Usimfanyie ubaya mtu usiyemjua, hujui kesho yako

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
1,186
2,000
Habarini wana JF,

Naamini mmekula Eidd vyema na waliokwenda kwenye kufurahia mbali na makwao naamini wamerudi salama.

Ok let go to the point of no return ni hivi na naamini nawe utaniunga mkono kwa hili kwamba mtu anapokuomba huruma au kukuomba kitu na ukamkatalia jua kuna siku na wewe utaingia kwenye angle yake na hautasameheka wala kuonewa huruma.

Jumamosi iliyopita kulikuwa na wedding ya office mate na kama ilivyo ada ikiwa mwenzetu anachukua jiko basi tunakuwa na kakamati ketu pale ofisini sasa mimi nilisema nitagharamikia mambo yote ya Media kwa maana videography na photography maana nina kampuni yangu binafsi.

Sasa nikiwa nimewapakia crew yangu kuwawaisha kanisani maana maharusi walikuwa wameshafika na tukapigiwa simu ndio wanaingia chuch sasa mimi nikaona isiwe tabu weka gear mwendo wa kuwahi chuch sasa kumbe kwenye kona jamaa wa toch trafic wamebana wakanipiga mkono, basi walikuwa kama 6 hivi ilikuwa ni dad mmoja mrembo sana basi akaniambia mwendo umezidi nilikuwa kwenye 90 sehemu ya 50 .

Basi dada akaniambia hamna maelezo nenda pale kwenye gari kaandike nikamuomba sana dada yani nimeamua kwenda mwendo huu sababu nawahi maharusi na wameshaingia kanisani ,akaniambia kwani mimi ndio nafungisha ndoa wewe nenda kalipe pale, nilimuomba sana, alinijibu vibaya nikasema sawa dada naenda , kufika pale nikalipa nikamwambia naomba leseni yangu nikasepa.

Sasa jana niko zangu ofisini pale kuna ofisini nyingi tu, nikawa naenda lunch kutoka nje nikakutana na yule dada na mkaka mmoja yeye dada kavaa jezi nyeupe na mkaka kavaa kawaida wanashangaa shangaa nikawauliza mnatafuta ofisi gani, wakasema wale mafundi wa simu wako wapi nikamwambia hawajaja leo kwani ulikuwa na shida gani dada labda naweza kukusaidia, akasema kuna hii simu mpya nilitaka kuhamisha vitu kutoka simu ya zamani kuja hii mpya, sasa nikaona hapa ndio penyewe nikamwambia lete nikufanyie chap. Mpaka hapo alikuwa ajanikumbuka ila mimi nimemkumbuka. Basi nikawakaribisha.

Nikamfanyia kazi yake nikamaliza
Akaniuliza eeh bei gani nikamwambia wewe nipe 30000/= inatosha akaanza ooh kaka mbona nyingi hvyo nkamwambia sema mimi nimekufanyia kidogo tena pale wangefanya 50.akalalamika sana hapana bwana nipunguzie .

Nikamwambia haishuki zaidi ya 30000/= nikamwambia ile uliyochukua juma mosi nirudishie akaniuliza Jumamosi vipi mbona sikuelewi, nikamwambia wewe si ulinishupalia nilipe fine pale uliponikamata nkakwambia nawahi kanisani harusini nikakuomba huruma ukanikatalia? Dada akakumbuka aliona aibu sana akaomba msamaha pale unajua sijui nn bana pale nilikuwa na mkubwa nisingeweza kukuruhusu sijui bwana mambo ya kazi nisamehe bure nakamwambia nimekusamehe leta 20. Basi akachukua namba ya simu sa hiv best kinyama aipiti siku bila kunipigia asee.

Nikaamini usimfanyie ubaya mtu usiye mjua ni hayo tu jamani.
 

Godyp

Senior Member
Oct 20, 2011
179
225
Mm huwa naamini katika upendo na utu ukiwa na hivi sheria haina umuhimu
Dada ni kweli alikuwa kwenye sheria lkn utu ni muhimu wakati mwingine
Ningekuwa mm pigo ambalo ningempa
Alivyodai apunguziwe hadi 20000/= ningempa bure na ukweli wake juu
Yeye ndo angejitafakari!!
 

rubii

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
11,465
2,000
Sasa ubaya upi alikufanyia ndugu?
Traffic kafanya kazi yake.
Kila mtu akienda speed kwa kuwahi harusini barabara zitakuaje?
Ni uzembe wako na crew yako kutokwenda na mda maana wapiga picha huwa na maharusi tangu wawapo masaluni,
Ninyi mmezubaa mpaka watu wameshaingia Kanisani??
Hata setting ya vifaa mtafanya saa ngapi?
 

Uvundo80

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
281
250
Mm huwa naamini katika upendo na utu ukiwa na hivi sheria haina umuhimu
Dada ni kweli alikuwa kwenye sheria lkn utu ni muhimu wakati mwingine
Ningekuwa mm pigo ambalo ningempa
Alivyodai apunguziwe hadi 20000/= ningempa bure na ukweli wake juu
Yeye ndo angejitafakari!!
Hawanaga fikra zile wale watu.....ovyo sana...
 

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,244
2,000
Nyie ndo mnasababisha ajali,halafu unataka tuwaangalie tu eti kisa harusi ndo uende mwendo huo halafu usamehewe kulipa faini?? Badilika bhas,hapo hakuna wema wala uzi wako content yake,si sawa na kichwa chake.
 

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,244
2,000
Mm huwa naamini katika upendo na utu ukiwa na hivi sheria haina umuhimu
Dada ni kweli alikuwa kwenye sheria lkn utu ni muhimu wakati mwingine
Ningekuwa mm pigo ambalo ningempa
Alivyodai apunguziwe hadi 20000/= ningempa bure na ukweli wake juu
Yeye ndo angejitafakari!!
Mkuu acha utani,unafikir bila sheria huko barabarani yangetokea mambo mangapi au binadamu hasa watz,tungeish vp?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom