Usipende kusaidia kila ombaomba, wengine ni chuma ulete

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,905
Habari zenu wakuu,

Husikeni mada tajwa hapo juu.Kutoa au kusaidia ni moyo lakini Wema wako unaweza kukugharimu milele.

Sio kila ombaomba au taahira au wagonjwa wanaombaomba ni wahitaji wa msaada; wengine ni chuma ulete au misukule wanaotumiwa na wanga kukusanya pesa na kuchukua nyota za watu.

Tunapenda Sana kusaidia ila sasa hii ni changamoto mjini.Wema ni mzuri ila Zama hizi ni hatari sana kutenda Wema kwa baadhi ya wanaoonekana kuwa wahitaji kutokana na kutumiwa na washirikina.

Usije sema hujaambiwa.
 
Kama nimechelewa kujua na nishasaidia Sana hawa watu, nifanyeje mkuu?
Sio wote pengine umetembelea nyota njema au bahati

Afu sijasema usisaidie ila na mimi nimekuwa nasaidia kama wewe kabla ya kupata hizi habari kwa yaliyemfika
 
Aise hii kitu ipo sana kaka, kwa upande wangu nikiwiwa kusaidia huwa napeleka kwenye vituo vyao ambavyo wamekusanywa wengi ila siyo wale wanaotega njiani nina imani nao ndogo sanaaaa tangu nielezewe michezo yao.
Best option
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom