Usiogope ndoa /dawa imepatikana

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
8,936
2,000
Wanandoa hatarini zaidi kuambukizwa VVU Send to a friend Thursday, 11 November 2010 20:31 0diggsdigg

aids.jpg.gif
Fredy Azzah
MWENYEKITI Mtendaji wa Tume y a Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Fatma Mrisho amewataka wadau wanaoeneza elimu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwu (VVU), kuleekeza nguvu kwa wanandoa kwa kuwa kundi hilo, limeathirika zaidi kuliko vijana.
Mrisho aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua sura mpya ya kondom aina ya salama stud zinazotengezwa na kampuni ya PSI Tanzania.

“Takwimu zinaonyesha kuwa kundi la wanandoa kwa sasa ndilo ambalo lina maambukizi makubwa ya VVU kutokana na kutokuwa waaminifu.
“Mwanzoni tulikuwa tukilitazama zaidi kundi la vijana, lakini kwa sasa inatakiwa serikali na wadau wote wa ukimwi tuelekeze nguvu katika kundi hili la wanandoa,” alisema Mrisho.
Alisema takwimu za tume hiyo, zinaonyesha kuwa maambukizi kwa vijana yamepungua kwa asilimia 25 huku yakiongezeka zaidi kwa wanandoa.

Aliwataka PSI na wadau wengine kuongeza nguvu katika kutoa elimu sahihi juu ya maambukizi ya ukiwmi.
Naye Mkurugenzi wa Mpango wa HIV/AIDS wa PSI John Wanyancha alisema, shirika hilo limefanya utafiti na kubaini kuwa bado kondom hazipatikani kwa wingi maeneo ya vijijini.
Alisema kwa sasa kinga hiyo inapatikana na kutumika kwa wingi zaidi maeneo ya mijini kuliko vijijini.
“Hata mijini kuna watu ambao bado wanadhani mpaka utumie kondom mbili kwa wakati mmoja ndiyo utajikinga na virusi vya ukimwi, hali hii inaonyeha kuwa bado elimu ni tatizo na inahitajika kwa makundi yote,” alisema Wanyancha.

Alisema kuwa, PSI Tanzania imejipanga zaidi kuhakikisha elimu juu ya ugonjwa huu, inaendelea kutolewa wananchi wote wa vijijini na mijini.
 

Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,556
1,170
kweli wanndoa wanatisha,duh ..tulitegemea kusikia vijana wanaongoza kumbe wanandoa kazi bureeeeeeeeeeeeeee:nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono::nono:
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom