Usipige Picha Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usipige Picha Tanzania

Discussion in 'Entertainment' started by Sikonge, Apr 1, 2008.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wana Mtandao.
  Nilikuwa juzi juzi Tanzania na kufurahia kuwa nyumbani baada ya miaka mingi. Huku nikiwa na camera yangu panasonic na cadi zangu kama 3 nilikuwa tayari kupiga picha picha na kuchukua VIDEO za kwetu ili nikirudi Ulaya basi niwaonyeshe Wazungu kwetu kulivyo na kuwaambia ni vema waende huko hasa ukichukulia Tanzania ni nchi ya Kitalii. Ehh, ikawa nikifika baadhi ya sehemu ninaambiwa usipige picha. Sehemu moja wapo ikiwa nyumba ya makumbusho kwa nje. Wakaniuliza eti camera yangu ni aina gani nikasema Panasonic. Wakauliza ni Digital au siyo nikasema kwani kwa dunia hii tofauti iko wapi? Wakasema bei. Nkaanza kuambiwa bei ya kupiga majengo, udongo na miembe kwa nje huku ukiwa ndani ya wigo wa nyumba ya makumbusho. Nikasema na ndani si itakuwa balaa na wao wakasema ni bei ile ile.

  Sasa ukiacha kukua kwa technology basi ushamba wa wenzetu kwa kweli unatia kinyaa. Sehemu hamna kibao wala maneno USIPIGE PICHA, sasa ukatoa kamera na kupiga maneno. Pia kwa sasa vitu vya nje unaweza kuangalia kila kitu kwenye GOOGLE EARTH. Mtu anaweza kuingia na miwani kumbe ni camera. Unaweza kuona mkoba au kitabu kumbe ndani ni camera. Wenye hela zao wanaweza kuomba kupigiwa picha sehemu yoyote za setelite na watazipata picha safi tu. Sasa haya ya kunyanyasana eti usipige picha si yamepitwa na wakati? Sasa watalii wakija na kupigwa mkwara je watarudi tena? Mbona mtu ukiwa Ulaya, Asia au America hasa mijini basi waweza kupiga picha kila sehemu na hakuna anayekunyanyasa?

  Naomba kama kuna wabunge humu ndani waangalia hili swala na ikibidi IPIGWE marufuku kumnyanyasa mtu kwa kupiga picha mjini. Na kama kuna jengo au sehemu hawataki wapigwe basi waombe ruhusa na sababu ya msingi ya kukataa mtu asipige pale picha. Kama si ya msingi basi akataliwe. Lazima kutangaza nchi kwa kila hali. Huu ushamba ulikuwa mjini karne ya 20, ila sasa hauna tena maana.
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Pole sana ndugu yangu, hii ndiyo BONGOland! Yaani siku hizi watu wanadhani picha ni mali. Nilikuwa nawaambia wale macurator wa huko Makumbusho kwamba wengine tumebahatika kufika katika museum kubwa tu za France na Italy na USA, na unapiga picha nje na katika baadhi ya maeneo uanweza ukaambiwa usipige picha kwa kutumia flash. Hata Last Supper ya Leonardo Da Vinci nilienda kuiangalia - the original one in Italy na tuliipiga picha bila tatizo ingawa bila flash! Sasa hapa ndo tunajifanya tunajua kuzuia picha, alafu uliza hizo pesa zinatumika vipi? Watapata kigugumizi.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Susuviri, utafikiri ulikuwepo. Sasa mie sikuwa na muda na nilitaka kupiga tu majengo kwa nje. Ni kweli kabisa jamaa huwa hawaruhusu FLASH. Hii hata uwe na pesa kiasi gani. Sasa kule kwetu ulimbukeni kweli unatisha. Wanafikiri kila mzungu ni tajiri na kumbe wengine ni jua kali tu kama sisi ila anahamu ya kuja Africa na akifika huko na mapenzi yake yote wanafikiri ni BUZI, basi hao wako tayari kuchuna. Niliwaambia MTAKUFA MASIKINI kwa mwendo huu. Hongera kwa kufika na kuona kazi ya Da Vinci. Mie si mpenzi sana ingawa pia nilishafika na kusikia hilo Tangazo la NO FLASH. Labda kuna viongozi wa juu watasoma hili na kulifanyia kazi maana kwa kweli hii njaa inatuvua sasa nguo.
   
 4. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2008
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  duh!! wanachaji!!!this is terrible!! ila nna wasiwasi, hawakuwa watoto wa mjini kweli hao??? manake bongo bwana lolote linawezekana.hako kanchi ketu kuna vifisadi vidogovidogo kila kona
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mzee wa jicho moja, habari za Izrael?
  Hawa akina mama walikuwa wamesimama na ticket zao kwa watu wanaoingia ndani basi unalipia. Sasa sijui ukipiga picha unapata risiti gani. Sikuwa na muda kwani siku ya jumatano ndiyo nilikuwa naondoka na mvua iliyonyesha sikuwa na hamu ya kubishana na PUMBAVU, watu watashindwa kuona tofauti.
  Next time ntawaingilia asubuhi na timu yangu ya matapeli. Tutasumbuana nao siku nzima hadi somo lieleweke. Ikibidi hadi kwa waziri tutafika siku hiyo huku tukiwa na waandishi wa habari kama wapambe na timu ya watu wa HAKI ZA BINADAMU. Upuuzi mwingine inabidi kuushambulia kwa juhudi zote.
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Apr 1, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  SIRI
  CONFIDENTIAL ! - !


  Ndiyo Tanzania yetu! Kila kitu siri...

  Hawajui tunaonwa hadi kila kifanyikacho ikulu. Wataalam wetu wa Ikulu nao sijui kama wako aware na hili. Aibu nyingine ni jengo nililokuta linajengwa MBELE ya ofisi za Usalama wa Raia ambalo ni refu kuliko ofisi hizo ambako bila shaka ukiwa juu kabisa na ukawa na kiona mbali unaweza kumwangalia IGP akiwa ofisini kwake. Lakini ukiwa ofisini kwake ukataka kumpiga picha huenda akakataa kwakuwa ni sehemu NYETI.

  Hahaha teknolojia inaleta balaa Tanzania!


  Kazi ipo, tena si ndogo
   
 7. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2008
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45

  habari za huku nzuri mkuu, a bit dry day at 66F.hao watu inabidi uwafate wakupe majibu mazuuuri.manake hai-make sense kabisa kuwachaji watu pesa kwa kupiga picha, kwanza hiyo ni moja ya njia ya kutangaza utalii.ukirudi ukawakomalie bwana
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Invisible,
  Haya ndiyo maajabu menyewe. Hii inanikumbusha mfalme aliyetaka kushonewa VAZI lisiloonekana. Siku alivaa wote wakasifu lilivyokali. Hadi katoto kalipotoka na kusema huku kakicheka MFALME YUKO UCHI. Sijui hawa watu husubiri waambiwe na wao mko uchi. Labda kwa upande fulani inabidi niisifu JF kuwa na UDOGO wake, inajitahidi saana kuwaambiwa viongozi wetu na watanzania kwa ujumla MKO UCHI. Keep it up JF.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kuna viwili hapa:
  1) Kutokujua masuala ya biashara. Kuna idara za serikali bado wanauza fomu! Hii hapa kutoka Tanzania Investment Centre.


  Tunakamua hata pale ambapo hapana haja. Wenzao fomu zipo kwenye mtandao, una'download' kwa kadri unavyotaka. hawa jamaa wanataka dola 100 ingawa kwenye homepage wameonyesha kuna fomu za ku'download'.

  Hapo makumbusho unaambiwa ukiwa na camera ya kawaida ni bure lakini digital wanataka mpango! Halafu wanalalamika watalii hawaji. Watakujaje kwa mpango huu? Watu wanaenda mahali mara nyingi kutokana na simulizi za wenzao na picha wanazoleta kutoka huko. Hili wenzetu hawalioni. Nyumba zinaanguka kwa kukosa matengenezo na akitokea mwenye mapenzi nazo wanaanza kumbughudhi!

  2. Kuendelea kupigana vita na makaburu. Huu wakati wa Google Earth kweli unakaa kuzuia watu kupiga picha daraja la salenda! maaskari sasa wamefanya mradi. Kwa wenzetu hata airport wewe piga tu maana wanajua hamna cha ajabu utakachoweza kufanyia wakati picha zimejaa kwenye mtandao. kwa mtazamo huu, hilo ongezeko la utalii tutalisikia redioni.
   
 10. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Fundi, umenikumbusha ishu ya airport! Eti tulikuwa tunamwaga mtu na kupiga picha, askari akaja kutuambia eti haturuhusiwi kupiga picha na kwamba eti utawala lazima wapewe taarifa, blablah. Tulimtoa nduki huyo askari mpaka akaamua kupiga patroli kwingine. Yaani ujinga huu wa kuona picha ni mradi ni ujinga!

  Suala la kuuza fomu ni vichekesho lakini nadhani itabidi tuanzishe mada nyingine maana tukianza kuangalia fomu zinazouzwa Bongo utacheka!
  Lakini vitu vyoet hivi vinatokana na fikra za zamani na ujanja wa watoto wa mjini!
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Apr 1, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  jamani kuna sheria ambazo bado ziko vitabuni ndio vimesababisha mambo haya. Miye nakumbuka pale Chuo cha Ualimu Korogwe miaka hiyo kulikuwa na bango kubwa ati "Hairuhusiwi kupiga Picha"! Sijui tulikuwa tunaficha vitu gani kwenye vyuo vya walimu.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Fundi mchundo mwenzangu,
  Umesema juu ya DARAJA la Sarenda na kwa hasira nimeingia kwenye GOOGLE EARTH na kuliona. Tena mjinga mmoja ajiitaye Aman kawewa na picha Hihiiii :) Nafikiri mmesema kweli kuwa kuna mawili yaani moja ni ushamba na mbili ni watoto wa mjini. Anyway ni kutafuta uwezekano wa wahusika kuambiwa na kuondoa uhuni huu. Iwe imeandikwa kabisa kuwa kama sehemu haijaindikwa basi Tanzania kama nchi ya kitalii ni RUKSA.
   
 13. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana Mlima Kilimanjaro unaaminika ni wa Kenya yote hii sababu yake ni UBUBU wetu. "NI SIRI" st....id philosophy.
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Bubu Msemaovyo. Sitoshangaa kusikia kuna watalii wanatolewa upepo kwa kuupiga picha mlima Kilimanjaro bila kibali!
   
 15. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Haswaaaa. Nimekuwa nafanya utafiti binafsi wa jinsi tulivyo butu katika kutoa MATANGAZO MAZURI YENYE KUVUTIA, iwe ni kupitia radio, magazeti ama TV. Ukilinganisha na wenzetu Wakenya na Waganda, sisi Watanzania tuko nyuma sana kutoa matangazo achilia mbali matangazo yenye kuvutia lakini pia ile nia ya kutangaza biashara. Hatujui. Mara nyingi matangazo yetu mathalani tunatangaza SABUNI huanza na nyimbo na huishia kibwagizo cha "...SABUNI HII NI KIBOKO CHA UCHAFU. Kama tutatangaza aina fulani ya KINYWAJI basi tutanza na wimbo na kibwagizo chake kitakuwa"....Kinywaji hiki ni KIBOKO cha KIU TANZANIA" HIVI KWANINI MATANGAZO YETU YANAKIBWAGIZO "KIBOKO" Je ina maana hatujui kujitangaza? sasa tunasomea nini katika masuala ya biashara katika kuzitangaza? Hadi nimechoka kusikia Hiki ni Kiboko cha...." TUBADILIKE JAMANI
   
 16. c

  coast Member

  #16
  Apr 3, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao viongozi wetu hata ramani ya nchi yetu hawaijui vizuri, ndio maana hata wanapotaka kuitangaza, wanashindwa wafanye nini.
  HTML:
  hakuna marashi ya kufunika harufu ya ushuzi uliooza
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280

  Lile Tangazo la Utalii la Tz kwenye CNN kwa kweli linasababisha mtu ubadili chanel. Tangazo hili linatakiwa liwe kwa Watanzania watembelee mbuga zao na si watalii. halina tofauti na matangazo ya India, Malesia true Asia, Thailand, nk. Ukija ya Tanzania ongeza neno BUREEE. Kila kitu wao ni BUREE.

  Nafikiri kwenye level ya kimataifa inabidi tangazo lako liwe fupi na kali saana. kikubwa zaidi liwe na kitu kimoja cha ajabu ambacho hakuna watu wameshawahi kukitumia na kila atakayeona basi MILELE ATAKUMBUKA. Mie hapa huwa nina wazo langu zuri tu la kuitangaza Tz na kwa kweli hata BUSH akiliona atacheka saana. Anyway nimeliweka kichwani mwangu na siku moja nikja pata fursa watu walinunue basi ntaliuza na kuomba mwenyewe kucheza kwenye hili Tangazo. Ila nina uhakika kwa asilimia 95% kuwa kila atakayeona basi kuanzia siku hiyo atajua TANZANIA ni nini.

  Nafikiri haya matangazo mengine watu wanapeana tu. Mtu anachukua pesa kwa kazi isiyoeleweka. Ndiyo maana watu wanasema watoto wa mjini. Kama watu wameipa RICHMOND ilete umeme, sembuse matangazo ya biashara? Huko itabidi ipite miaka.
   
 18. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  poleni sana kwa nyusumbufu hizo, wakuu huenda wakawa weshasikia malalamiko haya au kupelekwa kwao tuombe mungu awawezeshe kufanya mabadiliko ya maana kwa maslahi ya taifa
   
 19. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  October mwaka jana nilipita airport Copenhagen, nilikiona kibao kinakataza kupiga picha.
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mbalamwezi, naona hawa jamaa au kuna MJINGA fulani huko aliona aweke au wamekisahau tangu ule wakati wa UKOMINISTI hadi leo. Haingii akilini dunia ya leo kukataza watu wasipige picha wakati unaweza kununua picha yoyote na tena imepigwa unavyotaka kwa kutumia satelite. Anyway nafikiri ulitakiwa kumuuliza POLISI yeyote pale kama kile kibao kweli kina maana yoyote katika karne hii ya 21 au kipo ili KINYANYASE wasiojua kusoma.
   
Loading...