Usimfanyie mtoto haya kama unataka kuwa mzazi bora na sio bora mzazi

Hii tabia ya kupenda "kunyoosha" watu kama vile wamepinda ilipaswa ibaki karne ya 18.Ni ushamba kujivunia umenyooshwa.
Najaribu kufikiria baba yangu angeniacha tu nifanye vitu mpaka "nitakapojisikia" je ningekua wapi leo hii

Kila nikifikiria hilo na njia nilizopitia nikanyooshwa na yule mzee basis na mwanangu atanyooshwa tu mpaka atakapofika kujitambua ndo atachagua mwenyewe na kufanya vitu pale "anapojisikia"

Ila akiwa kwangu bado,mikononi mwangu atanyooshwa mpaka awe kama rula
 
Una uhakika dini yako ni sahihi?
Siku ukiamua dini yako sio sahihi na ulishamzamisha kwenye dini utamsaidiaje?
Hakuna sababu zozote za msingi za kumfunga mtoto hirizi au vitovu,ni uchafu tu.
kulala sawa mim mwneyew nipo against na mtoto kulala na yoyte yule awaye hata kama mdogo.na kuindoa hil we weka vitanda vya 3x6 .
kuhusu masuala ya din tena hapo wrong haupo sawa.mtoto mkunje angali mbichi.
hirizi nin sijui hayo mambo ya mila wachie wenyewe.
 
Usimlaze mtoto na wageni au ndugu wowote wa kiume ambao ni wakubwa kwake.

Usimtoboe masikio akiwa mdogo, muache aje kutoboa kwa hiari yake.

Usimfunge hirizi au kitovu mkononi, shingoni au kiuononi.Hiyo ni mizigo ya uchafu tu kwake, unaweza kuvaa wewe mzazi wake badala yake kama unazihusudu sana.

Usimlazimishe kwenda madrasa, msikitini au kanisani, akifikia umri wa kuchagua mwenyewe ataamua wapi pa kwenda.

Usimvalishe pia hijabu, kwa maeneo yenye joto kama Morogoro ni mateso makubwa sana.

Usimpake wanja mtoto mdogo anapendeza bila hayo makorokoro, kama ni kumkinga na jicho baya huo nao bado ni ushamba.Pia usimsuke nywele za kumtesa au kumnyoa viduku.

Usimuonjeshe pombe.

Akiwa anakataa kwenda shule au afurahii shule yake chunguza sababu ni zipi.

Usipende kuchapa mtoto msumbufu kuna watoto wenye matatizo ya Attention deficit hyperactivity disorder (ADHD), Dyslexia au autism

Usitumie viboko au vipigo kama njia kuu ya kumfundisha adabu au kutatua matatizo ya mtoto.Hii ikiwezekana acha nayo kabisa.
Viboko ni lazima, lazima aende na mm kusali, ushirikina kwa mtoto big NO, kulala na watu NO Unless ni ndugu yake wa Damu, akikataa kwenda shule atakula viboko huku nikiendelea kutafuta sababu ni nn, Urembo kwa mtoto kama wanja, make up kwa mtoto big NO, kumtoboa masikio namtoboa akiwa mdogo, mahirizi kwa mtoto big NO

All in all nataka mwanangu awe na maisha mazuri. Mleta mada nikuulize tu swali, mwanao hataki kwenda shule, kanisani/msikitini humpeleki ukimsubiri ajichagulie mwenyewe, mwanao hataki kufanya kazi za nyumbani na wew unamuacha ili kupisha uchunguzi wa kwa nn hataki.... Wewe kama wewe Unamtakia mema mwanao kwel????
 
Duuuh mkuuu huyoo mtoto hakikuwa atakuwa wa namna gani, , viboko ni lazima hakikosea pia kwenda kanisani ni lazima sio hiyari....mwanangu atafata sheria zangu mpaka atakapo kuwa!
 
Kumuogesha ni muhimu, hii ni kanuni ya afya.

Kumpeleka shule ni muhimu,kila mtoto anahitaji kupata elimu,tena bora. Kama hafurahi kwenda shule,hatua ya kwanza ni kichunguza sababu zipi.

Mtoto kukataa kula ni sababu za kisayansi kwa sababu binadamu kwa asili anapenda kula kupitiliza. Kufikiri kwamba unaweza kumlazimisha kula ni ujuha wa kushindwa kutatua changamoto.
Kama unaona kupelekwa shule Ni muhimu Basi hata kupewa elimu ya dini pia ni muhimu,kanuni ya malezi ya viumbe vyote mtoto anajifunza ustaarabu na kanuni za maisha kwa jamii aliyoikuta,ukichukua yai la Bata likalelewa na kuku Basi kifaranga kitaiga tabia na maisha ya kuku,kwa maana ya kwamba kiumbe chochote Ni matokeo ya jamii iliyimtangulia siyo kuja kujiamulia kuishi atakavyo Kama Bata,na hizo unazoita adhabu Ni katika kuwaweka kuenenda kuishi kma jamii yqke!
 
Mtoa mada ni watu wachache watakuelewa, unachotakiwa ni kutoa maelekezo ya kimalezi kwa mtoto siyo kumlazimishia vitu ambavyo wewe unaamini ni sahihi kwako. Mambo yanayohusu imani, mitazamo au aina ya maisha atakayotaka ataamua yeye akishakuwa mtu mzima..
 
Mleta mada, Mimi nakuunga mkono kwa ila humu utakutana na upinzani mkali sana.
Tatizo kubwa lililo kwenye jamii yetu ni kuwa wazazi wamekariri model ya malezi kwa watoto wao na model hiyo ni ile inayokandamiza uhuru wa mtoto kiasi kwamba akikua na kufikia umri wa ujana/utu uzima anakuwa na hali ya KUTOJIAMINI. Hili ni tatizo kubwa sana tulilo nalo kwenye jamii na maajabu ni kuwa tumekuwa tukiwashangaa vijana wetu kwa tabia yao ya kutokuwa na UTHUTUBU na UBUNIFU wa mambo mbalimbali ktk maisha yao.

Ni ukweli usiopingwa kuwa ili mwanao akue ktk mazingira ya kujiamini, kuthubutu na ubunifu ni lazima umuandae mapema kwa kumpa uhuru KIIMANI na KIJAMII, kinyume cha hapo tunaendelea kutengeneza kizazi cha watu waoga, wasio wabunifu, nk. Halafu mwisho tunaishia kuwalaumu.

Logging off!
 
Hii tabia ya kupenda "kunyoosha" watu kama vile wamepinda ilipaswa ibaki karne ya 18.Ni ushamba kujivunia umenyooshwa.
We kiazi nini??

Haya ni maisha tu kama ilitokea nimenyooshwa nimenyooshwa aidha nijivunie au nisijivunie(whatever "kujivunia means)

Haiondoi ukweli kuwa kuna njia tusingekuwa na mtu wa kuturudisha tungepinda na ninajua hilo na sitakosea hilo kwa mwanangu. We ishi karne ya 21 hata ya 32 ukitaka ila heshimu misimamo ya kila mtu hata kama in tofauti

Kama imekuuma sana chomoa uipake mafuta
 
Mkuu wewe umenielewa 100%.
Kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli kwenye nchi hii miaka 20 ijayo lazima tuubadili huo mfumo wa malezi kama ulivyosema, kuanzia sasa.
Mleta mada, Mimi nakuunga mkono kwa ila humu utakutana na upinzani mkali sana.
Tatizo kubwa lililo kwenye jamii yetu ni kuwa wazazi wamekariri model ya malezi kwa watoto wao na model hiyo ni ile inayokandamiza uhuru wa mtoto kiasi kwamba akikua na kufikia umri wa ujana/utu uzima anakuwa na hali ya KUTOJIAMINI. Hili ni tatizo kubwa sana tulilo nalo kwenye jamii na maajabu ni kuwa tumekuwa tukiwashangaa vijana wetu kwa tabia yao ya kutokuwa na UTHUTUBU na UBUNIFU wa mambo mbalimbali ktk maisha yao.

Ni ukweli usiopingwa kuwa ili mwanao akue ktk mazingira ya kujiamini, kuthubutu na ubunifu ni lazima umuandae mapema kwa kumpa uhuru KIIMANI na KIJAMII, kinyume cha hapo tunaendelea kutengeneza kizazi cha watu waoga, wasio wabunifu, nk. Halafu mwisho tunaishia kuwalaumu.

Logging off!
 
Ungekuwa umenyooka kweli usingekuwa unatukana na kupayuka huku JF badala ya kujenga hoja.

Back
Top Bottom