Usipotoshwe na watu wasioelewa maana na utaratibu wa kuwa na raia pacha. Angalia hapa maelezo ya uraia pacha na niulize swali lolote nitakujibu

Eti utaratibu wa raia pacha, nani kauweka,si binadamu tuu,tena kwa interests hasi.Achaneni na kusombwa na ideas fake zenye nia ovu,be pragmatic,that is deal with things sensibly and realistically in a way that is based on practice rather than theoretical considerations.
Umejibiwa vizuri. Kataa wenzio ndio tunaondoka hivyo

Freedom is coming tomorrow!!!!!

Hili swala la uraia pacha huwa linapotea na kurudi kama homa ya vipindi.....
kamwe hamtofanikiwa
Freedom is coming tomorrow!!!!!

Sasa ndio hoja unazofikiri zinaweza shawishi wengi kuunga mkono Uraia Pacha? Kwamba kwa vile vipo tulivyocopy na hili nalo tubebe tu?

Hatutaki! Hoja zako ni dhaifu, Dunia ina maelfu ya Sera na Itikadi, Kwanini usihoji kuwa hatukuchukua zote? Na kwanini iwe Uraia Pacha tu?

Hatutaki! Bakini na mkiitacho Usasa. Endeleeni kupiga poyoyo za hapa na pale kwa wakati huu. Muda bado.
Freedom is coming tomorrow!!!!!!

Hili la uraia pacha hatulitaki. Lilishindwa wakati wa kikwete na litashindwa hata sasa. Hatuhitaji raia mamluki wenye kuweza kua wazalendo kwa nchi nyingie au kuweza kutumiwa na adui wa nchi au kuweza kuisaliti nchi au kuihujumu uchumi wake. Hao wanaokupa uraia nao wana malengo yao.
Uraia pacha ndio huo unakuja, mtabaki madungaembe mnahangaika eeh!

Kwa hiyo Tanzania tukiruhusu uraia pacha, wageni wataruhisiwa kununua/kumiliki ardhi ya Tz freely?
Hawawezi kuwa wageni tena, watakuwa ni raia wa Tanzania waliopewa uraia kwa kuzingatia vigezo na masharti. Na wakiwa raia ndio watakuwa na haki sawa kama raia wengine, japo nimesema kunaweza kuwa na exceptions katika suala la nafasi za kisiasa, ingawa ukifanya hivyo inakuwa unapingana na Katiba.
 
Kwa ninavyowaona wageni wakipata uraia wa Tanzania hamna maajabu watafanya. Yani Mhindi umpe uraia wa Tanzania akiwa katoka India unadhani atafanya nini, ataleta mapikipiki yao auze achukue hela arudishe kwao India. Ukimleta Mfaransa hivo hivo atafanya. Hawa wataondoa nafasi za wabongo wanao-import bidhaa za nje, watakuwa export houses za makampuni ya kwao

Wabongo walioko nje ni wachache na wana hela kidogo tu za kupandia ndege. Ukiwaambia watoe mitaji walete uku haiwezi fidia hela inayochotwa kwenye mzunguko wetu kwenda nje. Kwa mtazamo wa kiuchumi

Umeeleza mengi ambayo sikuyafahamu. Asante
Ni Kwa nini jambo la uraia pacha huwa linahusishwa sana na kuleta hela Tanzania, uwekezaji na mengineyo? Hebu niambieni, tangu lini mama/Baba mzazi akamkana mtoto wake aliyepotelea ng'ambo kisa tu ana makaratasi mfukoni yenye nchi nyingine? Na huu uraia pacha kwa wageni, hivi utakuwa unagawiwa kama njugu? Mbona watawala wetu wakoloni wa uingereze, Ujerumani, Australia, Ireland , Kenya, Rwanda na nchi nyingine zote zinazoruhusu uraia pacha haziweki kigezo cha uwekezaji kama sharti kuu la uraia pacha? Mbona hizo nchi ziko poa tu hata uwe na makaratasi mia? Ni nini sisi kama nchi Tanzania tunaweza kujifunza katika nchi hizo zilizo tutangulia kuukubari uraia pacha kabla yetu au ni mawazo fiunyu tu, uvivu wa kufikria na ntima nyongo isiyo na wivu? Kama ni issue ya uzalendo, nafikiri wa-diaspora ni wazalendo number 1 kuliko hata hao wanaopoinga kulipa Kodi ya Miamala kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mwisho, haki ya mtu kuishi, kukaa au kwenda mahali popote pale duniani, ni haki ya msingi- fundamental right ambayo haitakiwi kuchanganywa (Breach) na mambo mengineyo kama ya usalama na uwekezaji, ili hali tu- save for- kama hawavunji sheria za nchi husika , haina maana kuwanyima kwa sababu tu ya ntima nyongo na wivu usio wa maana.

