Usiogope wewe ni kama mshumaa

Ras John I

Member
Oct 3, 2017
39
22
Urafiki kati ya Mshumaa na Binadamu kidogo ni urafiki wenye kutia mawazo mengi na viulizo vingi kichwani..? Maana urafiki huu wa binadamu na mshumaa hutokea tu pale ambapo giza huingia, wakati wa mwangaza mshumaa hauhitajiki kwa binadamu, isipokuwa pale panapokuwa na giza.

Ninapowaza aina hii ya urafiki napata kuwaza kuwa ingawa binadamu hauhitaji mshumaa pale panapokuwako na mwanga ila akilini mwake mawazo ya mshumaa yapo na hii inakuwa sababu ya kuutafuta mshumaa pindi tu giza linapotokea. Kwa hiyo uwepo wa mwanga sio kikwazo na wala hauvunji fikra za binadamu kwa mshumaa.

Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na hali kama hii, wapo wale marafiki zetu ambao tunawapenda mno lakini hawajawahi kutukumbuka mpaka pale tu wanapokuwa na shida ndio huuona umuhimu wetu na kututafuta..? Je wakitutafuta tunajisikiaje nafsini na akilini mwetu..?

Wengi tunachukia na hatupendi kabisa kuwa na wale marafiki zetu ambao wao hawatukumbuki isipokuwa pale wanapokuwa na shida tu, Lakini kiukweli ni kwamba marafiki hawa hutusaidia kutujenga kimawazo na kutufundisha kujitegemea wenyewe na kuamini kuwa tunaweza kusimama wenyewe na kufunya vitu vikubwa mno.

KInachomfanya rafiki yako akutafute pale anapokuwa na shida ni Imani yake kubwa kwako,na kuea kwenys akili yake amang'amua kuwa rafiki yangu flani anaweza kunisaidia kutatua tatizo hili linalonikabiri, ndio maana akaamua kukushirikisha wewe jambo hilo.

Hivyo hatupaswi kuchukia pale marafiki wenye shida wanapotutafuta wakati wa shida tu kwani hakuna kitu chenye kuponya zaidi duniani kama TUMAINI, kama hatuwezi kuwapa msaada wenye kushikika, basi tuwape tumaini tu kwani hilo pekee ndilo linaweza kurudisha FURAHA iliyopotea..

Kuwa kama mshumaa haimaanishi kuwa umedharaulika bali ni kiashiria kikubwa kuwa Uhitaji wako ni mkubwa na mara zote wewe ni mtatuzi hodari wa matatizo ya wenzako...

MPE TUMAINI MMOJA NA KILA MMOJA DUNIANI ATAONYESHA TABASAMU..

Rasta John
 
Back
Top Bottom