Usipitwe na Makala Hii ya Mayage S. Mayage-Raia Tanzania!

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,432
1,250
Wiki iliyopita nilipata wasaa wa kusoma Gazeti jipya lililoingia mtaani kwa kishindo. Si Gazeti jingine bali Raia Tanzania. Ni Gazeti Dada la Raia Mwema. Lina safu zinazovutia na waandishi makini (nisijue kama kweli na wao wote hutenda wanachokiandika!)

Makala ya kwanza iliyonivutia kwenye Raia Tanzania ilikuwa ya Mwandishi Mayage S. Mayage. Makala hii ilikuwa ikotoa rejea ya makala “Zitto, urais 2015 kwa chama gani?” Toleo la wiki jana halikuweza kukamilisha na kuhitimisha makala, itaendelea wiki hii.

Mwandishi Mayage anatoa yake ya moyoni juu ya watu wawili wanaojitaanabaisha kama Masterminds of Tanzanian Politics. Hawa si wengine bali Rostam Aziz (aliyekuwa Bosi wake Mayage) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Ndugu Zitto Kabwe. Anaeleza hujuma ya Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais kwa Mgombea wa Ubunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CCM. Analionyesha tendo hili kuwa la maksudi na la kupangwa ambalo lilijulikana kwa Rostam Azizi na Zitto Kabwe. Pia mwandishi anatoa uthibitisho wa matukio na kauli mbalimbali kuonyesha uwili usiotenganishwa kati ya hawa "magwiji wa siasa za Tanzania"

Ni makala ya kupevua macho nashauri kila atakayepata Gazeti la Raia Tanzania ajaribu kuisoma kwa umakini.
 
Last edited by a moderator:

TECHMAN

JF-Expert Member
May 20, 2011
2,657
1,250
wengine sio watu wa magazeti humu, kama unapenda tusome hiyo tuwekee hapa zaidi ya hapo pita kule.
 
Pagija

JF-Expert Member
Dec 6, 2013
380
0
Wiki iliyopita nilipata wasaa wa kusoma Gazeti jipya lililoingia mtaani kwa kishindo. Si Gazeti jingine bali Raia Tanzania. Ni Gazeti Dada la Raia Mwema. Lina safu zinazovutia na waandishi makini (nisijue kama kweli na wao wote hutenda wanachokiandika!)

Makala ya kwanza iliyonivutia kwenye Raia Tanzania ilikuwa ya Mwandishi Mayage S. Mayage. Makala hii ilikuwa ikotoa rejea ya makala "Zitto, urais 2015 kwa chama gani?" Toleo la wiki jana halikuweza kukamilisha na kuhitimisha makala, itaendelea wiki hii.

Mwandishi Mayage anatoa yake ya moyoni juu ya watu wawili wanaojitaanabaisha kama Masterminds of Tanzanian Politics. Hawa si wengine bali Rostam Aziz (aliyekuwa Bosi wake Mayage) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Ndugu Zitto Kabwe. Anaeleza hujuma ya Mwenyekiti wa CCM na Mgombea Urais kwa Mgombea wa Ubunge wa Kigoma Kaskazini kupitia CCM. Analionyesha tendo hili kuwa la maksudi na la kupangwa ambalo lilijulikana kwa Rostam Azizi na Zitto Kabwe. Pia mwandishi anatoa uthibitisho wa matukio na kauli mbalimbali kuonyesha uwili usiotenganishwa kati ya hawa "magwiji wa siasa za Tanzania"

Ni makala ya kupevua macho nashauri kila atakayepata Gazeti la Raia Tanzania ajaribu kuisoma kwa umakini.
Mkuu naona uko kibiashara zaidi..........unauza raia Tanzania, sawa ila mwambie mwandishi aache uongo kwani Zitto kaibuka kwenye siasa za Tanzania katika kipindi cha isiyozidi 8, sasa leo awe mastermind wa wa siasa za Tanzania. Ila Hongera Mayage kishakuona atakupa malipo yako. Peleka hii kwenye matangazo ya Biashara.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom