Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,561
USIKUBALI KUSAINI NYARAKA HII UNAPOPEKULIWA NA POLISI

Na Bashir Yakub. WAKILI
+255 714 047 241

Polisi wanapokufanyia upekuzi, iwe wewe mwenyewe binafsi, nyumbani kwako, kazini kwako, gari lako au penginepo ipo fomu maalum ambayo wao wenyewe huijaza na kumtaka mtu aliyefanyiwa upekuzi naye kuijaza.

Fomu hii huitwa Certificate of Seizure. Fomu hii hujazwa hasa pale ambapo katika upekuzi kuna chochote kinatakiwa kuchukuliwa kama ushahidi(exhibit).

Ni fomu ambayo huoredhesha mali ama vitu ambavyo umekutwa navyo. Chochote ambacho umekutwa nacho ambacho wao wanatakiwa kukichukua/kuondoka nacho kama ushahidi basi huorodheshwa.

Hata kama kidogo kama pipi ama sindano madhali wanatakiwa kukichukua kwa ajili ya upelelezi basi hutakiwa kuorodheshwa kwenye hiyo fomu/hati.

Aidha, ni muhimu kujua kuwa ikiwa unapinga kuhusu kile kinachochukuliwa kuwa hukukutwa nacho ama hakikukutwa kwako basi usikubali kusaini fomu hiyo.

Hii ni kwasababu kukubali kwako kusaini fomu hiyo tafsiri yake kisherria ni kuwa umekubali kuwa umekutwa na hicho kitu.

Na endapo utafikishwa mahakamani basi fomu hiyo itawasilishwa kama ushahidi na kwasababu ulisaini basi ulikubali kuwa ulikutwa na kitu hicho.

Vinginevyo uwe unakubali kuwa ni kweli hicho kitu umekutwa nacho, basi hapo waweza kusaini. Lakini kama hukubali basi usisaini.

Msimamo huu ni wa Mahakama ya rufaa kupitia kesi ya SONG LEI VS THE DPP, AND THE DPP VS XIAO SHAODAN and Two Others, Consolidated Criminal Appeal Nos. I6'A' of 2016 & 16 of 2017, ambapo mahakama ilisema kuwa kusaini hati/fomu ya upekuzi ya mali zilizochukuliwa ni kukubali kuwa umekutwa na huo ushahidi.

Katika hii kesi raia wa China walisaini Pembe za Wanyama kukutwa ndani ya gari lao na ndo ukawa ushahidi dhidi yao.

Maamuzi mengine mengi yameeleza msimamo huu kuwa ukikubali kusaini umekubali kukutwa na huo ushahidi.

Ni muhimu sana kulijua eneo hili la mtego ambalo linaweza likakupeleka jela na yafaa basi kuwa makini katika mazingira hayo.
 
Wakili hajatoa elimu amefanya uchochezi ambao watu wasipoelewa vizuri watajikuta matatizoni.

Alitakiwa kusema iwapo hukukutwa nacho kataa lakini kama umekutwa nacho saini.

Huwezi kukutwa na bangi (nazungumzia kukutwa nayo sio zile za kuwekewa) halafu ukaamua tu kukataa.

Kwahiyo watu waelewe ni kile usichokutwa nacho tu.
 
Wakili hajatoa elimu amefanya uchochezi ambao watu wasipoelewa vizuri watajikuta matatizoni.

Alitakiwa kusema iwapo hukukutwa nacho kataa lakini kama umekutwa nacho saini.
Uko sahihi kabisaa kama amekuja kujitangaza hapa na uwakili wake ni dhahiri ajitafajari upya unapotoa ushauri ni lazima ujiridhishe ukamilifu wako katika swala unalolitolea ushauri sasa unakuja hapa na mihemko yako na kujaza watu ujinga.
 
Wakili hajatoa elimu amefanya uchochezi ambao watu wasipoelewa vizuri watajikuta matatizoni

Alitakiwa kusema iwapo hukukutwa nacho kataa lakini kama umekutwa nacho saini

Huwezi kukutwa na bangi (nazungumzia kukutwa nayo sio zile za kuwekewa) halafu ukaamua tu kukataa

Kwahiyo watu waelewe ni kile usichokutwa nacho tu
Hakuna Wakili hapo, Mbabaishaji uyo
 
Ndugu hawa Jamaa nadhani huwa wanavuta mibangi,wanaweza wakakugonga virungu Hadi unakojoa,,acha kabisa.

Una sign signature ambayo si yako ukifika mahakamani unawakata kiulaini,hakuna haja ya kubishana nao hawa jamaa ni wajinga kweli kweli wakiwa katika anga zao wanaweza kukuumiza vibaya kisa ubishi wa kijinga ambao mwisho wa siku ukitumia akili unawaacha kwenye mataa.
 
Back
Top Bottom