Usipendelee kusikiliza Redio na kuangalia TV: Ushauri kutoka kwa Zee la Mjini!!!

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
801
545
Wakuu habari zenu!

Leo nilipokuwa natoka kanisani nikaanzisha mazungumzo na mzee mmoja hivi ambaye huwa tunasali pamoja lakini huwa sipendelei kuongea naye. Baada ya salamu, nikamwambia naona wazee mnazidi kupungua, mzee mwezio naye katutoka, sijui tutashauriwa na nani kama mkiisha wote! Akasema nani, Mandela? Mwache aende zake akapumzike, vijana wa kisasa si hamtaki ushauri wetu mnasema tumepitwa na wakati? Ndiyo akafunguka sasa, akasema 'Juzi nilikuwa nawashauri vijana wenzio wasipendelee kusikiliza Redio na kuangalia TV kwani havina faida yoyote katika maisha yao, badala yake watumie muda wao mwingi kufikiri na kutafakari mustakabali wa maisha yao' hawakutaka kunielewa kabisa! Walikuwa wanongelea habari za Mandela, nawambia hazitawasaidia kwa lolote, niliwambia wafikiri wataboresha vipi maisha yao na........,! nikawa nimepanda gari na kuondoka, nikamwambia ntakutafuta tuongee kwa kirefu zaidi. Nilibaki na maswali mengi kichwani ingawa jamaa yangu aliondoa gari haraka. Je babu yupo sahihi?
 
Cna uhakika kma ypo sahihi sabbu hajawa specific kuangalia tv/redio kipndi vipi?na pia kila mtu anamtazamo wak juu ya jambo fulni.
 
Dawa ni kuiondosha kwanza CCM madarakani, mambo megine yataji set yenyewe!
Hii s
asa kali kwni hapa tunazungumzia kuangalia TV na kusikiliza REDIO au ni CCM
kuiondosha CCM ni ndoto kwani Vijana wanaozaliwa wenye akili na kujishughulisha ndio watakaobakia CCM
Wale wapenda maisha ya haraka, vurugu, maandamano ndio wasiangalie TV na REDIO kwanindio zinawachochea wakisubiri na TZ ichafuke ili washike Madaraka na wengine wa STOW AWAY
 
Hii s
asa kali kwni hapa tunazungumzia kuangalia TV na kusikiliza REDIO au ni CCM
kuiondosha CCM ni ndoto kwani Vijana wanaozaliwa wenye akili na kujishughulisha ndio watakaobakia CCM
Wale wapenda maisha ya haraka, vurugu, maandamano ndio wasiangalie TV na REDIO kwanindio zinawachochea wakisubiri na TZ ichafuke ili washike Madaraka na wengine wa STOW AWAY

Crapist!
 
Cna uhakika kma ypo sahihi sabbu hajawa specific kuangalia tv/redio kipndi vipi?na pia kila mtu anamtazamo wak juu ya jambo fulni.

Yeye alimaanisha tuangalie taarifa ya habari tu ikiisha endelea na mambo yako mengine yenye manufaa katika maisha yako ya baadae. Alisisitiza ku-refrect mambo uliyofanya kwa siku hiyo, u-assess changamoto zilizojitokeza na kesho utafanya nini ili kukabiliana na changamoto hizo aidha ukiwa pekeyako au na wenzako!
 
Ni sahihi kabisa.

Mkuu hebu dadavua kidogo maana mimi mnavyoona tutakosa mambo mengi sana hasa kushindwa kujua dunia inavyobadirika hata mazingira yako. Ingawa kwa upande mwingine utajiuliza unataka kujua dunia inavyoendelea ili iweje? Wewe utanufaikaje na maisha yako baada ya kujua dunia inaendeleaje?
 
Ulikuwa naye mitaa gani hiyo? angalia huyo mzee asijekuwa anaumwa kidogo.

Huyu mzee alikuwa na akili timamu kabisa na alikuwa anaongea kwa kujiamini na kile anachoongea. Binafsi ushauli wake ulinishtua sababu ninamazoea ya kuangalia TV kwa muda mrefu na usiku huwa silali bila redio pembeni na alfajiri nikishtuka lazima niwashe redio kusikiliza nini kimejiri
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom