Usimuulize gharama ya Ujenzi mtu mwenye nyumba

Binafsi huwa sipendi kumkatisha mtu tamaa anaetaka kujenga.

Nikiulizwa gharama lazima nitashusha TU ili kumtia moyo Aianze safari.

Atakayokutana nayo,
atapambana mwenyewe uko uko mbele ya safari.

Mfano:
Kuna jamaa yang mmoja, ni mtumishi wa seirikali hajawahi kujenga kabisa.

Akasema anataka ajenge nyumba ndogo ya vyumba vitatu TU, jiko, stoo na sebure ikamilike kila kitu ahamie kabisa.

Nkamwambia, milion 10 inatosha kabisa.

Kaenda kachukua mkopo benk wa mil 11 kalianzisha.

Kainua boma,
Ela imeishia Kwenye kupaua TU.

Ananiuliza Mbona Ela imekata mapema,


Nkamjibu TU,
"Pambana mtu wangu, ujenzi huwa hauishi.
Ningekwambia Bei halisi hata ili pagare usingekua nalo.
Huo Ni mwanzo mzuri Sana"
 
Mimi nauliza bei ila siulizi wamiliki wa nyumba bali nauliza mafundi.

Naenda na mchoro/ramani naongea na fundi ananipa makadirio ya matofali kwa hatua husika, mfano kwenye msingi, kupandisha boma na hata kupiga bati.

Ukilinganisha mafundi hata watatu gharama hazitatofautiana kwa zaidi ya 2M.
 
Back
Top Bottom