TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,599
- 23,886
Amani kwako mdau.
[ ONE YEAR AGO ]
Kuna hali isiyo salama ktk maeneo kadhaa jijini Dar inayosababisha baadhi yetu kudhurika kisha kubakiwa na majeraha mwilini pindi unapokutwa na kadhia hii.
Kwanza ilinitokea mimi mwenyewe nikirudi nyumbani kutoka maeneo ya ununio beach majira ya saa 19:00, nilikuwa mwenyewe natembea, mbele yangu kulikuwa na jamaa anakuja na nyuma hakukuwa na mtu, hivyo sikujali nikaendelea kuchezea kaji_smartphone kangu.
Takribani dakika mbili hivi kukawa na jamaa wawili wanakuja upande wa nyuma wanaongea mambo yao ila walikaza hatua, nafsi ikanipa hisia nijitenge nao wapite kushoto me nisogee kulia wananikaribia na kunipa salamu ni vijana wawili ambao kwa kigiza kile si rahisi kuwafaham, sikuwajibu salamu yao kutokana na nilivyoji_tune mwenyewe.
Yule aliyekuwa anakuja mbele yangu alipunguza hatua.
Ktk hali ya kutoelewa nini kinatokea, hao vijana kwa gafla sana, walianza kunishambulia kwa mapanga, marungu na siraha nyingine, kuna wakati niliona naweza kuwamudu baada ya kumpa kichapo mmoja akatoa sauti ya maumivu ya kwenye nyonga, but niliona hapa si salama baada ya yule jamaa aliyekuwa anakuja kwa mbele kutoa siraha kama panga na kunikata nalo mgongoni, nilirusha ngumu but ile ngumi ilikutana na panga iliyokata kidole changu kidogo mkononi.
Nilikuwa na begi mgongoni ambalo nilijitoa mhanga nife ili waondoke nalo au nipate msaada!.
Baada ya kukatwa kidole damu ilivuja sana nikona hakuna jinsi, nikarusha simu mbali kidogo na gafla kuna gari ikawa inakuja usawa tuliokuwapo wakaikimbilia simu na kukimbia.
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
[ YESTERDAY ]
...Imetokea usiku wa leo.
Ilikuwa ni muda tofauti na mimi, hii ilikuwa yapata majira ya saa 21:00 ambapo.
Ni maeneo ya Boko kitendo/mazingira kama yale yaliyonikuta mimi ndiyo yamemkuta mtanzania mwenzako ambaye yeye amekatwa na kitu chenye ncha kali (sijui kama ni panga) kichwani na kuporwa fedha.
MY TAKE:
Kwa sasa hali hii inashika kasi chukua hatua stahiki kujilinda na kujiepusha kutembea mwenyewe labda pale inapobidi jua linapozama.
Asanteni.