usiku wa leo utaamua Tanzania inakwenda wapi.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

usiku wa leo utaamua Tanzania inakwenda wapi..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 19, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jua litakapotua na Giza litakapoingia...mwelekeo wa Tanzania utaamuliwa leo. Natumaini wapo watu ambao watasimama pamoja kupinga. Watu wema wa tanzania wapo wapi? Utafika wakati wale wenye kuamin katika udugu na umoja watoke na kusimama pamoja. Wasikubali kuiachia nchi ivurugwe hivi kwa uzembe wa wawatawala. Sijui usiku hu utapitaje..I dread the thought
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  ni upepo tu
  na maisha yataendelea kama kawaida
  alie raisi ataendelea kuwa raisi
  waziri mkuu atabaki palepale
  maskini na umaskini wake...
   
 3. zenmoster

  zenmoster JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ni upepo tu utapita by Jakaya kikwete
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "Nimetoka kapa"
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kwamba, kadiri center of gravity inavyozidi kwenda chini, ndio uwezekano wa muanguko unavyozidi.

  Sasa hivi watu walivyojichokea kutokana na kukosa matumaini, hawajali umewaletea jambo la maana au la kipuuzi, wengi wakipata nafasi ya kuwarushia mawe polisi na kufanya fujo watafanya tu.

  Serikali imeweka mazingira ya vurugu tayari kwa kuwaacha wananchi waishi bila matumaini, na hivyo kuwafanya wawe susceptible kwa makuwadi wa umwagaji damu wanaojifunika mwamvuli wa dini.
   
 6. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitakachobadili tanzania kwa usiku mmoja ni Mungu pekee anaweza kubadili lakini si mwanadamu mwenye moyo unaotawaliwa kuwanza kutenda mabaya tu kila siku
   
 7. A

  August JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  Labda JK anaweza kumuomba Mwamunyange ashikilie Nchi kwa Muda? ili kupunguza hi sintofahamu
   
 8. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Na maisha yataendelea "vertically"
   
 9. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Usiku unapita, watanganyika wanalala, kunakucha, Jumamosi tunaanza weekend. Hakuna chochote.
   
 10. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nchi ipo katika ombwe la uongozi,.. kiongozi mkuu bado ni kijana mtalii,mwenye kuhusudu starehe na anasa za kidunia.
  Paka aliefungwa kengele sasa ataamsha na kuwakumbusha watanganyika nini walichonyimwa chini ya kivuli fake hichi cha amani, huku jamii flani ikionewa,.. kama mkristo nakiri tumevumilia mengi, tumeonewa vya kutosha,tumelazimishwa wakati mwingine kukubali hata yale yanayoonekana si haki
  Ikumbukwe Raisi Mkapa alipowaruhusu waislamu watumie majengo ya Umma pale morogoro kufanya chuo chao, haikumaanisha mkristo asiruhusiwe ama akiruhusiwa pale atendewe kama mkimbizi
   
 11. i

  ibange JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Lingekuwa jambo la maana.Mwanakijiji una taarifa gani kwani kuna watu wamepanga kufanya fujo isiku huu.?
   
 12. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mi najiuliza hatma yake ni nini? najua leo watatawanywa, tar 1 nov kesi itakapotajwa tena mambo yatakuwa hayahaya kwahiyo kila siku tukimbie ofisi zetu kuwaogopa hawa jamaa wkt kuna watu tunawalipa watulinde? walizembea mwanzo sasa wakaze uzi
   
 13. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  si habari ndogo kwa yanayotokea sasa tanzania
   
 14. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kumbe hali ni tete hivyo? Nyinyi watawala tuliyowapa dhamana mmeshindwa? Tuanze kuhamisha familia zetu vijijini ana nchi?
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  ndo maana wengine wanasema MMM ni system!anaongea kimafumbo na mitego mingi..
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huu ni upepo tu
  hakuna lolote
  hii haitakuwa news two weeks from now
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli haijakaa sawa maana ni wasiwasi tele miongoni mwa raia.
  Hawaelewi usalama wao uko wapi.
  Na wanaposikia walinzi wa raia na mali wanauliwa ndio wanachanganyikiwa zaidi.

  Eh mungu pisha mbali!
   
 18. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mhhh Ngoja nitafakari kauli yako Ina maneno mazito Ntarudi baadae MMK.
   
 19. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  mkuu nchi itatulia inatakiwa mtu wa kuwakalisha hao waumini na watoe ya moyoni kwasababu kwa sasa hawana imani na bakwata atafutwe muumini atoke shia ,au wapi watakaa chini watasikiliza .watu wako frustrated na maisha magumu wanapopata nafasi ya kupunguza stress yuko tayari ajitoe mhanga kama tunavyoona sasa .hawa watu ni wamoja lakini kila mtu ana kwake hawakai wote msikitini .wakae nao watu wachache wazee wenye busara ,hekima ,maarifa tatizo litakwisha .Lakini nguvu ikitumika sana itakuwa si busara pia itaweka makovu hawatasahau watapumzika siku nyingine wanalianzisha .
   
 20. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kikwete anafurahishwa sana na hii hali,kama mtawala makini wkt hali ikiwa tete alitakiwa kukaa na kutatua matatizo ndani ya nchi yake lakini anadhurura hovyo hovyo sijapata ona rais punguani kama huyu.
   
Loading...