Usikurupuke kuoa Mbeya kama wewe nyoronyoro mtoto wa mama

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,820
MSICHOKIJUA KUHUSU DADA WA KINYAKYUSA (MBEYA)

Msikurupuke tu kuoa Dada zetu kabla hamjahesabu gharama.

Hivi kwanini nyie wajanga hamjiulizi wanapooana mnyakyusa kwa mnyakyusa ndoa inaenda tu, ni kwasababu tunajuana wenyewe,mnaopata shida ni nyie msiowajua.

1. Mdada yeyote Mnyakyusa au aliyezaliwa katika ardhi ya Mbeya, ana utawala. Si kwa mwanaume au mwanamke; hatakuwa tayari kupandiwa kichwani hata angefundwa kiasi gani. Ukitaka ndoa idumu kubali kushuka chini wewe na usijimwambafai wala kutumia mfumo dume kwa Mnyakyusa. Sifa yao kubwa wanajua kupenda, wapo tayari hata kutumia mali zao kuhudumia familia ila tu, usionyeshe kuwabughudhi.

2. Mnyakyusa yoyote ana ukuhani ndani yaani wito, aina ya uteule, hofu ya Mungu. Ukitaka ukosane naye onyesha kumwekea mipaka ya kumtumikia Mungu. Kuna wanaume wameoa wenye huduma ndani afu wanataka wawazuie mara ooh huu mwaliko usiende baki kulea watoto, nakwambia hawatakuelewa, wameshika sana andiko hili:

Mathayo 18:8-9
Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.
Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto. Wanao ufunuo kwamba huo mkono au jicho hilo ni ndoa inayombughudhi na kumletea ghasia.

3. Ukitaka uende sawa na dada wa Kinyakyu, usiwe na wivu naye, ule wivu wa kupindukia. Mpe uhuru fulani, mwamini, utaenda naye mbali, kama ana huduma ya kuimba usitake uongozane naye kwa lengo la kumchunga, wewe kuwa busy na shughuli zako na usizifuatilie hela zake. Wanaume kule nyuma mpo? Volume inatosha?

4. Usimwonyeshe dharau
Moja ya kitu ambacho hatakuvumilia, ni pale utapomwonyesha dharau, yaani utoke na mchepuko akajua afu utegemee atakuheshimu? atakuvumilia? Ni mpaka neema ya Mungu ihusike, japo ukimwomba msamaha ni wepesi kusamehe lakini atakufanyia uchunguzi. Akiona unaendelea atakuacha hata mchana kweupe na maandiko yanayokataza kuachana anayajua.

5. Katika ndoa, usimkate sauti.
Mpe uspika maana utakapomkata sauti atahesabu kama kifungo kwake....na kitu asichokitaka yeye ni kuishi kama mfungwa.

6. Hivi mnajua kwamba Mbeya ipo kwenye mwinuko (mlimani?)
Kila anayetokea Mbeya kwenda mkoa mwingine anatelemka, na kila anayekwenda Mbeya toka mkoa wowote anapandisha. Kiunabii ni kwamba, Mungu ameuinua kuwa baraka, kuwa juu mkoa wa Mbeya na ukioa mtu wa Mbeya familia yako lazima ibarikiwe sana na kustawi lakini vigezo na masharti kuzingatiwa nimeshavisema hapo juu.

7. Usijekutafuta msichana wa kazi toka koo za Kinyakyusa, hutaakaa naye; hawapendi kufokewa, eti umfungie ndani ya geti umwondolee uhuru, thubutu!

Ukimkuta kakaa kwenye sofa utafikiri yeye ndiye mama wa familia, yaani wanapenda kumiliki. Ukimfukuza atashukuru akisema afadhari nikakae bila kazi kuliko kazi na masimango.

8. Kama unataka mwanamke wa kujipigia makofi na matusi na manyanyaso, yaani kama mnajiona mna mikono ya kupiga msioe dada zetu, wao andiko la mtu akikupiga shavu mgeuzie na lingine haliwahusu. Ila ukiwaonyesha jeuri watakuonyesha kiburi tu! Hao ndio Wanyakyusa.

9. Msiwazuie kujishughulisha au kufanya biashara hata mwanaume ungekuwa na pesa kiasi gani hawatategemea pesa kutoka mfukoni mwako, .yaani kinachompa tabu ni ile kusema "naomba hela ya mboga" Hawapendi kujishusha kihivyo.

10. Wanapenda sana kusafiri, hata kama ni biashara basi ni zile za kusafiri. Ndiyo wanaoongoza kuleta ndizi Dar kutoka Tukuyu huku waume zao wakibaki na watoto nyumbani. Hutaki mke asafiri utakula mawe; wanajumua mitumba Mbeya kupeleka magulioni n.k.

SIFA WASIZOKUWA NAZO

° Hawana tabia za umalaya, labda muwafundishe wenyewe
° Hawana tamaa na fedha...ndio maana wanatafuta zao
° Waliosilimu kwenda Uislamu hawakudumu hata miaka miwili maana Waislamu sheria zao ni za mfumo dume
° Huwa hawatelekezi watoto wao, wana mapenzi sana nao.
° Hawana tabia ya kuua waume zao eti sababu ya mali. Nimekwambia wao hawana shida na hela za mwanaume.

UKIONA KUNA MWANAUME ASIYE MNYAKYUSA KAOA DADA WA KINYAKYU NA NDOA INAENDA, UJUE HUYO MWANAUME NI MNYENYEKEVU SANA NA MBINGUNI ATAENDA.

Na ukiona kuna mwanaume mnyakyu kaoa mnyakyu mwenzie analalamika na kulia ndoa ngumu mwanamke anamsumbua, ujue goigoi huyo. Sisi huwa tuko strong sana tukiishi nao tunajua chuma hunoa chuma!

Kama hamuwezi kuishi nao tuachieni sisi wenyewe tunawamudu kona zote. Na niwashauri Dada zetu, mkipata wachumba waonyesheni huu waraka wangu iwapo kama mchumba wako atakubaliana na haya.

Hebu wajitokeze wanawake wa Mbeya wanipinge kama nimewasingizia, au waliooa Dada zetu waseme. Jaribu kuwatag.

Zaidi ya yote

Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. Waebrania 13:4

Wanaume mjue hamuwezi kuheshimiwa kama hamna upendo, na wadada kupendwa kama hamna utii haiwezekani. Kwa hiyo kila mmoja asimame kwa nafasi yake.

By Kuhani Philemon Mlawi
 
Mimi nazani mnapo copy Habari au Ujumbe si vibaya.. Ila muwe mnatoa na respect na kumtambua mhusika. Hii inaonesha kua unalinda utu na kujali vya wenzako.. Ila MTU anatoa mda wake na alicho nacho kwaajili ya jamii alafu Mjinga mmoja anakopi mbio mbio na kukimbilia ku post sehemu bila kuonyesha heshima ya alipolitoa andiko hilo..
Hayo ni matumizi mabaya ya akili na kupenda sifa usizo staili.. Be you bro
Bro, umeusoma uzi hadi mwisho au umekimbilia tu kuhukumu na kulaumu?
 
Mwanamke wa Kinyakyusa hata azaliwe Dar na kwingine atakuwa sawa na aliyezaliwa ardhi ya Mbeya tu as long mzazi wake wa kike yaani mama yake ni mnyakyusa pia

Labda mama yake mzazi asiwe Mnyakyusa kwamba baba mzazi tu ndo awe mnyakyusa mama mzazi awe ea kabila lingine hapo huyo Mwanamke atakuwa na afadhali kubwa.
 
Write your reply...ugonile mtoa mada twambombo na kabila lako unalolisifia naskiaga sana hizo sifa na lisemwalo lipo ila Mimi upande mmoja mzazi ni Mnyakyusa sijakulia Unyakyusani wala sikijui kinyakyusa na sitegemei kuoa Mnyakyusa nitaoa upande wangu wa pwani, maeneo ya chakechake Pemba huko nitapata watoto wazuri na wastaarabu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom