Usiombee kutendwa

Wengi wenu mnapata tabu kwa vile mlikuwa na expectations kuubwa,hii hutokea hasa kwa vijana kwa vile awali hukuwahi kujua saikolojia hasa ya mwanamke
Binafsi nilichojifunza kwa miaka hii nimeishi duniani ni kwamba usiwe na matarajio chanya tuu kwa kitu chochote kwenye maisha wewe jua tu kwamba Jambo lolite unalolifanya kwa malengo chanya Basi jua Kuna hasi yake pia.Hii itakusaidia kujiandaa kisaikolojia kuhimili pindi hasi ikitokea ili usipotee kwenye reli yaani uwe na huzuni inayohimilika na kuganga yajayo,ukizaa watoto kwa mfano jua pia wanaweza wakafariki au wakaugua au ukabahatika wakawa vizuri
Ukioa wewe jua inaweza tokea ukawa cheated nk so jiandae kisaikolojia kwa Jambo lolote hasi kwenye maisha ,kuishi kwenye nadharia ya perfection,rightness na positive response mda wote ni mbaya lazima utatoka kwenye reli,utakata tamaa na inaweza pata stroke kwa heart attack
Ningekuwa na uwezo ningeita vijana wote waje kusoma huu ushauri mzuri
 
Kiufupi nitalia kwa mengine sio mapenzi, niliwah umia na kutetemeka mwili kwa mapenzi back in 2010s huko kuanzia hapo nilijifunza kupenda kwa kutumia akili na sio moyo tena Hadi Leo nimeoa mwendo ni huo huo.
Angalizo na tahadhari,kupenda kwa kutumia akili kutakufanya uone makosa zaidi kwa mwenzio na unaweza kuwa mkatili so jitahidi ku balance na hakikisha mwanamke unaempata ni yule anaeweza vumilia Hali hiyo,usijesema sijakutambua Ila hii njia haitakuja kukumiiza maana umeshajenga saikolojia ya lolote laweza kutokea na uko tayari.Faida ya njia hii ni kufocus kwenye mambo ya msingi ya familia kuliko kuwaza kuridhishana kwa kusimamia kucha kwenye mapenzi
Huu uzi una madini tupu kwa vijana

You are exactly like me
 
Pole mkuu
Japo mie sio kutendwa.wala sikumkosea
Nlipatwa na majanga,ndo ikawa byebye
Nlilazwa muhimbili nahangaika kwenye wheel chair,masindano kama yote.yule nliemuona rafiki wa hata kunitext ujumbe wa faraja kaenda kwa wazima..mi kaniacha!
Tena ananiambia hivihivi kabisa mi na we bhasi.

Mapenzi yametawaliwa na unafki sana.
Hope u're back on your feet now.
 
tafuta PESA haya yote hayana umuhimu wowote ule...kilicho na umuhimu katika maisha yako ni PESA, na FAMILIA yako na sio mtu wa kuja na kuondoka unaumia kwa ajili yake..thats buuullshittt
 
Wanaume tumeumbwa na ujasiri sana, na siyo rahisi kuonyesha udhaifu wake hata pale anapoona ameumizwa sana na mahusiano

Wengi wao huwa tunazuga kama hali hiyo haituumizi kumbe moyoni mwetu kunafukuta maumivu ambayo yanauma na ata umeze Lori la panadol sio rahisi kupata nafuu,binafsi hali hiyo imenikuta na kuna wakati natamani ata nisitoke nje kuona kinacho endelea ila ndio hivyo lazima maisha yaendelee.

Natamani nibadili namba ya simu pengine nahisi naweza kupata utulivu na kumkwepa ila nahisi nitapoteza watu wengi sana ambao tunasaidiana kimaisha,nipo kwenye msongo mzito sana wa mawazo

Hapa JF ndio sehemu pekee naweza kueleza hizi hisia ambazo siwezi Ku share na mtu yeyote physical ila nina uhakika na hili litapita.


Haya mambo ni saikolojiko, ni jinsi ulivyoyachukulia. Hivi ulishawai kufikiri ule uchungu wa kutahiriwa bila ganzi? Kutendwa kitu gani bwana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom