Usipotoshwe na watu wasioelewa maana na utaratibu wa kuwa na raia pacha. Angalia hapa maelezo ya uraia pacha na niulize swali lolote nitakujibu

Yaani wewe katika kufikiri kwako na conspiracy theory zako, katika ncho zoote Africa zinazoruhusu uraia pacha hilo hawajaliona ila wewe tu ndio una busara ya kuliona? Angalia ramani hapa chini hadi sasa ni nchi ngapi Afrika zimebaki madungaembe ya uraia pacha kwa kuwa zina mawazo kama unayosema. Yaani hawa wote ni peke yako ndio ukabaki na pua, basi wewe ndio utakaekuwa mwenye ulemavu wa pua. Fikiria hilo kwa makini.

View attachment 1883768
In short hujielewi Tanzania is not a photocopy machine or copy cat of any country.That is why we are called Tanzania hatuitwi majina ya hizo Nchi.Hatuitwi Kenya or Rwanda or South Africa etc

We are not copy cats please
 
Swali limeongezwa

15. Hadi sasa, ni nchi ngapi katika Afrika zinaruhusu uraia pacha?
Ni rahisi zaidi kuongelea ni nchi ngapi katika Afrika haziruhusu uraia pacha kuliko ni ngapi zinaruhusu uraia pacha, kwa kuwa karibu nchi zote za Afika sasa zinaruhusu uraia pacha isipokuwa Tanzania, Ethiopia, Eritrea, DRC, Malawi, Zambia, Liberia, Lesotho, Sao Tome na Cameroon, kama ramani hapa chini inavyoonyesha.
 
Are you sure we are not copycats? Kwani vitu vingapi tumeiga hadi sasa? Hata kutumia toilet paper tuliiga.
 
Wait Ni wao na Sisi Tanzania Ni Sisi Tanzania Sio copy cat please.Usitugeuze mashine ya photocopy.
 
Yaani wewe katika kufikiri kwako na conspiracy theory zako, katika ncho zoote Africa zinazoruhusu uraia pacha hilo hawajaliona ila wewe tu ndio una busara ya kuliona? Angalia ramani hapa chini hadi sasa ni nchi ngapi Afrika zimebaki madungaembe ya uraia pacha kwa kuwa zina mawazo kama unayosema. Yaani hawa wote ni wajinga wa kuuza nchi zao ila sisi ndio tunajua.

Unajua, siku ikitokea Watanzania wote wakapoteza pua zao na kutokuwa na pua, na wewe peke yako ndio ukabaki na pua, basi wewe ndio utakaekuwa mwenye ulemavu wa pua. Fikiria hilo kwa makini.

View attachment 1883768
Bado una hoja za Wengi wape kumbe. Naiona Mozambique hapo, Somalia pia na wengineo pia. Sasa labda mtuambie tunatofautiana nao nini na kwanini?

Simple logic ni hii.... Trump atapewa stahiki sawa na Mtanzania yeyote ndani ya Tz, na vile vile wale jamaa was Richmond/EPA/ESCROW nao pia watapewa (Kiini macho cha stahiki za kuwa Mmarekani) Umri wako unatosha kutafakari matokeo katika pande zote.

Msikaririshwe maneno vinywani mwenu na kuimba kila Leo dhana ya Conspiracy Theory.
 
Uraia pacha kwa Tanzania naona Kama ujinga tu uraia pacha unawafaa wazungu,wahindi na waarabu na wachina kwa sababu wana faida kwenye zao kiuchumi na kibiashara wakiwa Nchi sio zao

Mfano mhindi wa Tanzania ndio importer mkubwa wa bidhaa za India kuleta Tanzania

Mwarabu pia ndie importer mkubwa wa bidhaa za Uarabuni Kama mafuta nk kuleta Tanzania

Mchina vivyo hivyo

Diaspora wa kwetu wa nini kikubwa wanacho import kwenye Nchi zao waliko watafute masoko huko?

Uraia pacha kwa watanzania hawana maana yeyote ninkujaza tu mipassport tu kwenye kabati

Diaspora wetu was kitanzania Ni choka mbaya

Mhindi,mwarabu na mchina diaspora yeye huwaza tu namna ya kuleta bidhaa toka nchini kwake kwenye country of origin kuuza aliko tofauti na midiaspora mitanzania .Ni kelele tu ohhh tunataka uraia pacha kwa kipi Cha maana walichonacho wanachosaidia Nchi?
Kwani tanzania ina kitu gani kikubwa chakupeleka uko nje kwenye hizo nchi ambazo kuna watanzania.kwahito hapo tatizo nila nchi lakini ata hivyo tunaweza tusione umuhimu wao kwasababu milango haijafunguliwa ipasavyo.tungeweka kwanza hizo taratibu vizuri alafu tukafanya tasmini.
 
Are you sure we are not copycats? Kwani vitu vingapi tumeiga hadi sasa? Hata kutumia toilet paper tuliiga.
Labda wewe ndie unatumia Toilet paper Mimi natumia maji Toilet paper ukijisaidia haha kubwa unabaki na kinyesi ndani inzi watakufuata .Mimi nachamba kwa maji ndio yanasafisha vizuri . Chooni nikitoka hakuna inzi kunifuata Wala harufu.Toilet paper inabakiza kinyesi kwenye makalio na harufu maji yanamaliza vyote

Vitu vya kuoga na kuwa photocopy vitaachia Nchi kinyesi na harufu.That is why Tanzania we don't want to be copy cats .Mtahangaika sana ila uraia pacha mtasubiri sana

Wewe copy cat wa toilet paper utajijua.
 
Hili la uraia pacha hatulitaki. Lilishindwa wakati wa kikwete na litashindwa hata sasa. Hatuhitaji raia mamluki wenye kuweza kua wazalendo kwa nchi nyingie au kuweza kutumiwa na adui wa nchi au kuweza kuisaliti nchi au kuihujumu uchumi wake. Hao wanaokupa uraia nao wana malengo yao.
Umesoma kweli mada ukaielewa au umecoment tu?.
 
Kwa miaka kibao uzoefu uko wazi watanzania walioko nje hawasaidii viwanda vya Tanzania kuuza bidhaa za Tanzania kwenye nchi zao Kama wahindi na waarabu .kikubwa Ni kuangalia faida ya diaspora kwenye uchumi mkubwa wa movement of goods kwenda soko kule aliko sio vihela vidovidogo vya remmittance vya pesa za rambi rambi na michango ya harusi

Wahindi na waarabu tunao miaka nenda Rudi lakini wanachofanya Ni kutuletea tu bidhaa zao .Sisi soko lao la bidhaa zao tu kwa asilimia kubwa.miaka nenda Rudi.Mchina kaja ndio kabisa katufanya gulio la bidhaa zake.Ukimpa uraia pacha ana kipi kikubwa kwa Nchi.? Ni Ku drain tu our forex kununua bidhaa kutoka his country of origin at our forex expense Wahindi,waarabu,wachina etc hutoa uraia pacha wakijua what will happen kwa viwanda vyao na bidhaa zao.
Huna hoja zaidi ya chuki tu. Viwanda gani unazungumzia?
 
Kwani tanzania ina kitu gani kikubwa chakupeleka uko nje kwenye hizo nchi ambazo kuna watanzania.kwahito hapo tatizo nila nchi lakini ata hivyo tunaweza tusione umuhimu wao kwasababu milango haijafunguliwa ipasavyo.tungeweka kwanza hizo taratibu vizuri alafu tukafanya tasmini.
Viko kibao mazao yetu yanaozea mashambani ,madini yako kibao wageni ndio huchukua kuuza kwao ,bidhaa za viwandani kibao Diaspora mbona kimyaaa halafu ooh tunataka uraia wa Nchi mbili kwa lipi? Hivyo vipesa vyenu vya michango ya harusi na rambi rambi?
 
Are you sure we are not copycats? Kwani vitu vingapi tumeiga hadi sasa? Hata kutumia toilet paper tuliiga.
Sasa ndio hoja unazofikiri zinaweza shawishi wengi kuunga mkono Uraia Pacha? Kwamba kwa vile vipo tulivyocopy na hili nalo tubebe tu?

Hatutaki! Hoja zako ni dhaifu, Dunia ina maelfu ya Sera na Itikadi, Kwanini usihoji kuwa hatukuchukua zote? Na kwanini iwe Uraia Pacha tu?

Hatutaki! Bakini na mkiitacho Usasa. Endeleeni kupiga poyoyo za hapa na pale kwa wakati huu. Muda bado.
 
Labda wewe ndie unatumia Toilet paper Mimi natumia maji Toilet paper ukijisaidia haha kubwa unabaki na kinyesi ndani inzi watakufuata .Mimi nachamba kwa maji ndio yanasafisha vizuri . Chooni nikitoka hakuna inzi kunifuata Wala harufu.Toilet paper inabakiza kinyesi kwenye makalio na harufu maji yanamaliza vyote

Vitu vya kuoga na kuwa photocopy vitaachia Nchi kinyesi na harufu.That is why Tanzania we don't want to be copy cats .Mtahangaika sana ila uraia pacha mtasubiri sana

Wewe copy cat wa toilet paper utajijua.
Kwani maji siyo copycat ya mwarabu? Huna hoja hata kidogo. Hata huko bungeni una hoja gani zaidi ya ujinga ujinga tu? Hopeless. Kikubwa mlichonacho ni roho kutu tu na ndiyo maana hatuendelei kama Taifa miaka nenda rudi tokea uhuru.
 
Hata simenti tu mbona wapakstani walioko Tanzaniandio waagizaji wakubwa wa simenti toka Pakistan?
Simenti ipelekwe wapi? Hapa nchini yenyewe haitoshelezi. Nyie wazalendo si mgefungua hivyo viwanda ndo kisha muwalaumu diaspora? Huwezi kutaja hivyo viwanda unasema eti “hata simenti”. Matatizo yenu ya kushindwa kujenga uchumi imara wa kuweza ku export unasingizia diaspora eti hawana maana labda waarabu na waindi.🤦🏾‍♂️
 
Sasa ndio hoja unazofikiri zinaweza shawishi wengi kuunga mkono Uraia Pacha? Kwamba kwa vile vipo tulivyocopy na hili nalo tubebe tu?

Hatutaki! Hoja zako ni dhaifu, Dunia ina maelfu ya Sera na Itikadi, Kwanini usihoji kuwa hatukuchukua zote? Na kwanini iwe Uraia Pacha tu?

Hatutaki! Bakini na mkiitacho Usasa. Endeleeni kupiga poyoyo za hapa na pale kwa wakati huu. Muda bado.
Lengo sio kushawishi kuunga mkono uraia pacha. Lengo ni kufanya watu wajue ukweli kuhusu uraia pacha ndio waunge mkono au kutounga mkono, sio kuleta sababu zisizo na mshiko za kuunga au kutounga wakati hawajui hata maana ya uraia pacha na kusema vitu kama matajiri wote watanunua ardhi yetu au raia pacha watahujumu jeshi wakiingia JWTZ au siku moja tutakuwa na raisi raia pacha, au kukataa kwa sababu za wivu tu. Naona wewe umekalia upande wa wivu tu sioni pointi za kupinga unazotoa
 
Bado una hoja za Wengi wape kumbe. Naiona Mozambique hapo, Somalia pia na wengineo pia. Sasa labda mtuambie tunatofautiana nao nini na kwanini?

Simple logic ni hii.... Trump atapewa stahiki sawa na Mtanzania yeyote ndani ya Tz, na vile vile wale jamaa was Richmond/EPA/ESCROW nao pia watapewa (Kiini macho cha stahiki za kuwa Mmarekani) Umri wako unatosha kutafakari matokeo katika pande zote.

Msikaririshwe maneno vinywani mwenu na kuimba kila Leo dhana ya Conspiracy Theory.
Trump atapewa uraia wa Tanzania kwa msingi gani? Tuanzie hapo kwanza, na labda rudi ukasome thread.
 
Kwani maji siyo copycat ya mwarabu? Huna hoja hata kidogo. Hata huko bungeni una hoja gani zaidi ya ujinga ujinga tu? Hopeless. Kikubwa mlichonacho ni roho kutu tu na ndiyo maana hatuendelei kama Taifa miaka nenda rudi tokea uhuru.
Nadhani tungemuuliza kabla ya kutumia maji au toilet paper babu zetu walikuwa wanatumia nini!🤣🤣🤣
 
Bado una hoja za Wengi wape kumbe. Naiona Mozambique hapo, Somalia pia na wengineo pia. Sasa labda mtuambie tunatofautiana nao nini na kwanini?

Na kwa nini utaje Somalia na sio South Afrika, Kenya, Rwanda, Botswana, Uganda, Ghana?

Nimesema, ukiona wengi wamekubali kitu na ni wewe tu ndio umebaki, jiulize kwa makini kwa nini wengi wamekubali na wewe peke yako ndio unakataa. Usikute huna akili timamu. Ndio maana tuliacha siasa za Ujamaa kwa sababu tulibaki kama kisiwa na zikawa zinatuharibia, japo ulikuwa msimamo wetu.

Tuko enzi za globalization, you either swim with the crowd or get left behind.
 
Wait Ni wao na Sisi Tanzania Ni Sisi Tanzania Sio copy cat please.Usitugeuze mashine ya photocopy.
Huwa mara nyingi siungi mkono kaulu za Mulamula, lakini sasa naona amewakata kilimi watu wenye maoni yako.

Mweleko mpya kwa uraia pacha​

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Serikali inalifanyia kazi suala la uraia pacha na kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha, litakuwa limepatiwa ufumbuzi.

Pia, alisema wizara yake iko tayari kuwawezesha Watanzania waishio nje ya nchi (diaspora) kupiga kura endapo watapata ridhaa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa sababu ni rahisi kwa kutumia teknolojia.

Balozi Mulamula alisema hayo katika mahojiano maalumu na wahariri wa gazeti hili alipotembelea Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam jana kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.

Alisema Serikali ya Awamu ya Sita imetambua suala la uraia pacha linakwenda sambamba na ushiriki wa diaspora; na watu wengi, wakiwamo wabunge wamekuwa wakionyesha utayari wao.

“Tukiwa bungeni kuna mbunge mmoja aliondoa shilingi mpaka tumpe majibu, wakati ule zamani tukienda bungeni walikuwa wanasema ‘bwana wee usituambie habari za diaspora, wanakula kuku kwa mrija, wachague wanataka wapi, huwezi kupata huku ukapata kule’. Sasa mtazamo umebadilika, wao ndio wanaotaka,” alisema Balozi Mulamula.

“Wabunge wengi wametoka diaspora, nikawaambia kama mnalitaka hili basi, na ninyi ni watunga sheria, sisi tunalifanyia mkakati wa kisera, lakini likija kwenye sheria ninyi wabunge ndiyo mtusaidie tuipitishe.”

Balozi Mulamula alisema tangu akiwa balozi, msisitizo wake ni kwamba huwezi kumwondolea mtu haki ya kuzaliwa katika nchi aliyozaliwa.

Alisema Watanzania wengi walio nje ya nchi wamekwenda kutafuta maisha na wako kwenye fani tofauti, ukiwamo udaktari na biashara, hivyo, wana mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa.

“Ningekuwa na uwezo ningelimaliza hata jana, ingekuwa imenipa amani sana, hasa kukuza ushiriki wa diaspora. Mtazamo umebadilika, si kama huko nyuma, kwa hiyo mimi naamini kabla ya mwisho wa mwaka huu, tutakuwa tumelipatia suluhu hili la uraia pacha,” alisema.

Alisema suala la uraia pacha lilitakiwa lipite katika mchakato wa mabadiliko ya katiba, lakini ilionekana si suala la kuingia kwenye katiba, bali kuliwekea sheria maalumu kama zilivyofanya Ethiopia na India.

“Kubadilisha Katiba ni mlolongo mrefu, lakini ikishaingia kwenye katiba halafu ukaja utawala mwingine hauitaki, unaitoaje? Kwa hiyo kukiwa na sheria inawalinda zaidi.

“Sasa tumesema tunavyoainisha hii sera yetu ya mambo ya nje, tuko kwenye mkakati wa kuweza kuja na programu maalumu wanayoita hati maalumu zinazowatambulisha Watanzania walioko nje,” alisema Balozi Mulamula.

Suala la uraia pacha ni miongoni mwa mambo yaliyoibuliwa na wananchi wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba (CRC) inakusanya maoni ambayo yaliwekwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba kisha kupitishwa kwenye Katiba inayopendekezwa.

Ibara ya 72 ya Katiba Pendekezwa inasema: “Bila kuathiri masharti yaliyomo kwenye sura hii, mtu yeyote mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri ya Muungano, atakuwa na hadhi maalumu kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.”

Wadau wazungumza

Akizungumzia suala la diaspora, mbunge wa viti maalumu, Neema Lugangira alisema aliishauri Serikali bungeni kutunga sera maalumu ya diaspora itakayoondoa changamoto zinazowakabili kama kutoruhusiwa kumiliki ardhi na kurithi mali.

Hata hivyo, alisema suala la uraia pacha lina changamoto, hivyo, alipendekeza Serikali kuja na jambo la haraka la kuwapa hadhi maalumu diaspora kama ambavyo India wamefanya kupitia hati maalumu za diaspora zinazojulikana kama People of India Origin (PIO).

“Kwa kuwa jambo la uraia pacha lina changamoto zake, nilipendekeza tuje na utaratibu wa kuwapa hadhi maalumu, lakini ili liwezekane lazima tuwe na sera ya diaspora,” alisema mbunge huyo anayewakilisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs).

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema nchi zilizoruhusu uraia pacha duniani kote zimepiga hatua kiuchumi kwa sababu zimewajengea diaspora kujiamini na kupata haki kama raia wa nchi zao.

Mbatia alitolea mfano Kenya akisema mwaka jana fedha zilizotoka kwa diaspora kwenda Kenya zilikuwa ni Dola 4.4 bilioni za Marekani ukilinganisha na Dola 380 milioni ambazo diaspora walirudisha hapa Tanzania.

“Ili kujenga confidence ya diaspora, uraia pacha ni muhimu. Kutojiamini ndiyo sababu ya kuwekea vikwazo suala hili, tuangalie mizania ya kiuchumi zaidi ili tufanye maamuzi sahihi,” alisema Mbatia.

Diaspora kupiga kura

Balozi Mulamula alisema suala la diaspora kupiga kura linahitaji utaratibu na miundombinu, hasa kwa kutumia teknolojia kama zinavyofanya nchi nyingine zilizofanikiwa kwa kutumia mifumo ya kimtandao.
 
Hili la uraia pacha hatulitaki. Lilishindwa wakati wa kikwete na litashindwa hata sasa. Hatuhitaji raia mamluki wenye kuweza kua wazalendo kwa nchi nyingie au kuweza kutumiwa na adui wa nchi au kuweza kuisaliti nchi au kuihujumu uchumi wake. Hao wanaokupa uraia nao wana malengo yao.
Mulamula amekujibu mtu mwenye mawazo mgando kama wewe. Sasa kama hutaki uraia pacha hamia Eritrea! Mmetukera muda mrefu sana watu nyie, sasa mmeona hii ndhi sio yenu peke e

Similar Discussions

Back
Top Bottom