Usipendelee kusikiliza Redio na kuangalia TV: Ushauri kutoka kwa Zee la Mjini!!!


Mshua's

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Messages
668
Likes
290
Points
80
Mshua's

Mshua's

JF-Expert Member
Joined May 22, 2013
668 290 80
Wakuu habari zenu!

Leo nilipokuwa natoka kanisani nikaanzisha mazungumzo na mzee mmoja hivi ambaye huwa tunasali pamoja lakini huwa sipendelei kuongea naye. Baada ya salamu, nikamwambia naona wazee mnazidi kupungua, mzee mwezio naye katutoka, sijui tutashauriwa na nani kama mkiisha wote! Akasema nani, Mandela? Mwache aende zake akapumzike, vijana wa kisasa si hamtaki ushauri wetu mnasema tumepitwa na wakati? Ndiyo akafunguka sasa, akasema 'Juzi nilikuwa nawashauri vijana wenzio wasipendelee kusikiliza Redio na kuangalia TV kwani havina faida yoyote katika maisha yao, badala yake watumie muda wao mwingi kufikiri na kutafakari mustakabali wa maisha yao' hawakutaka kunielewa kabisa! Walikuwa wanongelea habari za Mandela, nawambia hazitawasaidia kwa lolote, niliwambia wafikiri wataboresha vipi maisha yao na........,! nikawa nimepanda gari na kuondoka, nikamwambia ntakutafuta tuongee kwa kirefu zaidi. Nilibaki na maswali mengi kichwani ingawa jamaa yangu aliondoa gari haraka. Je babu yupo sahihi?
 

Forum statistics

Threads 1,252,218
Members 482,048
Posts 29,800,741