Usiku wa mashetani

Jacaranda

Member
Oct 23, 2011
45
20
USIKU WA MASHETANI

Mtu ambaye atakufa ndani ya dakika kumi aliishikiria briefcase yake vizuri huku akitembea kutoka nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere.Kwa mwendo wa taratibu akatoka nje ya Mlango wa kiwanja kuelekea sehem zinapopaki teksi,Akasimama kuyapisha magari kabla hajavuka barabara na baada ya kuridhishwa kuwa hakuna gari nyingine inayopita akaanza kuvuka.

Alirushwa juu na kisha kutua kwa kishindo kwenye barabara,Maumivu yalitambaa kwa kasi mwilini mwake na kisha yakapotea ghafla,akahisi mwili wake unaelea angani ,huku nguvu zikimtoka taratibu .Akaikumbatia briefcase yake na kuisogeza karibu kabisa na mwili wake.Misuli ya macho yake ikaanza kulegea na kumfanya aanze kuona maluelue.Sura ya mtu aliyesimama mbele yake huku akiivuta briefcase yake ilipenya mpaka kwenye ubongo wake, ambao kwa muda huo ulikuwa umejaa damu aliitambua sura hiyo lakini hakuweza kugundua alimuona wapi na lini.Akajaribu kuzuia briefacase yake isipokonywe lakini nguvu za mikono yake zikamsaliti akaiachia kwa urahisi kisha jamaa akaendelea kwa kupekua mifukoni na kuochomoa vitu vyote akavidumbukiza kwenye kibegi kidogo alichokivaa mabegani

Kama mfinyanzi atazamaye kazi yake Muuaji akasimama na kumtazama mtu aliyelala kwenye dimbwi la damu moyoni akajisemea “haitachukua sekunde thelasini atakuwa amekufa” Maneno yake yalikuwa sahihi kama ya nabii Eliya kwani azikufika sekunde ishirin kwa mtu aliyegongwa na gari kumrudia Muumba wake.

Muuaji alikuwa ni mtalaamu katika kazi yake na kwa kipindi hicho wenda ndiye alikuwa muuaji wa kukodiwa maili zaidi huu duniani. Baada ya masaa arobaini na nane atakuwa tayari amekabidhi mzigo kwa mtu aliyemkodi na kisha kuelekea Rio De Janeiro ambapo atatembelea fukwe za huko na kubadirisha wanawake wa kibrazili kila usiku, hili nalo lilikuwa ni jambo jingine alilofuzu zaidi.Jambo ambalo hakujua ni kuwa kwa kitendo alichokifanya kitasababisha mgogoro mkubwa sana duniani,utakaowatia wendawazimu viongozi wa dunia na kuwatia hofu wakazi billion saba wa dunia,Hata angejua hilo asingejali
’ @@@@@@@@@@@@@@@@@
Doctor Anthony Mjuni alijeegemeza kwenye meza iliyokuwemo kwenye chumba cha kuchunguzia maiti katika hospitri ya taifa ya Muhimbili akisubiri msaidizi wake auandae mwili wa maiti vizuri.”Doctor tayari unaweza kuendelea” Sauti ya msaidizi wake aitwaye Omari ilimshtua toka kwenye kiusingizi kilichoanza kumchukua, akakurupuku huku akifikicha macho yake.usingizi na pombe alizokunywa jana vilikuwa vinazunguka kwenye ubongo wake na kuufanya upoteze umakini.

Usiku wa jana kwake ulikuwa mbaya kwani aliuanza kwa kunywa pombe na msichana ambaye alijitambulisha kwake kwa jina la Candice.Sura nzuri na umbo la Candice vilimvutia na hivyo alitarajia mapenzi motomoto. Baada ya chupa tatu Candice akalewa nyang’anyang’a kulewa na kugeuka na kuwa mzigo wa kubwaga kitandani.Hakupata lichotarajia na ili ndo lilimfanya auone usiku wa jana kuwa mbaya .

Alianza kwa kuiangalia maiti kwa mtazamo wa nje kuanzia utosini mpaka unyayoni,kisha akachukuaa damu kwa kutumia sindano na kuitia kwenye chupa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara baadaye akatumia kiwembe na mikasi na kuufumua mwili na kuangalia viungo vya ndani .Alipokamilisha uchunguzi akachukua faili na kuanza kuandika alichokiona, mwishoni akaandika sababu ya kifo ni kuvuja kwa wingi kwa damu kulikosababishwa na kugongwa na gari.

Msaidizi wake alianza kuuweka mwili vizuri ili ufae kwa ajili ya mazishi ndipo alipogundua kuwa kwenye bega la mkono wa kushoto wa maiti kuna maandishi yaliyofifia,yalikuwa yakisomeka hivi USIKU WA MASHETANI.Omari alipigwa na butwaa akageuka ili kumwambia daktari kile alichokiona lakini kwa kipindi hicho Daktari Anthony alikuwa akifungua mlango kuelekea nje na kisha kwenda kujipumzisha ili usiku wa siku hiyo aweze kutembelea kwenye kumbi za starehe vizuri bila ya bugudha za usingizi .

Siku tatu baada ya kuona maandishi kwenye mwili wa maiti Omari alikuwa akitafakari ni nini maana ya maandishi yale.Jambo jingine lililokuwa linamsumbua ni kuwa siku tatu zimepita tangu mwili uletwe hapo hospitalini ila hakuna mtu hata moja aliyeutambua watu kumi na mbili waliokuja mochwari wakitafuta ndugu zao waliopotea wote walitikisa kichwa kuashiria kutokuufaham mwili uliolala hapo mochwari

zilikuwa zimebaki siku nne tu kama asipotokea mtu wa kudai kumfahamu marehem basi maiti yake itazikwa na Manispaa.Omari akisumbuliwa na maswali hayo aliamua muda wa kazi ukiisha ataondoka na rafiki yake aitwaye John kwenda kupata bia atamueleza nini alichokiona wenda john akawa na majibu.Neno USIKU WA MASHETANI lilikuwa lilikuwa likikisumbua kichwa chake na hiyo ilikuwa ni Ijumaa, mwanzo wa wikendi basi ataenda baa atakunywaa atakunywa kisha atayasahau maandishi hayo,alijidanganya katika hilo la kuyashau maandiki na hakuwa sahihi hata chembe
 
Hotchpotch and namby pamby stuff. Aaaaghraah I feel like vomiting if not puking! Tell it to the birds if not goons.
 
Nice one. Horror story, huh! Ila tafuta mtu wa kukufanyia proof reading. Hongera sana ndugu mtunzi.
 
Tusubirie ujio mwingine part 2 ama hapo ndio mwisho wa reli? Manake kama Shigongo vile,bt nc half story anyway.
 
mtu yeyote anaetaka vitabu vya hadithi ani pm,nina vitabu kama 3 nimeshavisoma,napenda nimpe mtu yeyote yule wa jf maana na mimi ni mpenzi mkubwa wa kusoma hadithi
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom