Usiku mwema wanaMMU

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,654
68,612
Habari mabibi na mabwana,

Natumaini hamjambo na mnaendelea vyema,

Sasa ni muda wa kulala,kumpumzisha akili,miili yetu,kwa mlioko ndoani kufurahishana na kutafuta watoto,ambao ni mabachela tuendeleze kununua mablanket mazito maana mikoa mingine kuna baridi sio kama huna mpenzi au mnaishi sehemu tofauti blanket linahusika,mizunguko ya mchana,kazi za hapa na pale,kukorofishana,hebu sahau uupe raha mwili wako kwa maji ya uvuguvugu,kisha panda kitandani peruzi kidogo mitandaoni halafu lala,achana na mawazo,wivu,hasira, kumbuka maisha ni mafupi,akili yako ipe nafasi ya kuwaza mazuri tu ili uote ndoto nzuri usiku huu,kama una kambembeza hebu kavute ukakumbatie upate joto murua (mengine yanaondelea sijui)

Najumuika nanyi usiku huu kuwatakia usingizi mwororo WanaMMU huku mkiburudika na nyimbo ya Aje ya Ally Kiba Nawatakia usiku mwema nawapenda nyote hata ambao hamnipendi nawapenda tu maisha mafupi haya
 
Ok!!! Basi sawa wee lala kwa raha zako wengine sisi huku tumelemewa na vitendea kazi kwa ajili ya kuwalinda watu wanapenda kulala kama wewe!!
 
Habari mabibi na mabwana,natumaini hamjambo na mnaendelea vyema,sasa ni muda wa kulala ,kumpumzisha akili ,miili yetu,kwa mlioko ndoani kufurahishana na kutafuta watoto,ambao ni mabachela tuendeleze kununua mablanket mazito maana mikoa mingine kuna baridi so kama huna mpenzi au mnaishi sehem tofauti blanket linahusika,
Mizunguko ya mchana ,kazi za hapa na pale ,kukorofishana,hebu sahau uupe raha mwili wako kwa maji ya uvuguvugu,kisha panda kitandani peruzi kidogo mitandaoni halaf lala ,achana na mawazo,wivu,hasira, kumbuka maisha ni mafupi ,akili yako ipe nafasi ya kuwaza mazuri tu ili uote ndoto nzuri usiku huu,kama una kambembez hebu kavute ukakumbatie upate joto murua (mengine yanaondelea sijui)
Najumuika nanyi usiku huu kuwatakia usingizi mwororo WanaMMU huku mkiburudika na nyimbo ya Aje ya ally kiba
Nawatakia Usiku mwema nawapenda nyote hata ambao hamnipendi nawapenda tu maisha mafupi haya

We beki tatu unatafuta kiki eh?
 
Aisee ulale unono sana huko.

Nakupa offer leo ya kukuota usiku kucha, just free of charge kabisa.........
 
Back
Top Bottom