Nyamwage
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 634
- 1,535
Habari. kumekua na wimbi kubwa la marafiki au watu wakaribu mnaofahamiana nao au hata msio fahamiana wamekua na kawaida ya kupiga vizinga yaani kuomba vipesa vidogovidogo hili swala kwa sasa haliniumizi tena kichwa ni baada ya kuombwa kihela kidogo kama 10k na jamaa mmoja hivi akanunue kileo tunafahamiana mimi nilimchukua nikampeleka kwenye kijumba changu kinachoendelea na ujenzi kutoka hapo saiti na ninako nunua tofali sio mbali na ninapo jenga ni pua na mdomo nilikua nimelipia tofali kadhaa bado tu kuzihamishia kwenye eneo langu ili zijengwe nilimwambia huyo jamaa kuwa siwezi kukupa pesa bure utalemaa bro tupatane uzisogeze hizo tofali hapa saiti kwangu ili nikulipe tukabaliana kiasi cha pesa akazihamisha jioni nikamlipa pesa tuliyo kubaliana tangu nimeanza kuwa na hii desturi nikiombwa pesa na mtu nampa mtu kikazi anakifanya ndio nampa pesa kwa sasa wimbi la kuombwa vipesa tofauti na kukopwa naona linapungua taratibu kadri siku zinavyo zidi kwenda na ninamshukuru Mungu kwa hili.