Usimamizi wa mitihani ya taifa kidato cha nne

naggy

Member
Apr 27, 2011
97
152
<p>Tunaomba kujuwa kubadirika kwa taratibu za usimamizi wa mitihani. Tangu lini maafisa wa elimu shule ya msingi, wakaguzi, na wale wa elimu ya watu wazima wameruhusiwa kusimamia mitihani ya kidato cha nne kana kwamba na wao ni walimu? Kwa nini afisa elimu wa wilaya ya meatu anawateuwa tena bila aibu na kuwaacha walimu wake? Au ndo uswaiba kwa vile wote wako pamoja ofisini kama maafisa, wanakunywa chai pamoja? Huyu afisa elimu kawaonaje walimu wa meatu mpaka kawadharau kiasi hiki? Au kwa vile ni wilaya iliyoko pembezoni kabisa? Kusimamia mitihani ni jukumu la mwalim, hata afisa elimu mwenyewe halimuhusu, haruhusiwi kufungua mtihani wala kuingia chumba cha mtihani wakati mitihani inaendelea. Kazi yake ni kupokea mitihani na kuisafirisha. Huo Ujasiri na zarau kaitoa wapi mpaka anafanya hivyo? Anajiamini nini? Au anaukoo na Ndalichako? Na wewe mkurugenzi hulioni hili? Au ndo mpango wenu wa kujineemesha kwa kuwadhurumu walim, kwamba wao ni waoga hawawezi kuhoji? Na kwamba maadili ya ualimu yamewaingia sana? Hizo tamaazenu zitawatokea puani, ENDELEENI!</p>
 
Kazi ya mitihani ni confidential na hata wasimamizi mpaka sasa hawatakiwi kuwa wamejulikana wewe umejuaje kama Afisa Elimu kawateua jamaa zake? Na uko wapi ushahidi kwamba Afisa Elimu atafanya kazi hiyo? Ninavyojua mimi msimamizi Mkuu wa mitihani katika Mkoa ni REO akisaidiwa na Maafisa Elimu Taaluma (Mkoa) pamoja na Maafisa Elimu Wilaya na kwamba wao hawataingia madarasani (labda kuwe na tatizo) isipokuwa hao Maafisa watakuwa ma Supervisor tu. Usije ukakarupuka kutupa lawama wakati hujui hata taratibu zenyewe zilivyo
 
Pole sana mwalimu wangu kwa kukosa posho ya kushmamia mtihani mwaka huu.!?
 
Jamaa anahasira kweli. Tayari wameshatuma barua za kusimamia?
 
Back
Top Bottom