Usimtendee visa asiye kufanyia visa

iranna

Senior Member
Aug 4, 2021
149
617
Hapa mtaani kwetu jirani yetu ni fundi wa magari. Ana garage yake mtaani na watu wanamwamni ni fundi mzuri sana.

Ameoa msichana wa mijini peace kali, wale wa dada wa human hair na lace wigi. Wanaishi kwenye chumba na sebule na mrs hana ajira huwa tunashinda nae mtaani.

Juzi kati walikua na ugomvi, bibi yule alienda kwenye sherehe na alirudi asubuhi. Mume wake hakupenda, aliamua kwenda kazini kuepusha hasira za kumpiga mkewe.. Amefika kazini alikuja kibopa mmoja kutengeneza gari. Ni kati ya watu wachache wanoendesha ndinga za maana mjini. Alikua na tatizo kwenye tairi.

Wakati fundi yuko mzigoni, mke wake alipiga simu. Fundi anapokea simu tu battery ya simu ikakata. Hajui mke wake ana shida gani. Kwa uugwana alimuomba mteja wake simu. Kupiga namba ya mkewe anamkuta mteja ame isave kama ‘sister white’ ni kweli mke wa fundi ni mweumpe wa rangi.

Fundi aliishiwa nguvu, alimuuliza mteja unamfahamu vipi mke wangu. Wanaume kuanza kushikana mashati. Huu ugomvi ni mkubwa na hakuma anaeeleza mkasa ukanyooka. Mke analia mume wangu nisamehe. Fundi anachotaka kufahamu ni ukweli juu ya mahusiano wa kibopa mwenye ndinga kali na mke wake.
.
 
Usimtendee kabisa vitimbwi & visa yeyote; mgomvi mpishie mbali maana atakuharibia ratiba zako za maisha. Heri ya nusu shari kuliko shari kamili, wanasema wahenga. (Afadhali kuridhia -- japo shingo upande -- hasara kidogo, kuliko kuinkaa expenses ambazo zingeweza kuepukwa).

^A prudent person foresees danger and takes precautions, but the thoughtless person goes blindly on and suffers the consequences.^ Proverbs 22:3.
 
Usimtendee kabisa vitimbwi & visa yeyote; mgomvi mpishie mbali maana atakuharibia ratiba zako za maisha. Heri ya nusu shari kuliko shari kamili, wanasema wahenga.
Hembu jiweke kwenye viatu vya fundi magari.
 
Sasa mbona sioni? Kwani ni tatizo mtu kuwa na namba ya Mkeo?

Kwangu mimi sioni tatizo, labda kama endapo niliona Conversation yao.

Tena kamsave kistaarabu sana 'Sister White'. Najaribu ku-imagine endapo angekuta kamsave 'Tope la moto'

Jamaa ndiyo angeua.
 
Sasa mbona sioni? Kwani ni tatizo mtu kuwa na namba ya Mkeo?

Kwangu mimi sioni tatizo, labda kama endapo niliona Conversation yao.

Tena kamsave kistaarabu sana 'Sister White'. Najaribu ku-imagine endapo angekuta kamsave 'Tope la moto'

Jamaa ndiyo angeua.
Fundi anachotaka ni maelezo , jamaa aliipata wapi namba ya mkewe. Lakini si jamaa wala mke wa fundi aliye tayari kufafanua hili.
 
Back
Top Bottom