Usiri wa Serikali-Government Gazette: Make it Public! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usiri wa Serikali-Government Gazette: Make it Public!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 22, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hivi kwanini Gazeti la Serikali maarufu kama Government Gazette ambako mambo muhimu ya Taifa kuanzia sheria, kanuni, katiba, au matangazo rasmi huwekwa na mabadiliko katika sheria, kanuni, katiba, mikataba au miswaada huchapiswa si jambo la wazi na rahisi kupatikana kwa kila Mtanzania?

  Ukienda kwenye website ya Bunge, hakuna, ukija website ya Serikali hakuna, sasa ni vipi sisi kama wananchi tujue mabadiliko au ukweli wa mambo ambao unachapwa na Gazeti la Serikali kama sheria au katiba ikiwa kila kitu kinafanywa kwa siri na kufichwa?

  NI siri gani zilizomo kwenye kijarida hiki rasmi cha serikali tufichwe ukweli na kisha kuja kudhulumiwa haki kwa kuambiwa mambo yaliandikwa kwenye kigazeti hiki?

  Make the damn Government Gazette available to public and through all means including internet if the Gazette is still circulating in few the proud eyes!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Mzee hilo gazeti linapatikana kwenye maduka ya vitabu vya serikali. Mtu yeyote anaweza kwenda kulinunua. Labda kama tunataka kuwa nakala yake iwe inapatikana online, but then itakuja hoja nzima ya serikali yetu na matumizi ya Interneti!
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Zamani hilo duka lilikuwa mtaa wa Jamhuri karibu na kona ya kuelekea Mbowe ( mtaa wa Mkwepu?). Lakini sidhani kama utakuta gazeti zote na sidhani kama unaweza kuweka oda!
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Inaelekea Government printer ambaye ndiye pekee anayeruhusiwa kuchapisha nyaraka za serikali, hana uwezo wa kutoa machapisho ya kutosha.Matokeo yake utakapoenda pale kununua iwe ni Official Gazettes au hata statutes unakuta hakuna.Labda kama alivyosema mchangiaji mmoja, yapatikane kwenye mtandao.Hata hivyo tukumbuke kuwa machapisho hayo yanauzwa na ni chanzo cha mapato, yatakapotolewa kwenye mtandao utaratibu wa malipo unaweza kuwa na utata..sijui lakini. We need to find a way to inform the public on some of these issues.
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Asante womenofsubstance! Lakini hoja ndiyo inayo beg the question ya ulazima wa kitu kama Government Printer. Sidhani kama ni busara kuwa na chombo mahususi cha serikali cha kuchapa vijarida, diaries, kalenda, picha za viongozi n.k. Tukiondokana na imani kuwa kila kitu ni siri, tutaweza kufuta Government Printers na machapisho yote yakawekwa mtandaoni. Kwa wale ambao wanahitaji hardcopy, hizi zinaweza kuchapishwa na watu binafsi kwa kuwashindanisha! Kwa nini tuwe na chombo ambacho kukiwezesha hatuwezi?
   
 6. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #6
  Sep 22, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 7. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mpiganajinambamoja,

  Binafsi nashukuru kwa link ila nimejaribu kuifungua haifunguki is it a computer glich on my side au web site ndio in matatizo?? Is anyone able to open the link?
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Je kwa mikoani kijarida hicho unaweza kupata ofisi gani? Yawezekana ni kweli kuwa Tz ni Dsm na mikoani ni nchi nyingine kabisa.
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni kweli linapatikana lakini baada ya muda mrefu kupita, ukitaka la mwezi huu huwezi kulipata labda iwe inatolewa bungeni au uende Wizara ya Sheria wakutolee copy. Katika duka la vitabu vya serikali utapata vya mwaka jana
   
 10. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2008
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,957
  Likes Received: 20,288
  Trophy Points: 280
  Sina hakika na upatikanaji wa gazette katika maabara za mikoa na hata wilaya ukizingatia kuwa si mikoa yote yenye maktaba zinazoeleweka na wilaya nyingi tu hazina maktaba
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kwa maelezo ya Mkuu Halisi hapo juu,ndugu yangu Obe uko sahihi.Asante sana
   
 12. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Hata ulienda Ubalozini hawana, Maduka ya Serikali ni machache na upatikanaji wake huwa mgumu, kwa nini Gazette lisipatikane hata maktaba, mashuleni, vyuoni au maduka ya vitabu?

  Ikiwa online tuna picha kebekebe za Raisi akikagua mayai, kwa nini tushindwe kuwa na official site ya Gazeti la Serikali ambapo kila Mtanzania mwenye uwezo wa kwenda online atapata anachotaka?
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  gazeti hili linalenga kuwafahamisha wananchi kuhusu maamuzi yanayofanywa na serikali, kwa nini liuzwe wakati wananchi wanalipa kodi? Lichapwe kwa wingi na ligawiwe vijiji vyote, achilia mbali kwenye maduka ya serikali. Kuanza kuliuza ni kuwatenga wananchi wengine ambao nao wana haki ya kujua serikali yao imefanya nini. kwani serikali si ilishasema imeachana na biashara?!?
   
 15. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu Rev,
  Ukosekanaji wa Gov. Gazzette (GG) katika muda muafaka Inawezekana kabisa ikawa pia ni kinyume cha sheria. Yapo matangazo yanayotakiwa yatangazwe na GG ili yaweze kuwa sheria au pia yapo matangazo mengine yanayohitaji kutangazwa humo ndio yaweze kutekelezwa, k.m. masuala ya uraia, ubadilishaji majina n.k.


  Tatizo letu TZ ni kuwa, serikalini yetu siku nyingi sasa walishaacha kuendesha mambo yake kulingana na taratibu na sheria, bali mambo hufanyika kufuata "matamko" tu ya wakuu wake. Sitashangaa kuona kuwa Gov. Printers ikawa na bajeti ya kutosha mishahara tu ya watumishi wake na copy chache za GG, maana sidhani kama umuhimu wake unaonekana kwa watawala wetu.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inafunguka, nimeona nakala ya mwisho kuwa posted ni ya Mei mwaka huu ingawa sijaifungua hiyo nakala (i am busy kidogo)
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Haka kagazeti nimekaona toka nikiwa mdogo, enzi hizo mwandishi wake alikuwa ni Tabu Mangara (RIP), ambaye kama sikosei alikwua ndiye mchapaji mkuu wa serikali,

  Huwa sikaelewi vizuri hasa ni na madhumuni yake, na mara nyingi utakakuta kwenye nyumba za viongozi wa serikali, na huwa kanapelekwa na mtu kutoka Ikulu, lakini mpaka leo sijakaelewa nia na madhumuni yake hasa ni nini?
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kanaeleza maamuzi ya serikli yaliyofanywa, kuanzia uteuzi/kufukuzwa/kuhamishwa kwa watumishi hadi kuanza kutumika au kufutwa kwa sheria
   
 19. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2008
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  In Queen's language,

  Government Gazette, which is published by many other governments worldwide, is a means through which the government can communicate to its officials and the general public.

  It is the official publication for rules, proposed rules, and notices of the government agencies and organizations, as well as executive orders and other presidential documents.

  Government Gazette is a useful not only in monitoring the actions of the government, but also as a primary source documentation in research.
   
 20. C

  CHAUMBEYA Member

  #20
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 15, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kama unahitaji statutes si uende kwenye website ya bunge kuna very latest statutes zinawekwa pale. kuhusu government gazzette ni lazima mtu utambue kuwa lile ni kwa matumizi ya serikali na wadau wengine muhimu. ni kweli linapatikana kwa shida lakini huwa linatoka kila wiki vipande vipande.
   
Loading...