Usikubali ndoto zako zizimike kwa maoni ya mtu mwingine

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
USIKUBALI NDOTO ZAKO ZIZIMIKE KWA MAONI YA MTU MWINGINE

Zama hizi tunazoishi kila mtu ana maoni na kila mtu ana maoni kuhusu jambo lolote.Na kila mtu anaweza kutoa maoni yake juu ya jambo lolote bila ya kujali maoni yake ni mazuri au mabaya.Na kusema ni rahisi sana, hasa kama huhusiki kwenye utendaji.

Ni kitu kizuri kwa watu kuwa na maoni, ila pia kunakuja na gharama kubwa.Watu wengi wameshindwa kufanya mambo makubwa kwenye maisha yao kutokana na maoni ya wengine.

Labda ulipanga kufungua biashara fulani, ukawauliza watu wako wa karibu, na wakakupa maoni yao. Ukaacha hukufungua.Tatizo kubwa ni kwamba maoni sio ukweli, maoni sio uhalisia, maoni ni hisia za mtu tu anavyoamua kusema kuhusiana na kitu fulani na mara nyingi yanaendeshwa na hofu zake.

Watu sio kwamba wanafanya utafiti wa kina halafu ndio wanatoa maoni, wao wanaangalia hisia zao kisha wanatoa maoni yao, na kulingana na hisia walizonazo, maoni yanaweza kuwa mazuri au mabaya.Sasa haijalishi maoni wengine wametoa ni mazuri au mabaya, yasikuzuie wewe kuiendea ndoto zako.

Leo nakutangazia kwamba maoni yoyote ambayo mtu yeyote atayatoa kwenye ndoto yako kubwa kwenye maisha ni kelele, usisikilize hata kidogo. Tumia muda huo kupambana kufikia ndoto yako kubwa na sio kuanza kufikiria watu wanasemaje kuhusiana na ndoto hiyo.

Usikubali ndoto yako izimwe na maoni ya mtu anayeendeshwa na hisia za hofu au upendo. Weka juhudi kwenye ndoto yako, na utapata unachotafuta.
 
Ina maana mpaka leo unafika hapo ulipo, haujui kama akili za kuambiwa changanya na zako...
 
Back
Top Bottom