Usiongelee bei bali thamani unapomuuzia mteja bidhaa au huduma yako. Akiona thamani atanunua tu

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,655
Greetings.

Kama kawaida leo tunakutana tena katika darasa muhimu kabisa linalohusu mbinu za kuuza bidhaa au huduma yoyote ile kwa potential client.

Nafahamu watu wengi wanaoanzisha business mpya wanahangaika kufahamu jinsi watakavyoweza kuuza bidhaa au huduma zao. Na niseme tu kupata mteja wako wa kwanza inaweza ikawa changamoto kwa sababu, mosi, huna experience, pili hakuna anayekufahamu lakini pia hufahamu namna gani hasa utaweza kumshawishi mteja aone value katika bidhaa au huduma unayotoa ili atoe pesa yake kununua toka kwako.

Hii sehemu watu wengi wanakwama. Na sababu kuu ni kwamba hawajui jinsi ya kuuza. Watu wengi wanaoanzisha business wanadhani wakiwa na product au service, wakaweka watangazo ya kutosha basi watu watanunua tu.

Nop they won’t. Na hapa ndiyo test yako ya kwanza kama entrepreneur. Ngoja nikwambie kitu hapa. Kuuza huduma au bidhaa ni step by step process.

Si jambo la kusema tu nimeunda website, pia nina product au skills za kutoa solution fulani kwa hiyo nitapata clinet. Hapa JF nimekuwa nasema wazi kama kweli unataka kuuza bidhaa au huduma yako inabidi uwe tayari ku-pay price. Na price nayozungumzia hapa ni kujifunza mbinu za kuuza kwa vitendo.

Nafahamu watu wangu ukiwaambia sasa ni wakati wa kwenda mbele ya potential customers na kuuza huduma au bidhaa they are scared to death. Mimi nafahamu kwanini wanaogopa. Wanaogopa “kukataliwa na kubezwa”. Na ninakubaliana nao 100%.

Kwenye swala zima la kuuza utakutana na “rejections” kila siku. Sasa hapa inabidi ujiulize swali gumu. Upo tayari kwa ajili ya hili? Au wewe ni mtu wakuvunjika moyo mara moja?

You have your answers.

Ok. Sasa twende kwenye darasa la leo. Kwanini ni muhimu kuongelea Value na si Price unapojaribu kuuza product au service.

Let’s go through 5 points I’m discussing below.

1 • Mteja anayetaka kununua kweli huduma au bidhaa yako hujali zaidi “value” atakayopata. Suala la gharama (price) ni mtazamo tu.

Ok. Ngoja nifafanue kwa mfano wa kweli.

Binafsi nafanya kazi kama Online Business consulting. Wateja wangu ni watu wote wanaotaka kuanzisha Online Business, wanaotaka kufahamu jinsi yakupata wateja etc.

Sasa hawa potential clients mara nyingi wanakuja kwangu kutafuta value. Wengi huuliza vile nitakavyoweza kuwasaidia kweli katika Business zao. Sasa kadiri ninavyoongelea “value” nitakayowapatia ndivyo inavyokuwa rahisi kukubali price yoyote ile nitakayosema.

Price ni ile utakayosema baada ya kuongelea value. Na kwasababu tayari umeshamwonyesha potential customer jinsi atakavyofaidika basi wengi hawakatai kwasababu wanaona wakikataa wanakosa value kubwa unayoenda kuwapatia.

Does that make sense?

I hope it does.

2 • Mteja anayeenda kununua kweli anapenda asikie jinsi tatizo au hitaji lake litakavyotatuliwa kwakutumia huduma au bidhaa unayomuuzia. Wateja wengi wanaoulizia zaidi kuhusu price kabla hawajafahamu jinsi huduma itakavyowafaa mara nyingi hawanunui.

Hapa inabidi ujifunze kutofautisha aina za wateja.

Na kwa uzoefu wangu mteja anayetaka kununua kweli mara nyingi atapenda zaidi umwelezee jinsi huduma yako au product yako itakavyomfaa. Hapa utapata nafasi yakuonyesha umahiri wa bidhaa yako au service yako na kwakufanya hivi tayari umekamilisha deal hata kama utamtajia kiasi gani cha bei.

3 • Mara zote wateja hununua kwa muuzaji wanayedhani anauelewa mkubwa na huduma au product anayouza. Na kufanikisha hili inabidi uongelee value zaidi kuliko bei.

Ok. Hapa ngoja nikuulize.

Ulijisikiaje ulipohitaji kununua huduma au bidhaa fulani na muuzaji alikuelewesha vizuri sana? Najua ulishawishika kununua. Sivyo? Au kama hukununua basi labda haukuwa na pesa wakati huo tu.

Mimi binafsi napenda kununua huduma au bidhaa nyingine yoyote toka kwa mtu ninayedhani anaufahamu mkubwa kwasababu inafaa kumwamini. Uelewa wake katika huduma au bidhaa anayouza ni kishawishi tosha chakunifanya niamini bidhaa ninayouziwa ni bora.

4 • Bei ni ile unayomuuzia. Thamani ni ile mteja anapata kwa kutumia huduma au bidhaa uliyomuuzia.

Hapo vipi?

Wauzaji wengi wanadhani bei ndiyo kitambulisho cha thamani ya bidhaa au huduma.

No. There so many fake product in the market sell for thousands of dollar but they are useless. Hapa inatakiwa uwe mindful. Ongelea value atakayopata mtaja baada ya kununua bidhaa au huduma na si bei ukidhani ukifanya hivi mtaja ataona thamani.

Ongelea value hadi mteja aone kama hatonunua bidhaa basi anakosa nafasi yakuongeza yakutumia bidhaa au huduma nzuri itakayomsaidia iwe kwenye Business au matumizi binafsi.

Kwa leo niishie hapa.

Tukutane siku nyingine kwa ajili ya darasa kama hili.
 
Kawe Alumni huwezi kumuona hapa!

Nimeshampuuza kuanzia leo.....................
 
Back
Top Bottom