Usimuamini sana mtu, yamenikuta mwenzenu

thebogo055

Member
Jun 22, 2020
19
176
Habari wana JF,

Leo nina story fupi sana kuhusu urafiki.

1. Ninaweza kuwa rafiki yako lakini usiwe rafiki yangu, nikimaanisha mimi ninaweza kujiweka kwako kama rafiki nika share mambo mengi na ww ya maisha na kukushirikisha maamuzi mengi.

lakini wewe ukaniona mimi kwako ni wa kawaida wa wakupita tu na wewe ukawa na rafiki yako.

2. Rafiki yangu sio lazima awe rafiki yako, na adui yangu sio lazima awe adui yako, hii inaeleweka and it's obvious.

3. Mtu kufanya mawasiliano na ww kila wakati haimaanish kuwa huyo ni rafiki yako, wengine huwa wanahitaji mtu wa kuongea nae tu kwa wakati fulani kutokana na mazingira.

4. Kuna urafiki wa kukutana mahali kwa sababu kuna jambo limewaweka pamoja lakin haimaanish mtakuwa hivyo forever.

Hii ndo mbaya sana kwa watu wanaotafuta marafiki ukubwani na kuona mtu umezoeana naye sana hasa mnapokutana vyuoni, mashuleni, makanisani etc. Urafiki wa watu wa aina hii huwa mara nyingi ni kwa sababu watu hawana other options tu lakini kila mtu ana mtu wake wa kumuita rafiki.

Watu hujisahau sana na aina hii ya urafiki, itasikia kuna rafiki yangu nilisoma naye ngoja nimuombe connection za kazi halafu ukimtafuta anakutupa tupa.

Hii imenikuta mimi binafsi, kuna mtu I considered rafiki yangu kweli, tumefanya vitu vingi pamoja, tumesoma wote pale UDSM.

Baada ya miaka kadhaa tumeishi wote baada ya maisha ya chuo, kutafuta maisha ku-struggle pamoja na vitu kama hivyo.

Ila kama wasemavyo wahenga ridhiki mafungu 7, ghafla mwana akapata fungu lake maisha yakawa matamu, kapata vitu vingi kwa muda mchache. Akapata demu, akaoa, hapo nakumbuka tumepanga nyumba nzima Kinondoni.

Sasa mwana baada ya kuoa akaanza kunitupa tupa na mke wake akawa ananiona kama chawa vile. Mi nikajiongeza nikarudisha mpira kwa kipa.. nikarudi zangu home kwa wazazi kujitafuta kwanza hapo nishafanya ma interview kibao lakini holaaaa. Biashara, kilimo lakini holaa!

Ghafla yule mwanangu akanipgia simu nirudi mjini kuna mchongo natakiwa kuusimamia mimi. Nafika town kanipokea fresh nikafikia kwake, lakini wife wake akawa anaish na mimi kichina china tu, sijui anaona mimi nakula time ya mumewe au niaje, au damu tu hazipatani.

Sasa namwambia mwanangu, bwana vipi ule mchongo,, naambiwa ngoja cjui partner wangu wa biashara cjaongea nae, au wait mwanangu soon mambo yatakuwa poa. Dah muda unaenda hakuna dalili.

Mpaka kuulizia tena nikaona jau, nikawa natoka kwenye misele natafuta michongo ikitokea napga huku nasiklizia mchongo wa mwana.

Baadae nikaja kugundua the guy is playing with me, ana-enjoy kuniona mimi niko chini yake like twende huku, twende kule.

Mwisho wa simu akaanza kumtongoza na demu wangu ana mwambia mm si deserve kuwa nae na maneno kibao.

Mwanamke wangu akaogopa kuniambia akahisi atavunja urafiki wetu, lakini hali ilivyoendelea ikabidi aniambie tu. Dah! Niliumia sana nikasema binadamu tuko tofauti sana, ukizingatia nime sacrifice mambo mengi sana kuhusu yeye hapo mwanzo coz mwana ana kisukari so nimemsaidia mengi kupata matiba, mazoezi, hata huo mchongo aliopata akatusua tumepigania wote, too bad akapata peke yake.

Lakini Mungu hamtupi mja wake saivi naishi kwangu na mwenzangu na biashara zangu zmasimama.

Juzi mwana kanicheki tena anadai kuna mchongo mwezi wa nane kama vipi niibuke twende mkoani tukapige hela, nikamwambia poa haina noma, lakini najua sitathubutu kumu entertain tena.

Maana nilimpa taarifa kwamba naoa! Akarespond ile kinafiki saana like duh unamuoa yule dem wako au huyo ni mpya? Nikamwabia ni yule yule, akaguna, si anajua alishamtongoza na anajua mm cjui kitu.

So guys tuwe makini sana na hawa tunaodhani ni marafiki zetu na kupoteza muda wetu mwingi tukiamini tutapata msaada.

In this life we should trust no body, hata kama trust ipo but iwe 50/50

Inatosha kusema kwamba story imeisha.

Asanteni.
 
Mkuu kwanza pole sna,

Kuna baadhi ya binadamu wanatamani kila siku uwe chini yao

Ndo furaha yao ila Mungu ni wetu sote anagawa ridhiki kwa wakati wake

Usiamini sna watu, penda sna kua jeshi la Mtu mmoja. Mpaka itakapo kulazimu ndo ujaribu kutafuta msaada kwa marafiki.

Kuna marafiki wata kuwekea standards zao
Ukiwa chini wata kudharau
Ukiwa sawa nao, hawana time na wewe
Ukiwazidi watakuchkia
Ishi na watu kwa akili sana.
 
Ndo mana snaga rafiki,tukifanya kazi/biashara/shughuli iliyotukutanisha tukimaliza,ujue imeisha hyo ukiweza futa na namba yangu. hata kama tumekaa wote miaka kadhaa,ile tunapeana kisogo huwa ndo kwa heri vinginevyo tuwe na ktu kinachotuunganisha(common interest) mfano mpira,siasa n.k
 
Mkuu humwamini mtu ndio.lakini umeamua kumwamini demu wako alipokwambia jamaa alitongoza tu na hakufanya chochote.

Anyway,sio kosa kosa ni nyinyi binadamu kidhani kuna watu ni malaika leo,kesho na hata milele.
Wanazingua ndugu wa damu sembuse msela tu mmekutana chuo,kikubwa tusijiachie sana.
Mara nyingi urafiki wa karibu hupoa baada ya mmoja wenu kuoa au kuolewa,ujue hili.
 
Back
Top Bottom