Usikubali kufanya mambo haya katika maisha yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usikubali kufanya mambo haya katika maisha yako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 3, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Unapotafuta mwenzi wa maisha si suala la kubahatisha kama vile kuwa kwenye chumba chenye giza totoro na kuanza kutafuta sindano sakafuni bali ni suala la kuhakikisha kuna mwanga wa kutosha kupata kabla ya kuingia kutafuta.

  Ukweli ni kwamba dalili za ndoa kushindwa huweza kujulikana mapema hata kabla ya ndoa kufungwa hasa kutokana na jinsi mwenzi alivyopatikana

  Usikubali kuoana haraka mno.
  Kuwa wachumba kwa muda mrefu huwezesha ndoa yenye afya.
  Hapa unatafuta mtu wa kuishi nawe maisha yako yote ina maana utalala naye chumba kimoja maisha, utakula naye chakula maisha yote, utakuwa naye katika matatizo ya kifedha maisha yako yote, utauguzana naye miaka yako yote, mtakumbana na kukatishwa tamaa pamoja maisha yako yote.
  Kuamua haraka haraka kuoana ni kujitengenezea risk kubwa.

  Usikubali kuoana wakati bado umri mdogo sana:
  Oa au olewa wakati kwanza wewe mwenyewe unajijua vizuri.
  Pia hakikisha unamfahamu vizuri yule unaoana naye.
  Kuanzia miaka 24 kwenda mbele ni umri mzuri kuoa au kuolewa.
  Kuwa na umri mdogo maana yake bado hujatimiza mambo ya msingi kama pamoja na kukomaa kiakili kuishi kama mke na mume.
  Tafiti zinaonesha ndoa stable ni zile ambazo wanandoa walioana wakiwa na miaka kuanzia 28.

  Usikubali kitu chochote, mazingira yoyote au mtu yeyote kukusukuma kuoa au kuolewa.
  Hakikisha umetuliza akili zako ndipo ingie katika biashara za kuoana.
  Inawezekana unataka kuoana haraka kwa sababu uliachwa na mchumba mwingine, au unajisikia mpweke, au anahisi ukiolewa suala la uchumi litakuwa limepata jibu.

  Usikubali kumridhisha mtu yeyote na chaguo lako:
  Ni wewe utakaye pata faida au hasara, raha au machungu, furaha au huzuni, utamu au kuumizwa na si muda mfupi bali hadi kifo kitakapowatenganisha.
  Haina haja kuwafurahisha wazazi au marafiki, au mchungaji, au mchumba mwenyewe kwamba unaoa au unaolewa eti wawe very happy.
  Hii haina maana kwamba hutakiwa kuwasikiliza katika ushauri wao kuhusu wewe kuoa/kuolewa bali hii ni ndoa ni yako a lifetime opportunity.
  Wala usikubali mtu awaye yote akuchagulie au kukufanyia uamuzi hata kama anauzoefu namna gani.
  Wewe ndiye unatakiwa kuwa na uamuzi wa busara hata baada ya kupokea ushauri wa kila aina kutoka kwa watu tofauti

  Usikubali kuoana na mtu hadi uweze kumfahamu katika njia tofauti.
  Unatakiwa kumfahamu vizuri huyo mwenzi wako mtarajiwa, mfahamu tabia zake kwa kadri unavyoweza.
  Kutembea mmeshikana mikono miaka 10 ijayo kunategemea sana jinsi unavyomfahamu vizuri kabla ya kuingia naye kwenye ndoa.

  Usiolewe au kuoa huku una matarajio makubwa sana (unrealistic):
  Ndoa kimbilio la faraja; inahitahiji kazi ya maana ili ikupe faraja.
  Usiingie kwenye ndoa umeweka matarajio ya juu sana as if ni solution kwa shida zako zote kifedha, kihisia na kimaisha.
  Hata kama sasa kuna mapenzi ya juu sana na una matumaini makubwa uwe makini kwani kila kitu kinaweza kuyeyuka kama barafu kwenye jua.
  Kama unataka kuwa an ndoa imara jiandae kwa kazi iliyombele, kujitoa kutakuwa na maumivu, kuvumiliana, utakutana na changamoto ambazo inabidi ushindi na kuthibitishwa ili kuwa na true love kwa mwenzi wako.

  Usikubali kuoana na mtu ambaye tabia yake unahisi hutaweza kuivumilia maisha yako yote.
  Kama kuna tabia Fulani ambayo hupendezwi nayo kama wivu, uchoyo, uchafu, hasira, uvivu, kutowajibika, siyo mkweli au msumbufu; jiulize kama utaweza kutumia maisha yako yote na yeye huku ukipambana na hiyo tabia.
  Hiyo tabia mbaya kwake haitaondoka, kama unaomba muujiza abadili tabia hakikisha unatokea kabla hujaoana naye lakini si kuoana naye huku unajua kuna tatizo kubwa eti ukioana naye muujiza utatokea.
  Siku njema.....................................
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Kumpata mwenza au mke au mume ambaye utaishi naye maisha yako yaliyobaki hapa duniani ni jambo la msingi sana katika maisha ya binadamu.
  Na kwa kupenda wenyewe hupelekana hadi kwa viongozi wa dini na kutangaza hadharani kwamba mimi na mwenzangu tunataka kuwa mke na mume na ulimwengu ujue.
  Huwa tunakuwa tumejawa na mioyo yenye furaha na kutaka siku ifike upesi ili nianza kuishi na mwenzangu haraka iwezekanavyo.

  Mungu bariki mioyo ya maharusi wapya maana hawajui kazi halisi wwanayoenda kuianza kazi halisi (real life) na kuachana na maisha ya uchumba ambayo mengi ni tambarare kama nyikani.
  Baada ya honeymoon tu wengine siku ya pili tu, wengine mwezi wa kwanza tu na wengine mwaka wa kwanza tu wa ndoa huanza kujiuliza hili swali;
  Lakini hakuna aliyeniambia itakuwa kama hivi?

  Alikuwa anaacha mialiko ya watu kwa ajili yako lakini baada ya kukuoa si hivyo tena, unadhani kwa kuwa alikuwa ana cancel mialiko ya kwenda kufanya mambo yake kwa ajili yako kabla hamjaona na mkioana itakuwa the same?
  You are wrong!

  Ili usipoteze matarajio ya mahusiano yako ya ndoa jaribu kuzingatia mambo yafuatayo (kama unategemea kuoa au kuolewa please print na kafiche haya unaenda kuyasoma na baada ya kuanza ndoa soma tena na pia ukiyaweka moyoni na ukizingatia utakuwa candidate mzuri sana)

  Hakuna binadamu anaweza kutimiza mahitaji yako yote:
  Mtu ambaye anaweza kutimiza mahitaji yako yote ni BWANA, na ilimpasa kufa ili aweze kukutimizia yote.
  Usitegemee ndoa au uliyeoana naye atakutimizia mahitaji yako yote au ahadi zake zote alizoahidi kabla hamjaoana.

  Kiwango cha mapenzi hakiwezi kuwa juu kama ilivyo mwanzo wa ndoa.
  Jinsi anavyokwambia ‘I love you” huweza kupungua hadi ukashangaa kadri ziku zinaenda ingawa neno “I love u” huleta raha sana kwa mwanamke akisikia kutoka kwa mumewe hata hivyo siku zinavyoenda mwanaume hujisahau na kuanza kula jiwe kusema " I love u"
  je, utadai?
  Pia wanawake nao (wachache sana) akishazaa huanza kujisahau na kujiona mama na si mrembo bado. Huku ni kukosa ustaarabu na kinyume cha maadali.
  shame on you!

  Mwanaume anaweza kuwa anakupenda mno lakini bado hatajua unahitaji kitu gani.
  Wanawake wengi huja na sentensi ‘ Kama ananipenda angefanya kile napenda afanye” kumbuka usiposema na kumwambia ujue hawezi kujua unataka kitu gani au nini kinakusumbua.
  If you don’t ask the answer is NO.
  Men read newspapers not minds!

  Si mara zote uliyeoana naye atapenda kuimarisha mahusiano.
  Katika mazingira ya kawaida wanawake hupenda hata kuimarisha kitu kizuri (mfano ndoa ambayo hata haina mgogoro) hata hivyo wanaume wana msemo wao
  “If it is not broken, don’t fix it”
  Hivyo tumia hekima na kuomba Mungu ili Mungu awape moyo wa umoja na juhudi ya kuishi kwa amani.

  Ndoa haiwezi kukufanya uwe umekamilika.
  Si mara zote ukiongeza nusu na nusu unapata kitu kizima.
  Wengi ambao ni ‘Single’ hudhani wakioa au kuolewa watakamilika na kujiona complete na kuwa na furaha ya kweli.
  Na wengine hufika mbali zaidi kwa kujinyima vacation, kununua vitu vizuri wakisubiri kufanya hivyo wakioa au kuolewa.
  Unapoteza muda wako anza kukamilika kwanza kabla ya kuolewa au kuoa na ingia ukiwa si tegemezi kwamba mwenzako atakukamilisha hadi kukupa furaha.
  Ndoa ni kuunganisha strength na ku-balance weakness siyo kukaa tu kutegemea mwenzako akukamilishie furaha yako.

  Usitegemee kufanya kila kitu pamoja
  Kufanya kazi pamoja, kupanga mipango pamoja, kuweka malengo pamoja ni suala zuri sana hata hivyo kila mmoja huhitaji breathing room.
  Usitegemee kila kile unapenda basi na mwenzio atakuwa excited nacho si kweli hivyo kuna wakati utahitaji kuwa mwenye na yeye kuwa mwenyewe.
  Nakwambia mapema ili siku ikifika usiseme hakuna aliyeniambia, mimi nimekwambia!

  Mtu ambaye anaweza kumbadilisha ni yeye mwenyewe si wewe.
  Kama unategemea ukioa au kuolewa utambadilisha (change) mpenzi wako basi utakuwa very much disappointed.
  Kama kuna vitu vinasumbua kwa mpenzi wako kabla humjaona viangalia vizuri, kutegemea kwamba utamsaidia kubadilika baada ya honeymoon ni kujidanganya kulikokithiri.
  Ndoa si mahali pa kulaumiana, kukefyakefya (nagging), hasira na kukosoana.
  Kama mpenzi wako hajui UCHAFU ni kitu gani hakikisha anafahamu kabla hamjaoana, na kama unategemea utambadilisha aache ulevi, kuvuta sigara, kuwa mwongo nk shauri yako!

  Maswali ya kujadili
  Wewe ambaye upo kwenye ndoa sasa je, unaona maratajio yako yote ya ndoa yalitimia?
  Je, una matarajio yoyote ambayo unahisi yalikusumbua zaidi?
  Je, una ushauri gani kwa wanandoa wapya?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Kutoa zawadi ni tendo la upendo.
  Lakini wakati mwingine kupeana zawadi huleta kasheshe na kufikia mahali watu kuumizana.
  Unapotoa zawadi kwa mpenzi wako ni vizuri kuzingatia yafuatayo:
  Toa kile ambacho mpenzi wako anakipenda siyo kile wewe unakipenda vinginevyo kutoa kunaweza kuwa ni kitendo cha uchoyo uliopindukia kama utatoa kila wewe unapenda.
  Wengine huwapa wapenzi wao zawadi ambazo wao wanazipenda wakidhani kwamba kwa kuwa wao wanazipenda na wapenzi wao watazipenda, ni vizuri kuchunguza mpenzi wako anapenda kitu gani. Hata kama zawadi ni zawadi.

  Zawadi si biashara.
  Kutoa si deal kwamba ukitoa basi na yeye lazima atoe. Na kuna wengine akikupa zawadi na wewe usipompa ni kununiana tu.
  Unatoa hata kama hutapokea in return ( hata hivyo watoaji hupokea)

  Toa zawadi nzuri.
  Inawezekana mpenzi wako amekuwa anahitaji Digital Camera na inaonekana kama vile ni usumbufu maana kila wakati anakukumbushia.
  Huhitaji kununua bora Digital Camera isipokuwa nunua Digital Camera bora zaidi ya ile alikuwa anahitaji na tofauti na vile alikuwa anategemea.

  Toa kwa furaha;
  Kutoa kwa furaha (smile) huongeza value ya zawadi. Usitoe kwa kushurutishwa kwa sababu bila kutoa zawadi mpenzi wako anakuwa mkali, toa kutoka moyoni na kwa furaha.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Miaka 60 iliyopita ilikuwa ni illegal kwa mweusi na mweupe kuoana katika states 40 za USA.
  Watu walioamua kuoana huku wakiwa na race tofauti walitumikia kifungo cha miaka 2 au 1 na aliyehusika kufungisha hiyo ndoa aliweza kupata fine inayomtosha.

  Kwa mfano katika jimbo la Virginia, Supreme Court iliwahukumu wahusika kwenda jela mwaka mmoja na wakishamaliza kifungo kuondoka Virginia bila kurudi kwa miaka 25 na Jaji aliwahukumu kwa kipengele kinachosema
  "Mungu aliumba races tofauti kama vile white, black, yellow, malay na red na akawaweka kila race kwenye continent yake na kwa hiyo Mungu alifanya hivyo kwa makusudi ili watu wasichanganyane au kuona".

  Hata hivyo Supreme Court of USA ilikatisha hiyo hukumu na kuwaruhusu watu kuoana race tofauti tarehe 12/06/1967 kwa maana kwamba kukataza mixed marriages si suala la kikatiba kuanzia hapo sasa kuna biracial marriage za kumwaga duniani kote ingawa bado baadhi ya jamii zina mashaka na hili.
  Tunaitumia marekani kama mfano kwa sababu ndiyo nchi yenye mchanganyiko wa rangi zote za ngozi kuliko nchi yoyote na kwamba wamepita katika machungu mengi kuhusiana na races.

  Biblia haina tatizo na watu wa races tofauti kuona ingawa wapo wakristo vipofu ambao wanadhani kuona rangi tofauti za ngozi ni kinyume cha Biblia.

  Hata hivyo binadamu wote wametokana na mtu mmoja Adamu hivyo tangu Mwanzo hadi Ufunuo hakuna mstari unaokataza kuoana races tofauti.

  Musa mwenyewe alioa mwanamke wa kiafrika kutoka Ethiopia (Hesabu 12:1) hata Mfalme Sulemani ambaye alivunja rekodi ya kuoa wanawake wengin duniani bado Mungu hakasirikia kwa kuoa wanawake wageni (race tofauti) bali alimkataza kuoa wanawake wanaoamini Mungu tofauti na Jehova.
  Hata hivyo unapoamua kuoana na mtu ambaye ni rangi ya tofauti ni muhimu kukumbuka sana kwamba suala la kubaguana lipo na utakumbana nalo ila kama mkishikana vizuri mume na mke na watoto athari huwa kidogo.
  Watoto huweza kutaniwa sana na baadhi ya jamii ingawa kwa sasa kuna kukubalika kwa kiwango cha juu sana duniani.

  Sasa mambo yamebadilika mweupe anamtaka mweusi (chocolate colour) na kizazi cha sasa kinaona rangi si kitu.

  Hata hivyo kabla ya kuoana lazima ufikirie vizuri suala la tamaduni maana tamaduni zingine job description kwa mwanaume ni tofauti, angalia usije ukajuta ni muhimu kuangalia mbali zaidi miaka 30 au 50 ijayo kuliko kuangalia sasa.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Kawaida ikiona kuna alama ya NO EXIT kuingia humo lazima ufikiria mara mbiliKitendo cha kutoa ahadi kwamba Hadi kifo kitakapotutengenisha ukweli binadamu unakuwa ume –launch moja ya ahadi za pekee duniani.
  No turning back, no escape route kulia au kushoto, wawili mnaingia kwenye life boat, hakuna kwa kwenda zaidi ya kubaki na huyo umemkubali.

  Ukweli ni kwamba mtu mwenye akili timamu akiambiwa nyumba unayoingia haina EXIT atafikiria kwa makini zaidi na zaidi ya mara mbili.

  Kazi yako ipo well defined hakuna kutoka, hapa nazungumzia mtu ambaye kweli yupo serious kwanza kuhakikisha ndoa yake inampa Mungu utukufu na kwamba Kristo ni Bwana katika maisha yake.
  Na kwamba suala la dini na imani ni muhimu sana kwake otherwise hakuna shida.
  Mambo ambayo wakati mwingine huleta shida sana kwenye ndoa ni dini, rangi (race) na taifa hata hivyo linaloweza kuwa mwiba mkali ni suala la dini.

  General rule ni kwamba
  “The more couples have in common the better the chance of success”

  Ukweli unabaki palepale kwamba waumini wa kweli wa dini tofauti (let say muislam wa swala tano na mkristo aliyeokoka) wakioana kuna uwezekano mkubwa kukumbwa na matatizo yanayohusiana na dini katika ndoa yao.
  (Najua ukianza kuzungumzia dini unaweza kuwasha moto ambao kuzima ni ngumu hata hivyo lazima kuongea ukweli)

  Watu ambao hupuuza hiki kipengele baada ya kuoana wanayo ya kusimulia kwa masikitiko.
  Jambo la msingi kabla ya kuoa au kuolewa ni vizuri kupata solution ya suala la dini au suala la imani, usijidangany kwamba mkioana utanyoosha kwa pasi ya umeme kirahisi suala la hili la dini, hapa unahitaji kuwa genius tumia akili zako zote kuhakikisha umejua nini hatima yake.

  Unaweza kuvuka mito mingi tu lakini mto wa dini ni lazima uvuke ukiwa makini kabisa maana unaweza kuzama mbele ya safari.

  Je, mtasali wapi na kivipi, na watoto wakizaliwa watakuwa dini gani na dini ya mwenzako ina amini vipi kuhusu ndoa?
  Ni maswali ya msingi sana.

  Wengi huona hii ni issue ndogo sana na tutakabiliana nayo tukiona sasa muhimu ni love maana nampenda kuliko suala la dini.
  Ukweli vitu vidogo ndo hupelekea ndoa kwenda shimoni.
  Na kuacha kujadili sasa haiwezi kumaliza tatizo baadae, kumbuka
  “the sooner the better”
  au niseme
  “the more you solve now the greater your compatibility later.

  Imani ya dini ni moja ya njia mke na mume huwa connected, dini ni big deal na zaidi ili ndoa iwe strong haina budi kuwa na 3 layers yaani connection ya kimwili, kihisia (emotions) na kiroho na bond ambayo hushika ndoa (siyo sex) mara nyingi ni kiroho.

  "Marriage is not a trial like foreign dish sampled to see if it is tasty
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Kisaikolojia wanaume wengi (si wote) ni genital aroused (wakiwa kwenye sita kwa sita huwaza sana south pole na kupeleka mkono sharp kama kupokea pesa bank), hata akiwa na Mwanamke anaweza kusisimua matiti na uke tu then akaendelea kuchimbua dhahabu yake na kwa namna na style zote anajua.
  Wanawake wao ni “Generally aroused” kwa maana kwamba kwao foreplay ni mwili mzima na mwili mzima kwake ni “one big sex organ” hivyo wana uwanja mkubwa sana wa mwanaume kuchezea kabla ya kwenda bondeni kuchimbua gold habari njema ni kwamba wanawake wanajua kwamba wanahitaji mwanaume mwenye mikono slow kuchezea uwanja mzima kabla ya south pole.

  Kwa Mwanamke erogenous zones si matiti na between the legs bali ni entire body, huwa Inaumiza sana wakati mwingine Mwanamke anakuta mwanaume hata kukisi tu anasahau na moja kwa moja anakimbilia kwenye clit.. kwa kuwa ni joy button, ni vizuri lakini unahitaji kuuandaa mwili mzima kwanza hadi mind yake ifunguke na kuwa ready kwa shughuli ndipo ukimbilie kwenye kisimi then nice sex moments.

  Wengi katika kujifunza masuala ya mapenzi (hasa wanaume) na hasa suala la kufanya maandalizi (foreplay) anajua kitu cha msingi ni kwenda moja kwa moja kubusu, kuchezea matiti kidogo (geresha tu) then anakimbilia bondeni na kuanza kupima kuona kama kuna unyevu wa kutosha ili mtambo uanze kuchimbua dhahabu huku anasahau kwamba lazima mwili mzima wa mwanamke lazima uhusike kupata matokeo mazuri ya dhahabu unataka kuchimbua, sex ni mwili, mood, ubongo na lazima vyote vijui kwamba kuna mitambo ya kuchimba dhahabu imefika.

  Mwanaume kukimbilia bondeni haraka hupelekea sex kuwa na utaratibu unao bore ambao mwisho husababisha Mwanamke kuepukwa sex kwani anajiona unamtumia kutimiza raha zako bila kumpa yeye raha.
  Kumpa mguso (emotional touch) kwa kumhudumia mwili mzima ambao kwa mwanamke ni kiungo kimoja cha mapenzi.

  Fikiria mwanaume umechelewa kurudi na unakuta mkeo kalala fofofo, kwa kuwa unahamu na kuwa mwili mmoja bila kusema chochote wala kujua mwenzio ameshindaje wewe moja kwa moja na mkono wako sharp unakimbilia kuanza kusugua clit.. yake, huo si ustaarabu kabisa, ni kukosa maadili ya ndoa (immoral) na unahitaji kufahamu kwamba kila kitu kina utaratibu wake huwezi kuweka unga kwenye maji kabla hayajachemka ukitegemea ugali utaiva na kuwa mtamu shauri yako utaishia kujaza unga hadi kiwe kitu kingine na si ugali tena.

  Pia kuna wanawake ambao maumbo yao huwa na kasoro kama unene sana, au kifua Kuwa flat kama mwanaume au matiti kuwa makubwa mno (Nido au mtindi, watermelon), huwa hawajisikii vizuri au kutojiamini (bad self image) na huwa na mtazamo negative so akiona wewe ume concentrate hapo anaanza kujisikia vibaya na husababisha kutojiamini (insecurity) then kutosisimka.
  Ni vizuri kujifunza strength na weakness za maeneo ya mke au mume wake ili kutosababisha kuharibu mambo pia ni muhimu mtu kujiamini kwamba wewe ni mzuri na kama ulivyo unaweza kuwa mtaalamu na kurishika na kurishisha mwenzako.
  Ni wewe so unaogopa nini na mume au mke ni wako.
  Wapo wanandoa ambao ni waoga na hawajiamini kiasi cha kushindwa kabisa kuwa uchi mbele ya mwenzake. Ni aibu na kupitwa na wakati.

  Pia utafiti unaonesha kwamba wanaume wengi waliooa ni wagumu sana lipokuja suala la kubusiana na wake zao wakati wa maandalizi ya tendo la ndoa, wengi walikuwa wazuri sana kubusu wakati ndoa zilikuwa mpya na miaka inavyoenda basi wanazidi kupunguza skills na muda wa kubusu ingawa wanaonekana kwa sex ndo wenyewe skills zimeongezeka.
  Upendo daima!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Sex ni zawadi murua kutoka kwa Mungu yenye makusudi ya ajabu.
  Sex hutufanya kuzaliana, kujenga upendo (mutual love au one flesh) pia ili tujisikia raha (pleasure).
  Sex ni God given drive kama vile tunavyojisikia njaa, ili tule Mungu aliweka ndani yetu kujisikia njaa. Na ili tuzaliane, kujenga upendo na ku-enjoy kati ya mume na mke katika ndoa Mungu aliumba sex, Mungu ndiye ame-innovate sex si binadamu.
  Sex ni kitu ambacho kina nguvu sana na uwezo wa ajabu (powerful) kinachoweza kuharibu na pia kupotoshwa na binadamu.

  Sex ni kama moto, uweza kukufanya ujisikie joto kama kuna baridi ila huo moto ukishindwa kuithibiti unaweza kuchoma nyumba yako au misitu na kuweza kukuua.
  Watu wengi sasa wamekufa kwa sababu ya sex kama vile magonjwa ya zinaa kama UKIMWi, Kisonono, Kaswende nk.

  Wengine wameachwa na wake zao au waume zao na kuzifikisha familia nje ya ndoto zao na maumivu makali wka watoto.
  Wengine wamekatwa mapanga na wengine kupata ngeu za kila aina kwenye miili yao.
  Wengine hawana amani maana siri walizoziweka ndani ya mioyo yao kuhusiana na sex zinawatafuna kila siku.
  Ni kama vile aibu kuona watu wanapata maafa na wengine kufa kutokana na bado decisions kuhusian na sex.

  Kama hujaolewa au kuoa kumbuka kusubiri (abstinence) ni uamuzi wa busara kuliko kujiingiza kwenye mapenzi kabla ya ndoa.
  Kama umeoa au kuolewa kumbuka mapenzi nje ya ndoa ni janga kubwa kuliko unavyofikiria.
  Kwa Mungu hakuna lisilowezekana:

  (Luka 1:37)
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Jun 3, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante kwa angalizo mkuu ila ungeweka source ya hiyo habari rafiki!.
   
 10. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hii ina biase sana katika hili kuna feminine biase. Hii ni ushauri kwa wanaume tu wakifanya kwa wanawake. Sijaona point ya nini kinatakiwa wanawake kuwaridhisha wanaume kwenye ndoa. Ni zawadi tuu na inayoweza kataliwa. Mungu tu ndio anayeweza kukupa unachohitaji tena ikiwa utafaulu kutambua unahitaji nini na uombeje? Na si wakati wote hukupa kila unachohitaji. Huu ni ubinafsi na ni tabia zinazopitishwa kwa vinasaba. What I know is everywoman can be taken by everyman BUT not every woman can be married by everyman and most are not married; for their behaviour, thinking etc
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  “Our deepest fear is not that we are inadequate. Our deepest fear is that we are powerful beyond measure.

  It is our light, not our darkness that most frightens us. We ask ourselves, Who am I to be brilliant, gorgeous, talented, fabulous? Actually, who are you not to be?

  You are a child of God. Your playing small does not serve the world. There is nothing enlightened about shrinking so that other people won't feel insecure around you.

  We are all meant to shine, as children do. We were born to make manifest the glory of God that is within us. It's not just in some of us; it's in everyone. And as we let our own light shine, we unconsciously give other people permission to do the same.

  As we are liberated from our own fear, our presence automatically liberates others.”

   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Wakati mwingine ukikosa kuguswa unapata "skin hunger" MGUSO (physical touch)
  Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa.
  Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
  Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.

  Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni.
  Jambo la msingi fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia anapendwa na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa au mahusiano yako kuwa matamu au machungu.

  Unaweza kutumia muda mwingi kumpikia chakula kitamu, au kununulia mizawadi ya gharama, hata hivyo kama mwenzi wako kupendwa ni kupokea mguso wa kimwili bado zawadi zako hazitamkuna vizuri kama ungempa mguso wa kimwili.
  Ktk milango ya mitano fahamu, kugusa ndiyo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaa zaidi na zinahusisha watu walio katika ndoa tu.
  Kuona tunatumia macho, kunusa tunatumia pua, kusikia tunatumia masikio, kuonja tunatumia ulimi lakini kugusa ni mwili mzima.

  Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation North pole hata hivyo hapa tunazungumzia sex ndani ya ndoa na si vinginevyo.
  Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
  Unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?
  Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha,

  KUSAIDIANA KAZI
  Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

  Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.
  Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

  Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.

  MANENO YA SIFA
  (Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
  Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyofaanya kitu ambacho kilionekana kizuri?
  Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
  Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mwenzi wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA.
  Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wakoHuleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfarijiMwenzi hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.

  Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu.
  Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
  bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
  yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.

  Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
  Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri?
  Huwa unajisikiaje?
  Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.

  Nami mwenzi wangu yupo kwenye hili kundi, kwake kumpenda ni pamoja na kumpa appreciation ya yale anafanya hadi jinsi anavyovaa, mwanzo wa ndoa ilikuwa ngumu kujua ila nilishangaa ananiambia mbona wenzako wananiambia nimependeza na wewe husemi chochote?
  Kwa kutojua nilikuwa namjibu “ndiyo maana nilikuoa ni kweli unampendeza na hilo najua.

  Hata hivyo sasa nimejifunza kusema asante na kumshukuru na kumpa sifa kwa kila anachovaa hata akivaa akapendeza nakuwa mtu wa kwanza kumwambia bibie leo umependeza na unawake.
   
 13. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Wakati mwenzi (Spouse) wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi (emotionally na romantically) hujisikia salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na matokeo yake hujitoa zaidi kuhakikisha anajiweka katika kiwango cha juu kwako kuimarisha upendo na mahusiano kwa ujumla.
  Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia mweupe, empty na kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha na kutimiza hitaji lako la mapenzi.
  Moja ya tatizo kubwa katika kuonesha upendo (love) tumeshindwa kufahamu kwamba mke na mume huongea lugha tofauti za upendo.
  Kila mmoja huwa na namna tofauti jinsi anavyojisikia unampenda kwa mfano mwingine ukimpa zawadi yoyote hujisikia unampenda na ukimsifia anaona ni maneno matupu na mwingine ukimsifia basi hujiona raha na hujisikia unamthamini na kumpenda.
  Kuonesha upendo kuna lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano na utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kwa kuisikia na kwa kuiongea, pia utamu wa upendo katika ndoa au mahusiano ni pale unapofahamu lugha ya upendo kati yako na mpenzi wako.

  Itakuwa vigumu sana kwa anayejua kibena kuanza kuongea na anayejua kimasai na wote wakawa wanadhani inawezekana.
  Kumbuka Babeli haikujengwa ikaisha kwani baaada ya lugha kuharibiwa kila kitu kilisambaratika.
  Kimsingi ili kuelewana na mpenzi wako kuna lugha za msingi tano ambazo kati ya hizo moja wapo inaweza kuwa ni maalumu kwa ajili ya mpenzi wako na kuifahamu au kuzifahamu lugha zake basi unaweza kujenga mahusiano imara.

  Hata hivyo mahusiano bora huanza kwanza na Hofu ya Mungu (Christ in you)
  Lugha tano muhimu ambazo mara nyingi wapendanao hutumia ni:
  1. Kuwa na muda na mwenzi wako (Quality time)
  2. Kupeana zawadi (Receiving gifts)
  3. Kusaidia kazi (Acts of services)
  4. Kumpa maneno ya kumsifia, kumtia moyo kwa kile anafanya (words of Affirmation)
  5. Mguso wa kimwili (physical touch)

  KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO
  (Quality time)
  Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili.
  Kukaa na kuangalia TV pamoja si kuwa na muda na mwenzi wako kwani hapo mnaipa TV qulity time.
  Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu. Ni kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini.

  Kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi.

  Kama mpenzi wako yupo kwenye hili kundi yaani kwake kupendwa ni kuwa pamoja basi ni dhahiri ukifanya haya mara kwa mara anatajisikia raha sana na atajisikia unampenda sana.

  Hata hivyo kama mpenzi wako kwake lugha ya upendo ni zawadi ataanza kulalamika why unakuwa na mimi tu muda wote hata zawadi huniletei?
  Maana kwake kupokea zawadi ndo kuonesha unampenda na si kufuatana kila mahali.

  KUPEANA ZAWADI
  (Receiving gifts)
  Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
  Zawadi huelezea upendo kwamba alikuwa ananiwaza na kuniona mtu wa maana sana kwake.

  Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi, pia wapo wengine hudhani zawadi kwa mpenzi hadi kiwe kitu kikubwa kama gari au nyumba, vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
  Nahisi hata wewe msomaji ulikuwa maarufu sana kutoa zawadi wakati wa uchumba na sasa umeacha, Bisha!

  Zawadi muhimu pia ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako au mpenzi wako anakuhitaji anapokuwa na shida (wapo wakiona shida hukimbia wapenzi), uzoefu inaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia huongeza level ya mapenzi kwako.

  Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapenda.
  Kama mpenzi wako kupewa zawadi ndo lugha yake ya upendo basi ikitokea wewe unampa sifa kwa mambo mazuri anafanya usishangae akikwambia punguza maneno zawadi zipo wapi? Atakwambia anataka matendo si maneno!
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  Rangi si Kitu sasa!

  Miaka 60 iliyopita ilikuwa ni illegal kwa mweusi na mweupe kuoana katika states 40 za USA.
  Watu walioamua kuoana huku wakiwa na race tofauti walitumikia kifungo cha miaka 2 au 1 na aliyehusika kufungisha hiyo ndoa aliweza kupata fine inayomtosha.

  Kwa mfano katika jimbo la Virginia, Supreme Court iliwahukumu wahusika kwenda jela mwaka mmoja na wakishamaliza kifungo kuondoka Virginia bila kurudi kwa miaka 25 na Jaji aliwahukumu kwa kipengele kinachosema
  “Mungu aliumba races tofauti kama vile white, black, yellow, malay na red na akawaweka kila race kwenye continent yake na kwa hiyo Mungu alifanya hivyo kwa makusudi ili watu wasichanganyane au kuona”.

  Hata hivyo Supreme Court of USA ilikatisha hiyo hukumu na kuwaruhusu watu kuoana race tofauti tarehe 12/06/1967 kwa maana kwamba kukataza mixed marriages si suala la kikatiba kuanzia hapo sasa kuna biracial marriage za kumwaga duniani kote ingawa bado baadhi ya jamii zina mashaka na hili.
  Tunaitumia marekani kama mfano kwa sababu ndiyo nchi yenye mchanganyiko wa rangi zote za ngozi kuliko nchi yoyote na kwamba wamepita katika machungu mengi kuhusiana na races.

  Biblia haina tatizo na watu wa races tofauti kuona ingawa wapo wakristo vipofu ambao wanadhani kuona rangi tofauti za ngozi ni kinyume cha Biblia.

  Hata hivyo binadamu wote wametokana na mtu mmoja Adamu hivyo tangu Mwanzo hadi Ufunuo hakuna mstari unaokataza kuoana races tofauti.

  Musa mwenyewe alioa mwanamke wa kiafrika kutoka Ethiopia (Hesabu 12:1) hata Mfalme Sulemani ambaye alivunja rekodi ya kuoa wanawake wengin duniani bado Mungu hakasirikia kwa kuoa wanawake wageni (race tofauti) bali alimkataza kuoa wanawake wanaoamini Mungu tofauti na Jehova.
  Hata hivyo unapoamua kuoana na mtu ambaye ni rangi ya tofauti ni muhimu kukumbuka sana kwamba suala la kubaguana lipo na utakumbana nalo ila kama mkishikana vizuri mume na mke na watoto athari huwa kidogo.
  Watoto huweza kutaniwa sana na baadhi ya jamii ingawa kwa sasa kuna kukubalika kwa kiwango cha juu sana duniani.

  Sasa mambo yamebadilika mweupe anamtaka mweusi (chocolate colour) na kizazi cha sasa kinaona rangi si kitu.

  Hata hivyo kabla ya kuoana lazima ufikirie vizuri suala la tamaduni maana tamaduni zingine job description kwa mwanaume ni tofauti, angalia usije ukajuta ni muhimu kuangalia mbali zaidi miaka 30 au 50 ijayo kuliko kuangalia sasa
   
 15. mwilongo Aron

  mwilongo Aron Senior Member

  #15
  Dec 29, 2016
  Joined: Oct 15, 2014
  Messages: 105
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hii mada wanandoa wangekuwa wanasoma hakika wangeishi kwa raha sana.
  Pdidy umedadavua mambo kwa undani sana.
  Wenye macho na waone.
  Hongera sana
   
 16. mwekundu

  mwekundu JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2016
  Joined: Mar 4, 2013
  Messages: 20,002
  Likes Received: 7,974
  Trophy Points: 280
  Ndefu sana.. anzisha seminar kabisa
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Dec 29, 2016
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  P Didi kabla ya kutwangwa rungu kichwani:D.
   
 18. Mkushi wa kusi

  Mkushi wa kusi JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2016
  Joined: Jun 23, 2015
  Messages: 3,112
  Likes Received: 4,202
  Trophy Points: 280
  upo smart upstairs
   
 19. Mwamba028

  Mwamba028 JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2016
  Joined: Nov 15, 2013
  Messages: 2,970
  Likes Received: 902
  Trophy Points: 280
  aisee huu uzi wa kitambo ila mzee p diddy alitema madini ya hataree
   
 20. Kirikou Wa Kwanza

  Kirikou Wa Kwanza JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2016
  Joined: May 24, 2013
  Messages: 3,057
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi ni bahati kukutana na uzi kama huu.
   
Loading...