Kama watakuwa waharifu, sheria nyinginezo za criminal law perocedures zitachukua mkondo wake ikiwemo jela kama wakipatikana na hatia.
Sheria nyinginezo hazilali , uraia pacha ni fundamental rights za wanadamu na dunia inaelekea huko kwa sasa ...Amkeni enyi mawazo Mgando, ndondocha na wakaidi wa haki za raia, mko fofofo sana na dunia inakimbia mwendo kasi sana kwa haya mambo. Amkeni na Amkeni sana , fofofo za uraia pacha zinadumaza maendeleo yetu kama nchi...
 
Kama vile nawaona Wakenya...
Hawawezi kuwa wageni tena, watakuwa ni raia wa Tanzania waliopewa uraia kwa kuzingatia vigezo na masharti. Na wakiwa raia ndio watakuwa na haki sawa kama raia wengine, japo nimesema kunaweza kuwa na exceptions katika suala la nafasi za kisiasa, ingawa ukifanya hivyo inakuwa unapingana na Katiba
 
Hili la uraia pacha hatulitaki. Lilishindwa wakati wa kikwete na litashindwa hata sasa. Hatuhitaji raia mamluki wenye kuweza kua wazalendo kwa nchi nyingie au kuweza kutumiwa na adui wa nchi au kuweza kuisaliti nchi au kuihujumu uchumi wake. Hao wanaokupa uraia nao wana malengo yao.

Na wewe wape raia wa nje uraia wako kwa manufaa yako. It's that simple.

Hii inferiority complex itawaisha lini nyie watanganyika?

Mnaona nyie ni watu wa kuonewa na kuibiwa tu as though nyie hamuwezi kuonea na kuibia wengine.

Wekeza kwenye elimu na maarifa zalisha watu competent wanaoweza kushindana katika soko la kimataifa badala ya kujifungia ndani ukiogopa kuibiwa, kama huna maarifa utaibiwa tu hata ubane vp. Tayari sasa tunapigwa na hatuna uraia picha sijui mnazuia nini. Smh
 
Binafs nina watoto wanne Mocambique, na wote wamezaliwa huko, na mama zao ni raia wahuko, inawezekana vipi kwa wao kuja kusoma Tanzania kama raia wa Tanzania?

Nb. Sijui sheria ya nchi yetu inasemaje, kwa mtu asie raia kupata haki ya kupata elimu kama raia wa kawaida.
 
Suala hili linapaswa kufikiriwa haswa kwakuwa umiliki wa ardhi unahitaji kuwa raia, hii imesaidia kutunza ardhi ya tanzania na kuifanya kuwa ya bei inayohimilika mpaka sasa, wakiruhusu tu uraia pacha watajaa raia wa nchi mbali mbali kwa njia ya upacha na kuhodhi ardhi ya tanzania.

Ikibidi kuruhusu basi iwe kwa watu wenye asili ya tanzania tu, yaani mtu mwenye mzazi mtanzania au kuzaliwa tanzania lasivyo wachina na wengineo kutoka watahodhi ardhi ambayo ni muhimu kwa vizazi vijavyo.
 
Uraia pacha kwa Tanzania naona Kama ujinga tu uraia pacha unawafaa wazungu,wahindi na waarabu na wachina kwa sababu wana faida kwenye zao kiuchumi na kibiashara wakiwa Nchi sio zao

Mfano mhindi wa Tanzania ndio importer mkubwa wa bidhaa za India kuleta Tanzania

Mwarabu pia ndie importer mkubwa wa bidhaa za Uarabuni Kama mafuta nk kuleta Tanzania

Mchina vivyo hivyo

Diaspora wa kwetu wa nini kikubwa wanacho import kwenye Nchi zao waliko watafute masoko huko?

Uraia pacha kwa watanzania hawana maana yeyote ninkujaza tu mipassport tu kwenye kabati

Diaspora wetu was kitanzania Ni choka mbaya

Mhindi,mwarabu na mchina diaspora yeye huwaza tu namna ya kuleta bidhaa toka nchini kwake kwenye country of origin kuuza aliko tofauti na midiaspora mitanzania .Ni kelele tu ohhh tunataka uraia pacha kwa kipi Cha maana walichonacho wanachosaidia Nchi?
Kingine hao diasprora wenyeywe kwa wenyewe hawapendani huko ughaibuni,hawana umoja kama wenzetu wa bara Asia.Mtz kumpa dili za pesa mtz mwenzake ni ngumu sana
 
Uraia pacha ndio huo unakuja, mtabaki madungaembe mnahangaika eeh!

Tukutane bungeni waambieni madalali wenu wa uraia pacha akiwemo huyo Mulamula Waziri wa Mambo ya nje Mwambieni anasubiriwa kwa hamu bungeni ndipo atajua miaka aliyokaa USA Haina maana kuwa anaijua Tanzania

Mulamula peleka mswada Bungeni wa uraia pacha
 
Hulitaki wewe, na sisi tunalitaka. Kwa hiyo tufanyeje sasa?
Hawa watu wanatoka vichakani huko wao wanapinga kila kitu Yani pamoja na elimu zinazotolewa especially kuhusu faida ya uraia pacha bado tu anaibuka anasema hataki uraia pacha, sasa muulize hata kuvuka mpaka wa nchi ya mguu tu pale tarakea au Namanga au Tunduma kama amewahi kuvuka tu ataanza maelezo mengi yasiyo na maana.

Ujinga bado inasumbua hili taifa letu especially Hawa watu ambao wamekuwa mjini sababu ya kusoma wakaishia kupata kibarua kwa shida.
 
Binafs nina watoto wanne Mocambique, na wote wamezaliwa huko, na mama zao ni raia wahuko, inawezekana vipi kwa wao kuja kusoma Tanzania kama raia wa Tanzania?

Nb. Sijui sheria ya nchi yetu inasemaje, kwa mtu asie raia kupata haki ya kupata elimu kama raia wa kawaida.
Kama vyeti vyao vya kuzaliwa vinaonyesha wewe ndio baba, na wewe ni Mtanzania, basi haina tatizo, wao wanatambuliwa kuwa ni Watanzania hata kama wana passport za Mozambique kwa sasa. Unatakiwa kuwaombea passport za Tanzania ili uweze kuwaleta Tanzania na wataishi nawe bila Tatizo. Il a wakifika miaka 18 lazima wathibitishe uraia wao wa Tanzania na hiyo itabatilisha uraia wao wa Mozambique ambao huenda wanao.
 
Tukutane bungeni waambieni madalali wenu wa uraia pacha akiwemo huyo Mulamula Waziri wa Mambo ya nje Mwambieni anasubiriwa kwa hamu bungeni ndipo atajua miaka aliyokaa USA Haina maana kuwa anaijua Tanzania

Mulamula peleka mswada Bungeni wa uraia pacha
Hivi wewe, kwa upeo wa akili yako, unafikiri wabunge wa CCM wanaweza kupinga muswada wa serikali? Unafikiri wamesahau kwa nini na kwa namna gani walifanywa kuwa wabunge?

Nionyeshe Mbunge atakaethubutu kupinga muswada wa serikali akijua ubunge alionao aliupataje. Unafikiri lengo la Magufuli kupiga chini wabunge wote wa upinzani lilikuwa nini, na unafikiri limebadilika kwa kuwa sasa tuna Raisi Samia?

My friend, inabidi ujifanyie reality check katika kufikiri kwako juu ya Bunge la sasa
 
Kingine hao diasprora wenyeywe kwa wenyewe hawapendani huko ughaibuni,hawana umoja kama wenzetu wa bara Asia.Mtz kumpa dili za pesa mtz mwenzake ni ngumu sana
Kwa hiyo hicho ndio kiwe kigezo cha kutoruhusu uraia pacha?

Sasa wewe na wenzio ambao sio Diaspora mnapendana, hadi sasa wenzio wameshakupa pesa ngapi za kuwekeza nchini?
 
Suala hili linapaswa kufikiriwa haswa kwakuwa umiliki wa ardhi unahitaji kuwa raia, hii imesaidia kutunza ardhi ya tanzania na kuifanya kuwa ya bei inayohimilika mpaka sasa, wakiruhusu tu uraia pacha watajaa raia wa nchi mbali mbali kwa njia ya upacha na kuhodhi ardhi ya tanzania.

Ikibidi kuruhusu basi iwe kwa watu wenye asili ya tanzania tu, yaani mtu mwenye mzazi mtanzania au kuzaliwa tanzania lasivyo wachina na wengineo kutoka watahodhi ardhi ambayo ni muhimu kwa vizazi vijavyo.
Huo ni ubaguzi.

Watanzania mnang'ang;ania ardhi ambayo mnataka siku zote muione ikiwa mapori tu au mlime vishamba vya nusu eka na kuomba Mungu alete mvua kisha mnaishia kupata mazao afadhali hata ungenunua sokoni badala ya kupoteza nguvu na fadha kulima.

Sasa kama hao watu wa nje wakija na kufanya mapori yote yawe mashamba makubwa ya kumwagilia na kuzalisha mazao na kuendeleza majengo ya ofisi na makazi, tatizo liko wapi? Si watatuingizia fedha kwa kutufanya expoerters wa mazao na majengo?

Unajua Rais Carter wa Marekani alimwambiaje Nyerere? Kwamba nikuletee wakulima wa USA watano tu Tanzania, ukiwapa ardhi Tanzania haitakaa tena ije kutuomba mahindi ya njano na itakuwa iki-export chakula nje.
 
  • Thanks
Reactions: CES
Huo ni ubaguzi.

Watanzania mnang'ang;ania ardhi ambayo mnataka siku zote muione ikiwa mapori tu au mlime vishamba vya nusu eka na kuomba Mungu alete mvua kisha mnaishia kupata mazao afadhali hata ungenunua sokoni badala ya kupoteza nguvu na fadha kulima.
Hiyo ardhi ni benki ya akiba populaton inaongezeka wanakuwaq na eneo la kupanukia kuishio na kulima

Nenda nchi jirani tu hapo kenya ambako hakuna ardhi bure uone wananchi wanavyotaabika

Iache ibaki mapori kizazi kijacho kisipate shida ya ardhi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom