Usilolijua kuhusu mchakato wa Uchaguzi nchini Tanzania

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Habari za majukumu wanabodi, naamini tumekuwa pamoja katika mada mbalimbali za maswala yahusuyo Chaguzi nchini Tanzania. Nikiwa mmoja wa wafuatiliaji wa Siasa za Tanzania na hasa chaguzi mbalimbali naomba tujikumbushe kuhusu MCHAKATO WA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA.

Kama tujuavyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania ndiyo yenye Mamlaka ya kusimamia na kuendesha chaguzi za Urais, Ubunge na Udiwani kwa Tanzania Bara. Vilevile ina jukumu la Kusimamia Sheria za Uchaguzi, Uandikishaji wa Wapiga Kura pamoja na Uboreshaji wa wa Daftari la Wapiga Kura.

Katika kuendesha chaguzi hizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huteua watu kwa nyadhifa zao na sifa zinazotakiwa ili waweze kusimamia Uchaguzi katika maeneo yao, watu hawa ni pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mtumishi wa Umma ambaye husimamia shughuli zote za Uchaguzi katika ngazi za majimbo. Wengine ni Wasimamizi wasaidizi na wasimamizi wa Vituo vya kupigia Kura ambao husimamia upigaji wa Kura katika Kata zao na katika vituo vya kupigia Kura.

Tuangalie mambo mbalimbali ambayo hufanyika kwenye Mchakato wa Uchaguzi;-

Uandikishaji wa Wapiga Kura - Kama tunavyojua uchaguzi ulio Huru ni lazima utoe fursa kwa kila mwananchi kujiandikisha ili aweze kupiga kura. Kama mnakumbuka Tanzania ilifanya zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hili lilikua ni zoezi muhimu sana katika kufanikisha uchaguzi ulio Huru na wa Haki, ipo mifano mingi ya baadhi ya nchi ambazo hazikufanya vizuri katika chaguzi au zimeshindwa kufanya chaguzi kwa sababu tu wananchi wa nchi hizo hawakuandikishwa.

Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura, Uboreshaji wa Daftari la Wapiga hufanyika ili kuondoa wananchi waliofariki, kufanya marekebisho kwa wananchi waliohama kutoka eneo moja kwenda jingine, Wananchi waliokosa sifa au kupoteza Kadi zao za kupigia Kura waweze kupatiwa kadi nyingine za kuwawezesha kupiga Kura wakati wa Uchaguzi. Hivyo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 kutakuwa na Uboreshaji wa Daftari hilo ili kutoa fursa kwa wananchi wenye sifa ambao hawakujiandikisha au kupiga Kura mwaka 2015 waweze kupiga Kura katika uchaguzi ujao.

Jambo la msingi hapa ni kwamba mara baada ya uboreshaji, Daftari hilo hupelekwa kwenye Majimbo na Kata kwa ajili ya kuwekwa wazi ili wananchi wakague kama taarifa walizotoa ni sahihi na zimeingizwa kama walivyojieleza.

Uteuzi wa Wagombea, Kazi ya uteuzi wa wagombea hufanywa ndani ya Vyama vya Siasa, kwa mujibu wa Sheria vyama vya Siasa vilivyopata Usajili wa kudumu vinaweza kuwasilisha jina la mgombea Urais na Makamu wa Rais kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na jina la mgombea Ubunge na Udiwani kwa Msimamizi na Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi kulingana na siku au muda uliotangazwa na Tume.

Kwa leo naomba tuishie hapa mada hii itaendelea!
 
Muhimu sana sana
Kupiga kura,
Kuhesabu kura ,
Kutangaza mshindi.

Haya maeneo matatu tuna shida kubwa sana.
 
Safi sana na hapa ndani yake kuna elimu ambayo umeitoa kwa wasiojua umuhimu wa kujiandikisha,bila kujua kutofanya hivyo ni kujinyima haki yako ya msingi
 
Ninajinyima haki yangu ya msingi kama uchaguzi huo ni huru na haki.Kwa jinsi mambo yalivyo sasa,ikiwa ni pamoja na mazingira ya kutokuwa na tume huru,kupiga kura ni wastage of time and our countries' resources.
 
Muhimu sana sana
Kupiga kura,
Kuhesabu kura ,
Kutangaza mshindi.

Haya maeneo matatu tuna shida kubwa sana.

Tuelezane ukweli! NEC sio huru! Vivyo hivyo na mahakama, bunge n.k. Hii inafanya demokrasia yetu isiwe demokrasia kamili. Tena, sheria zetu zina mapungufu. Sio haki kusema matangazo ya NEC hayawezi kuswaliwa.
 
Nimejaribu kufikiria kwa muda mrefu nimegundua michakato yote ya uchaguzi ni hadaa kwa wananchi na viongozi wa ccm na upinzani wanajua kinachoendelea na sisi wapumbavu na malofa kwao
 
Naheshimu sana mchango wako! labda utusaidie tu kwa lengo la kuelimishana unaposema michakato yote ni hadaa kwa wananchi unamaanisha nini?
 
Ni kwamba hakuna chama cha upinzani chochote ambacho viongozi wake wa juu wanataka ccm iondoke madarakani kwa maana kwamba wanajua ila wanacheza na akili zetu. Anza kufuatilia toka enzi Mlema, uje kwa Dr Slaa na juzi E. Lowasa tathimini chaguzi hizo kwa umakini utaelewa namaanisha nini.
 
Hata mie nilikuwa na mawazo kama yako,haiwezekani upinzani wakubali kushiriki uchaguzi ilhali wakijua kabisa hata kura wakipata nyingi bado hawashindi
 
Safi sana na hapa ndani yake kuna elimu ambayo umeitoa kwa wasiojua umuhimu wa kujiandikisha,bila kujua kutofanya hivyo ni kujinyima haki yako ya msingi
kujiandikisha sio kila mara kunamaana wakati mwengine tume hii ya uchaguzi ya CCM wanayafuta majini kwenye daftari unakwenda kituoni jina lako halipo
 
Hata mie nilikuwa na mawazo kama yako,haiwezekani upinzani wakubali kushiriki uchaguzi ilhali wakijua kabisa hata kura wakipata nyingi bado hawashindi
Hata kuyakubali matokeo huwa wanakubali kirahisi sana
 
Kumbuka ile tension ya baada ya uchaguzi,watu walikuwa wanawaskiliza ukawa tu wato kauli watu waingie barabarani,lakini wakafyata mkia
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom