufu wa mapato kwa shirika la ndege husika na serikali (kama uzito utakaosafirishwa utakuwa mkubwa kuliko ulio unaoonyeshwa kwenye nyaraka)
  2.0 Kusababisha ajari kama ndege hiyo itabeba mzigo kupita kiasi( kama mwendesha ndege hatakuwa makini kugundua hilo)

  3.0 Kurahisisha shughuli za uharamia wa ama kuteka au kulipua ndege unaoweza kufanywa na watu wasio na "utu" na kusababisha maafa makubwa(endapo mizigo hiyo itakuwa ni ya kudhuru usalama wa abiria).

  USHAURI WANGU: Mamlaka zinazohusika(Usalama,TRA n.k) zifuatilie jambo hilo.

  Nawasilisha.
   
Loading...