Usimpeleke mzazi Hospitali ya Kwa Kilonzo, Mwanza ... kisu guaranteed

Fisadi.Jones

Senior Member
Aug 15, 2008
110
7
Jamani hii nimeona nishee na wenzangu hasa wale wakaazi wa Mwanza.

Kuna hii hospitali ya Kwa Kilonzo ambayo inajulikana kama ndio best kwa wanaojifungua.

Lakini ukweli ni kwamba wana tabia mbaya sana ya kulazimishia operation badala ya kujifungua kawaida, hata kama umuhimu wake hakuna. Yaani wanajitahidi juu chini kuhakikisha wanakufanyia opeation.

Wapo kadhaa ninaowajua ambao walilazimishiwa operation wakagoma, wakaenda bugando na wakajifungua kawaida safi.

Sasa hivi imekuwa kama ni open secret kwamba mama akienda Kwa Kilonzo ni kisu tu.

Kwa hiyo chungeni.

Kikubwa kinachowavutia kufanya hivyo ni tofauti ya zaidi ya 500,000 kati ya anayejifungua kwa operesheni na anayejifungua kawaida.
 
hizo ndio negative za biashara huria, hiyo kuna kipindi hata Aga Khan Dar walikuwa nayo sijuhi sikuhizi, pole sana kama yameshakukuta hayo
 
hizo ndio negative za biashara huria, hiyo kuna kipindi hata Aga Khan Dar walikuwa nayo sijuhi sikuhizi, pole sana kama yameshakukuta hayo

Ndio matatizo ya ubepari uchwara, hakuna tena standards wala utu.
 
so bad, hizi biashara ambazo zinahusisha huduma sensitive lazima ziwe zinatupiwa macho, wakati mwingine unaandikiwa tu dawa za ajabu ili store yao ipungue, haya mama zetu wanapigwa visu ili waongeze faida ya biashara. Wenzetu waliondelea wapo makini sana na hizi biashara ambazo sensitive kwa uhai wa raia
 
Aise, pole sana mkuu inauma sana mtu anapokuwa anatanguliza pesa kwenye taaluma yake na kukiuka maadili ya kazi yake, na bado hata ufanisi nao unakuwa chini ya kiwango. Tunahitaji fumua fumua kila kona haswa haya mambo ya afya, elimu, na sehemu zingine kama hizi.

Hizo ni sehemu nyeti za nchi yeyote duniani, mtu anaweza kuja leo na midawa ya malaria akaanza kuwatibu bilakujua analengo gani. Its dangerous, unaweza kwenda hospitali mchwara hizi unaambia magonjwa kibao, harafu hawakupi solution ya uhakika zaidi ya kukupa midawa kibao.


Na hiyo Kilonzo ishakuwa ya bepari anajua anachokifanya. sera zetu zinaishia kwenye makaratasi, watu wanafanya kazi kwa kutanguliza pesa mbele maana hata yeye lazima 10% atoe. Pole mkuu.
 
Private Hospitals zote ziko hivyo, kwa sababu wateja wake ni watu ambao ni wa daraja la kati na la juu. Bila kufanya hivyo wenye hizo hospital watawalipa nini wafanyakazi wao.

Remember kuugua kwako ni biashara kwao-they don't count you kama mgonjwa but a client. ...A CLIENT IS ALWAYS WRONG!!!
 
Lakini pia utashangaa kuwa ma Dr wote hasa wa wanawake wana opt kuzaa kwa kisu!!!!
 
Wakazi wa Jiji la mwanza pigeni kelele juu ya udhalimu huu, kumfanyia mtu upasuaji wa uzazi una madhara makubwa kwa mama na hata kwa mtoto pia, na wala sio njia ya mkato ya mtu kukwepa uchungu wa kuzaa. Lakini hata watoa huduma za afya msifanye biashara kupitia miili ya watu, kwa sababu unamuumiza mtu ili wewe uneemeke!!!!!!!!!! That is very bad.....
 
Tatizo unakuta muhusika wa kuwashikia bango kutoka wizara husika ana hisa katika hiyo hospitali. Unajua Nyerere aliposema viongozi na watumishi wa umma wasiwe na hisa kwenye makampuni binafsi aliyaona haya, kitu ambacho katika corporate governance wanaita "third part disclosure" - unaweka wazi to the public kama una ndugu, jamaa au mwenyewe ndani ya biashara hiyo. Kuna jamaa yangu mkewe walimzalisha kwa kisu tokea hapo hajisikii tena kushiriki tendo la ndoa, yaani ni kama wali-muhasi vile. Ukifika wanachofanya ni kutengeneza mazingira ya hati hati, tukichelewa itakuwa worse na wewe kama umechanganyikiwa kila kitu unasema poa, halafu wanakonyezana $%£%$$%.
 
Kuna hospitali zinajulikana ukizubaa tu daktari anakuandikia kitanda ili chenji iongezeke..siku ya kutoka utashangaa bili kama ya kuishi 5 stars hotel..Nchi ishaharibika hii.
 
Hata St Thomasi, Kwa Dr Mohamed zilizoko Arusha Nao wanatabia hiyo...na wagonjwa wa kaaida ukienda una pewa madawa kibao ambayo haya husiani na ugonjwa unaogua ili wayauze tu hasa wakigudua unalipiwa na shirika mbona utayanywa sana madawa..
 
Kwani taratibu za kitabibu zinakuwaje? Criteria ipi inatumika kuchagua mama kujifungua kwa kutumia kisu au kwa uchungu au nyingie nyinginezo kama zipo? Na nani mwenye uamuzi wa mwisho? Je kuna sera na sheria za kitabibu kuhusu hili jambo kwa tanzania au Dakatari na Mgonjwa ndo wanapewa nguvu ya kufanya maamuzi.?

Sina evidence lakini kwa hospitali kama aghakhan kuwafungulisha wanawake kwa kutumia visu nadhani ni priority sababu ni culture ya wahindi nadhanai hata mataifa ya ulaya kutumia njia hii.

Sasa wataalamu kama wapo watuambie faida na hasara za kutumia kisu.as kwa tetesi nasikia wadada wa siku hawapendi mambo ya kuzaa kwa uchungu.
 
hizo ndio negative za biashara huria, hiyo kuna kipindi hata Aga Khan Dar walikuwa nayo sijuhi sikuhizi, pole sana kama yameshakukuta hayo

mpaka kesho hiyo ami hela azina muda
 
Kuna hospitali zinajulikana ukizubaa tu daktari anakuandikia kitanda ili chenji iongezeke..siku ya kutoka utashangaa bili kama ya kuishi 5 stars hotel..Nchi ishaharibika hii.


heeeeeeeeeee wako wengi oooooooooooooohhhh hapa n kuomba tu mugnu akuepushe na magonjwa nting else
 
kwani taratibu za kitabibu zinakuwaje? criteria ipi inatumika kuchagua mama kujifungua kwa kutumia kisu au kwa uchungu au nyingie nyinginezo kama zipo? Na nani mwenye uamuzi wa mwisho? Je kuna sera na sheria za kitabibu kuhusu hili jambo kwa tanzania au dakatari na mgonjwa ndo wanapewa nguvu ya kufanya maamuzi.?

Sina evidence lakini kwa hospitali kama aghakhan kuwafungulisha wanawake kwa kutumia visu nadhani ni priority sababu ni culture ya wahindi nadhanai hata mataifa ya ulaya kutumia njia hii.

Sasa wataalamu kama wapo watuambie faida na hasara za kutumia kisu.as kwa tetesi nasikia wadada wa siku hawapendi mambo ya kuzaa kwa uchungu.

mkuu.....in short......daktari na mama mjamzito na mume/partner wake wanaweza kuamua kuzaa kwa kisu.......
Daktari anaamua iwapo kuna complications zitakazoweza kuleta madhara iwapo natural/vaginal birth itatumika[sasa hapa ma-dr businessmen ndio wana-take advantage kwani mimi na mke wangu tukiambiwa kuna complication hatuwezi kupinga kwani hatujui chochote].
Familia[mume na mke] wana hiari ya kuchagua kuzaa kisu,unaweza kushangaa but this is not unusual na % ya wanaozaa kwa kisu kwa kupenda inaongezeka kwa kasi,zamani ilikuwa ni celebs kama mrs beckham,siku hizi hata akina sisi.
 
Back
Top Bottom