Usilinganishe mikutano ya nyomi ya Lowassa na nyomi ya Lissu

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
458
1,000
Wakuu, kuna watu nimeona wakisema kuwa lowassa alijaza watu wengi kuzid Lissu Lakini bado CCM ikashinda, watu Hawa nikama vile wamekosa uchambuzi na uelewa wa kitaalam labda nikuelekezeni

Ni kweli kuwa Lowassa alijaza watu Sana kuliko lisu na kuliko Magufuli na baado CCM ikashindwa, ila Faham kuwa kipindi cha kampeni Ya 2015 na kipindi cha kampeni 2020 kuna utofauti Mkubwa Sana Mwaka 2015 watu walikuwa friendly kiupinzani, watu walikuwa wanachagua Kwa mapenzi wanampenda Nani ndio wanachagua Lakini Faham kuwa kipindi hiki watu wanaenda kuchagua Kwa hasira, hasira za watanzania zitatumika kipindi hiki katika kuchagua tofauti na zamani.

Watu wameteswa, watu wameumizwa, watu wameporwa Mali zao, wakulima wameporwa Mazao yao, wafanyabiashara wamefilisiwa Kwa hila, wafanyakazi wameteswa na kunyimwa haki Zao Kwa ubabe, vijana waliokuwa wanaajiriwa moja Kwa moja walizuiwa kuajiriwa Kwa ubabe, watu wameuwawa, watu wameswekwa magerezani, vikundi vya kigaidi Kama wasiojulikana vilianzishwa kuteka watu, watu wamefungwa Kwa hila, watu wamezuiwa kuwa pesa kila anaepata hela anafuatiliwa, mfano magufuli juzi tu akasema hela zao tutazidhibiti, kuna Siku alisema watu wataishi Kama mashetani, watu wamekufa Kwa mishtuko

Hivyo hao wote hawataenda kupiga kura Kwa Upendo Au Kwa kufuata mkumbo, watapiga kura zao Kwa hasira kubwa, hivyo uliokuwa unawaona Kwa lowasa waligeuka wakapiga kura Kwa magufuli Kwa sababu huko Nyuma wengi Sana walimpenda magufuli kwa sababu hawakujua tabia yake, wengi wao walikuwa na lowassa toka Mwaka 2012 hivyo waliingia kimkumbo Lakini mwishoni karibia na Uchaguzi walimuacha, wasukuma wengi Sana walimchagua magufuli Kwa kigezo cha ukabila pasipo kujua tabia yake kitu ambacho Kwa sasahivi wamegawanyika, wafanyakazi walimchagua mwishoni kutokana na kuwa hawakuwahi kupata madhira Ya haki zao kupokonywa, vijana wengi walimuunga mkono mwishoni Kwa sababu ya ahadi Ya viwanda wakihisi kuwa watapata ajira nyingi na akina mama Vijijini walimpa kura Kwa sababu Ya 50,000,000 kila kijiji, hawa wote walibadilila mwishoni Kabisa muda wa kukaribia kupiga kura na haya pia yalichangiwa na Yule Katibu Mkuu wa chadema, na lipumba kuwageuka wenzao,na akina nchimbi na mama Sofia Simba kubadili maamuzi ya kumuunga lowassa mkono, hivyo kulikuwa na mabadiliko Ya wapiga kura kwenye sanduku yaliyosababishwa Ma mazingira Ya kipindi kile kuwa Hakuna madhara yaliyokuwa yanawatokea wananchi toka Kwa serikali Kama Kwa sasahivi, Kwan sasahivi watu wanahasira Hakuna wa kubadilisha maamuzi,

Pia swala la mikutano Ya kipindi kile ni tofauti na mikutano Ya kipindi hiki, mikutano Ya lisu asilimia tisini wanaoenda watampigia kura, Lakini Kwa magufuli wanaoenda hawawez fika asilimia hamsini watakaompa kura no, Kwan sababu wengi wanaenda Kwa kulazimishwa, kutishwa kufukuzwa Kazi, kutishwa kufukuzwa uwaanachama, na pia kujazwa na watu toka wilaya zooote za Mkoa husika tofauti na lisu ambae anapata watu Wa eneo hilo hilo, pia Faham kuwa magufuli wanaccm karibu asilimia 30 hawatampigia kura wakiwemo makada mbali mbali

Najua wapo watakaopinga Hapa Lakini naomba wakipinga waje na hoja
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,532
2,000
1) 2015 ilikuwa ni UKAWA (Chadema, CUF, NLD & NCCR). 2020 ni Chadema pekee.

2) 2015 watu walikuwa wapo huru kuhudhuria kuliko 2020 ambapo kuna TRA, TAKUKURU, TCRA, kufukuzwa ajira serekalini, nk.

3) 2020 vyuma vimekaza kwa ukata - wananchi wengi wanaotaka kuhudhuria kwa Lissu hawana nauli

4) 2020 tupo wana CCM wengi ambao hatuhudhurii mikutano ya Lissu lakini tutampa kura zetu mgombea huyu
 

Agogwe

JF-Expert Member
Feb 20, 2013
1,758
2,000
2015 ilifikia hatua ukivaa kijani tu unazomewa, CCM ilidhalilishwa sana watu wakahama kwa maelfu kama haikuanguka wakati ule ndio basi tena rip UKAWA.

Awamu hii upinzani wako hoi bin taaban, muungano wa vyama vya upinzani ilikuwa mbinu madhubuti kupata wabunge idadi ya kutosha na hata nafasi ya uraisi.

Leo upinzani wanavuna walichopanda 2015 wanaishi kuishi kwa upepo wa matukio na kuomba kura za huruma.
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
7,919
2,000
Wakuu, kuna watu nimeona wakisema kuwa lowassa alijaza watu wengi kuzid lisu Lakini bado Ccm ikashinda, watu Hawa nikama vile wamekosa uchambuzi na uelewa wa kitaalam labda nikuelekezeni

Hivyo hao wote hawataenda kupiga. Najua wapo watakaopinga Hapa Lakini naomba wakipinga waje na hoja

Mengi uliyoandika ni ya kusadikika. Umeorodhesha na kufafanua matukio ambayo kiuhalisia ni ya kijinai na yanashughulikiwa na vyombo husika.

Iwapo kutakuwa na kura za chuki ni dhidi ya Lissu anayetumia lugha isiyo staha, anayehamasisha vurugu, na asiye na Sera.

Hiyo nyomi yake ni ya vijana wapenda kusikia udaku wa Lissu. Pamoja na nyomi hiyo, haitumii kuwashawishi wamwamini na hatimaye wampe kura.

Kama unaamini hata hao vijana wanakubali udharilishaji wa Rais anaoufanya Lissu, basi uchambuzi wako ni wa KITOTO.
 

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
458
1,000
Sasa Ndugu nyomi Ya vijana na nyomi Ya wanafunzi wa msingi ipi afadhali? Au hujaona mikutano Ya magufuli kuwa kila akiwa Mkoa shule zote hufungwa? Au hujaona?
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,146
2,000
Yani hizi lawama katika huu utawala wa Magufuli zinaonesha kuwa kumbe ccm ilikuwa bado inapendwa na watu huko nyuma kabla ya Magufuli hajawa rais,maana naona lawama zote anaelekezewa Magufuli kuonesha kwamba yeye ndio aliyekuja kuharibu mambo katika hii miaka yake mitano.
 

Joyce joyce

JF-Expert Member
May 23, 2020
458
1,000
Yani hizi lawama katika huu utawala wa Magufuli zinaonesha kuwa kumbe ccm ilikuwa bado inapendwa na watu huko nyuma kabla ya Magufuli hajawa rais,maana naona lawama zote anaelekezewa Magufuli kuonesha kwamba yeye ndio aliyekuja kuharibu mambo katika hii miaka yake mitano.
Hilo liko wazi Ccm ilikuwepo na ilikuwa na utaratibu Mzuri Tu, huyu ndio kaharibu Ccm na ukichunguza watu hawaichukiii cccm wanamchukia magufuli Kama magufuli, nakuhakikishia huyu akiondoka Ccm itabaki kukosolewa tu Kama kawaida ila sio chuki, huyu mtu kaumiza watu bhana, Kakosea Sana, kaleta ubabe, kaleta Chuki na ukabila, kaleta mateso had kwa Ccm wenyewe, Kaja na kakikundi kake kakihutu kanaitwa wasiojulikana unategemea Nani ampende ndio maanaa wabunge wa Ccm watapita ila kura maeneo hayo hawatampa magufuli kamwe anachukiwa yeye Kama yeye
 

1 to 10

Member
Apr 24, 2020
98
125
Ukizungumzia waliofilisiwa ni wachache kuliko walionufaika na uwepo wa magufuli kuna watu wengi kwa sasa wamerudiahiwa viwanja vyao Kwa uwepo wa magu pia kuna watu wameacha kudhurumiwa kuna watu hawatoi rushwa nena wakukima wamefaidka kwa waliokuwa wanauza mazao kupitia vyama vya msingi wanjua walivyokuwa wanapigwa hela zao kwa sasa hayapo tena angali kati ya wafanya biashara na qakulima wepi ni wengi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom