usimdharau mtu kwa kazi yake hata kama mpakua choo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

usimdharau mtu kwa kazi yake hata kama mpakua choo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Leo asubuhi nimekutana na kituko cha mwaka, naomba nikiri kwamba hata mimi nilikuwa ni mjinga kwani sikutarajia kwamba jambo hilo nililolishuhudia linawezekana. Naomba nikiri kuwa hata mie nilikuwa nawapa watu hawa mtazamo tofauti kabisa nikidhani labda mie ni mjanja kuliko wao, lakini hili nililolishuhudia asubuhi ya leo, nimenifunza jambo moja muhimu sana maishani, kwamba kamwe usimhukumu mtu kutokana na muonekano wake.


  Ilikuwa ni majira ya saa kumi na mbili alfajiri, niko maeneo ya Msasani, nikisubiri daladala la kuelekea Kariakoo, mara likaja basi moja hivi aina ya Toyota Coster. Kama kawaida abiria wakiwemo wanafunzi tulilikimbilia na kuanza kugombea kupanda kila mtu akijaribu kuwahi kiti. Japokuwa hatukuwa wengi, lakini nilishangazwa na jinsi abiria walivyokuwa wakigombea kupanda utadhani watakosa nafasi ya kukaa. Lakini cha kushangaza ni kwamba vurugu zote zile ilikuwa ni ili kuwahi viti vya Dirishani!


  Pale mlangoni alisimama mpiga debe mmoja ambapo kwa hapa Dar hujulikana kama Mateja, yaani watumia madawa ya kulevya, ambaye alikuwa amevaa nguo kuu kuu na zilikuwa chafu ajabu. Alikuwa pale mlangoni kuzuia wanafunzi wasipande. Kwa hapa Dar ni jambo la kawaida wanafunzi kuzuiwa wasipande kwenye basi na abiria wakabaki wakiangalia tu, kama vile haiwahusu. Kule Arusha mambo ni tofauti kidogo, wanafunzi huwa hawaachwi, tena kama hajavuka barabara, hasa watoto wadogo, kondakta anamfuata na kumvusha ili apande kwenye basi, kwa kweli nilishangazwa na ustaarabu wa makondakta wa daladala za Arusha.


  Baada ya abiria wote kupanda, yule mpiga debe aliwaambia wale wanafunzi kuwa atachukua wanafunzi sita tu, wengine waende kwenye mabasi mengine. Pale chini kulikuwa na wanafunzi zaidi ya kumi na tano hivi na wote walionekana wakitaka kupanda kwenye hilo basi ili kuwahi shule. Yule kijana mpiga debe aliongea kwa usataarabu akiwaelewesha wale wanafunzi, akiwaambia kuwa hata yeye anajua adha ya usafiri kwa wanafunzi lakini ile gari ina Hesabu, yaani wanatakiwa wafikishe kiwango fulani cha hela kwa mwenye gari na wao wabaki na chochote, na kwa kuzingatia kuwa leo ni Jumamosi, ni ngumu sana kupata hesabu ya tajiri.


  Lakini kulitokea kutoelewana kati ya wale wanafunzi na yule mpiga debe, wanafunzi walimjia juu wakimwambia aache siasa, wao wanataka kuwahi shule na hawahitaji Lecture pale. Kulitokea kutoelewana, lakini yule mpiga debe alisisitiza msimamo wake wakutaka wapande wanafunzi sita tu. Ni kweli walipopanda wanafunzi sita, aliwazuia wengine wasipande na kuruhusu dereva aondoe gari. Baadhi ya wanafunzi walioachwa pale chini walilazimisha kuning’inia mlangoni, lakini yule mpiga debe aliendelea kuwazuia huku gari likianza kuondoka mdogo mdogo..


  Wakati zogo kati ya wanafunzi na yule mpiga debe likiendelea, ghafla akaibuka abiria mmoja, akaanza kumfokea yule mpiga debe, akimuonya kwamba kama hatawaruhusu wale wanafunzi wapande basi atalipeleka basi lile Polisi, yule Mpiga debe hakumjibu alikuwa akiendelea kuzozana na wanafunzi.


  Yule abiria alianza kumtolea yule mpiga debe maneno ya kashfa huku akimtisha kuwa atampiga. Basi liliondoka na baadhi ya wanafunzi waliachwa pale kituoni, ndipo yule mpiga debe akamgeukia yule abiria na kumuuliza kisa cha kumkashifu wakati yuko kazini.


  Yule abiria akawa kama amechokozwa, alimshambulia yule mpiga debe kwa maneno makali na kumkashifu kuwa hajasoma na ni mvuta unga tu na kibaka wa mtaani.


  Yule mpiga debe akamwambia, ni kweli hajasoma, kwa sababu ingekuwa ni jambo la kustaajabisha kukuta mpiga debe msomi, hata hivyo hakuishia hapo, akamtupia swali yule abiria………


  "inaonekana mwenzangu umesoma sana eh!….. hivi una degree ngapi mpaka sasa, au una masters?” Yule abiria aliendelea kumtolea maneno ya kashfa yule mpiga debe huku akisisitiza kuwa hajasoma na ni mjinga tu.


  Yule Mpiga debe akaonekana kukerwa na yale maneno kutoka kwa abiria mkorofi, akamgeukia na kumwambia, kwa kiingereza, ngoja nimnukuu hapa……..


  “Listen my friend, don’t judge me because of what I am doing, I have good education background than you. To be a Daladala tout does not justify that I am ignorant. For your information, I am educated enough to work for a white-collar job. I am here because of frustration, after being fired from my job; I had a nice job with a lot of benefits and privileges, I am not a fool ok!”


  Wakati anamwaga kiingereza, kwanza abiria walishikwa na butwaa, na baadae wakaanza kumshangilia wakiwemo wale wanafunzi waliokuwa wakitetewa na yule abiria mkorofi. Hata hivyo yule abiria aliposikia jamaa anamwaga kiingeza, alikaa kimya asiamini masikio yake,hakujibu kitu.


  Abiria waliendelea kumchagiza mpiga debe aendelee kutoa dozi kwa mshkaji, na yeye ili kupata ujiko zaidi akaendelea kumwaga ma-vitu, palikuwa ni patamu hapo…….


  “You know sometimes people think all daldala touts are drug users and they are not educated ……..… No, you are totally wrong my friend, for this job I am earning more than enough, I can make your salary which you get from you Boss Indians for 10 days. Although I have been fired but I decided to work as a daladala touts rather than stealing someone’s money.”


  Kisha akaendelea…..


  “Why you are quiet, talk now Mr. Educated” ………… “You see,” akatugeukia sisi abiria na kutuambia ……….. “Mr. Educated have failed to speak even two English words”


  Jamaa akajikakamua na kumjibu,


  “Hebu ondoka na kiingereza chako cha kuombea maji, mwenyewe unajiona umeongea kiingereza hapo, hamna kitu,unachapia tu”


  Mpiga debe hakumkawiza akamjibu…….


  “Ok, my English is just for begging water, where is yours, if you can speak only two English words, I will give you ten thousand, right now, in front of passengers, I am not joking”


  Yule mpiga debe akatoa elfu kumi na kumpa abiria mwingine aishike, ili kuthibitisha kuwa hatanii. Kumbe jamaa alikuwa ni mweupe, hajui Ngeli, yaani ilikuwa ni aibu, karibu abiria wote wakawa wana mzodoa kwa maneno ya kejeli.


  Tulipofika kituo cha Namanga jamaa akashuka kwa aibu na ninadhani alikuwa hajafika safari yake, naona alishuka ili kujisitiri na aibu iliyomkumba mle ndani ya basi.


  Nakwambia ilikuwa ni gumzo ndani ya basi lile kila mtu akisema lake wapo waliosema kuwa yule mpiga debe ni mpelelezi wa Polisi, wapo waliosema ni shushushu yaani anafanya kazi usalama wa Taifa. Na hilo ndilo tatizo tulilonalo Watanzania, yaani mtu akijibainisha tofauti na muonekano wake basi ataitwa shushushu…….. Basi na yule mpiga debe akapewa cheo cha ushushushu pale pale, kisa kaongea Kiingereza, kuna wengine walisema sio Mtanzania bali ni Mkenya, kwa kuwa hakuna Mtanzania anayejua Kiingereza kama vile halafu afanye kazi ya kupiga debe, ili mradi kila mtu alisema lake.


  Tulifika Kariakoo kilamtu akashika hamsini zake, nimerejea nyumbani jioni hii nikaona niwashirikishe wasomaji wangu katika kisa hiki ambacho hata mie kiliniacha mdomo wazi.
   
 2. M

  Mlabondo Senior Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 140
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo Kali
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hahahaha hio kali
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  kweli ni kisa kizuri sana.....ni kimenifurahisha mno......hii tabia ya kudharau watu usiowajua nilishaidelete katika maisha yangu siku nyingi sana.....ni bora kila binadamu amuheshimu mwenzie......big up konda
   
 5. T

  Tabby JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 9,898
  Likes Received: 5,530
  Trophy Points: 280
  Kwa ujumla, haitakiwi kumkashifu mtu kwa failure yoyote katika maisha kama hujui chanzo chake. Wako watu hawakusoma kwa sababu walikataa shule. Lakini wapo watu hawakusoma kwa sababu hawakupata opportunity hiyo maishani. Wapo watu wamesoma na hawana kazi inayolingana na elimu zao kwa sababu mbali mbali, kuna watu wanafanya kazi nzuri zisizolingana na elimu zao. Jamani maisha haya ni fumbo jamani.

  NINADHANI NI VIZURI KUMWONYA MTU KWA KOSA ANALOTUHUMIWA NALO NA SI KUMSIMANGA KWA MAMBO YASIYOHUSIKA NA MADA HUSIKA.
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kisa kizuri ila kilishaletwa kabla.....
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  ufisadi ni tabia iliyopo katika jamii, ila kila ufisadi una level zake na standard ukiwa severe ndio unazungumzwa kidogo kidogo kama hivi
   
 8. m

  mareche JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  usidharau usiyemjua kilimasera
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaa mie nawaheshimu wote ila sasa kuna watu huwa wanataka kumshusha mtu wakati hata hawamjui kiundani nimekutana sana na mambo kama haya!
   
 10. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kisa kimefundisha jambo moja kubwa kuwa usimhukumu mtu kwa muonekano wake
   
 11. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hii hata hapa JF ipo, hawa jamaa wanasiasa wa JF wao ndio wanajifanya wanaelewa umuhimu wa maisha kuliko wengine wote, lakini kuna siku tutamwaga data za Kikwete na Slaa hapa na nakuhakikishieni wataomba razi, watu tumehifazi katiba nzima mpaka full stop na bracket lakini tunawachora tu.
   
 12. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  that is my Klo.....wahifadhi kwa leo...
   
 13. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kisa kizuri sana....usimdharau mtu usimjua
   
 14. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa
  Hii iliwahi kutokea miaka ya 90. Kuna jamaa mmoja namfahamu! Alikuwa msomi wa haja! Alifanya kazi nchini Kenya kama boss wa kitengo na kuoa huko. Majungu yakazidi na kurudi Tanzania. Alitafuta kazi na kwa CV yake hakufanikiwa jamaa zetu wa hapa hawakumpenda sana. Akaishia mtaani. Mbaya zaidi mke naye akawa mkorofi na kuamua kumwacha. Jamaa akakata tamaa kabisa! Nakumbuka alikuwa anakaa pale shekilango makonda wanampa mia mia na saa ingine madereva wanampa daiwaka. Siku moja Prof wa pale UDSM akawa natafuta driver wa kabasi kake kadogo (kipanya) ambacho kilikuwa kimekaa tuu baada ya kuleta kibasi kipya. Jamaa akapata bahati ya kupewa gari. Kwa shida alizokuwa nazo akawa anapiga kazi kwelikweli. Siku moja akarudi akakuta yule dereva wa gari jipya anabishana na bosi wake! Driver anasema mimi siwezi kuongea kiingereza bana kama vipi tafuta mtu mwingine. Jamaa alinambia kuwa aliposikia wanabishana akashawishika kuuliza kulikoni! Ndo bosi akamwambia kuna tenda amepata chuoni na inatakiwa dereva ajuae lugha japo kidogo. Jamaa akamwambia nitajaribu boss! Akaambiwa kesho avae smart aende kujulishwa kwa wageni. Jamaa akaja kesho smart kiaina kapelekwa kwa wageni akatambulishwa. Kilichofuatia ni maajabu! Jamaa alijimwaga bosi akabaki mdomo wazi! Jioni boss akamuuliza umesoma hadi wapi jamaa akamwambia ni graduate! Akamuuliza kwa nini nafanya kazi ya daladala! Akamwambia ugumu wa kupata ajira ndo umemfanya. Unaweza usiamini lakini ndio ukweli wale wazungu toka USA nao walishangaa uwezo wa jamaa! Mwezi mmoja tu ulitosha kubadilisha maisha ya huyu msikaji. Huwezi amini saa hii anakula bata pale Brown University! Ni lecture pale!
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ujumbe mzuri nashukuru.Lakn hii thread ni kama ilishaletwa hapa wiki zilizopita,,au haya mambo ni yanawatokea watu the same kila siku hadi nukta?
  Copyright pleasee!!1
   
 16. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,248
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hii ulishawahi kuiweka hapa! Umeshapageuza hapa jf kama kijiwe chako kutuburuza vile utakavyo? Tumia akili yako!! Acha uzembe!!!
   
Loading...