Ninadaiwa Tala, Branch na M-pawa. Nisipowalipa watanifanya nini?

jamani mimi tala ndo wananisumbua . nilifikia kiwango cha laki mbili nilipe alafu waniongezee mkopo cha ajabu nililipa wakanikata mkopo nikawa siez kuongeza mkopo wakanipa laki moja badala ya laki mbili na nusu hapi sikuwalipa tena laki yao wamebaki kunitisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe upo timamu kweli??? Unataka kuwalipa tala??? Hiiiiiiii yaani mkopo ambao nalipa ni wa bank tu ....labda na mtu binafsi nikimkopa nitamlipa ila sio tala ...branch ...airtel timiza Mara tigo nivushe hiii siwalipi ng'o hawa viumbe .....

Sent using Jamii Forums mobile app
Tigo wananidai laki moja ina miaka karibu miwili Sasa.Ila kwa Airtel ukiwa na deni hiyo laini isipite hela yeyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulivyojiunga uliconnect account yako na facebook account ndio huko utaanikwa kila mtu akuone

ACHA UJINGA ,UNAJISIFIA UJINGA
 
katika nchi isiyo jua kukopesha tanzania itakuwa inaongoza.nimejifunza mengi kwa wenzetu sijui tulikosea wapi.
kama unaweza kukopa unajiwekea mda na hata ukishindwa unaweza kuomba mda na kuendelea na kulipa hata kukopa.
Dizaini ya mtoa mada ukimkopesha na Urafiki utaisha na hawez rudisha.
Watu wanashabikia asililipe lakini ni kukosa kujitambua.
Yaani akili ya kujisimamia ni ndogo miongoni mwa watanzania wengi kama si wachache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nilivyoelekeza hapo juu, nimekuwa mfanyabiashara mdogo muda mwaka sasa tangia nijiunge na mikopo ya tala na kufikia mkopo wa laki 3 na nusu nikachukua biashara nikapeleka Morogoro.

Nikakuta soko sio zuri hivyo mtaji ukayumba.

Nlivyowaelekeza TALA wakasema hawanielewi tulishakubaliana hiyo pesa irudi kwa muda wa mwezi. Mpaka sasa nimezidisha siku 15 wameongeza riba asilimia 10.

Najuta mpaka sasa nimeomba wanifahamishe ofisi zao zilipo labda niende nikakutane na mkuu wao nimueleze yaliyonikuta wanasema niwasiliane kupitia facebook au sms za kawaida.

Hivyo naomba kama kuna yeyote anajua ofisi zao zilipo anielekeze niwafuate.
Hapa ndiyo mtu unajua jeuri ya mkopaji anayekopa bila dhamana! Wakati wa kukopa anakuwa na ahadi na lugha nzuriiiii lakini wakati wa kurudisha hakosi sababu. Kweli kukopa ni harusi lakini kulipa ni matanga. Mimi nadhani unapokopa kuna masharti ya mkopo ambayo unayakubali. Haijalishi umeugua au umepigwa na radi na meno yote yakang'oka, ni lazima uyafuate. Mengine ni kiswahili kisicho na na maana. Ulipokuwa unakopa ulidhani biashara ni faida tu? Anyway, hiyo kampuni nayo ni mbumbumbu wacha wapigwe! Tangu lini ukamkopesha mtu bila dhamana kwenye haya mazingira na utamaduni wetu wa kiafrika akakosa sababu wakati wa kulipa?
 
Kama nilivyoelekeza hapo juu, nimekuwa mfanyabiashara mdogo muda mwaka sasa tangia nijiunge na mikopo ya tala na kufikia mkopo wa laki 3 na nusu nikachukua biashara nikapeleka Morogoro.

Nikakuta soko sio zuri hivyo mtaji ukayumba.

Nlivyowaelekeza TALA wakasema hawanielewi tulishakubaliana hiyo pesa irudi kwa muda wa mwezi. Mpaka sasa nimezidisha siku 15 wameongeza riba asilimia 10.

Najuta mpaka sasa nimeomba wanifahamishe ofisi zao zilipo labda niende nikakutane na mkuu wao nimueleze yaliyonikuta wanasema niwasiliane kupitia facebook au sms za kawaida.

Hivyo naomba kama kuna yeyote anajua ofisi zao zilipo anielekeze niwafuate.
Usiende wewe kausha tu.
Utajikamatisha kizembe sana wakati waliokopa Ni wengi sana na hawalipi na hakuna kilichotokea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulizeni mioyo yenu,hata nchi inadaiwa,kwani hamjawahi jiuliza tukishindwa kulipa deni la Taifa na nchi ikapigwa mnada tutaenda kuishi wapi???

Kama hilo hamuliwazi kwa nini muteseke na hayo madeni yaliyo mukononi mwenu?,tafuteni pole pole mtalipa pole pole,hakuna asiye daiwa,
Mtu unadaiwa elfu 30 unaanza kuhaha kwa msj za TALA na BRANCH, mimi wala siwezi pata tabu,dawa ni kuwalipa tu mana ukitumia chao,ukipata lipa baasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom