Usikivu wa JK umekonga nyoyo za Upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usikivu wa JK umekonga nyoyo za Upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 13, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Upo msemo kwamba dalili njema huonekana asubuhi. Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake uliomalizika juzi limeonyesha ukomavu, umoja na mshikamano baada ya kufikia muafaka wa pamoja kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2012.
  Muswada huo wakati unawasilishwa mwaka jana uliteta mvutano mkubwa bungeni kiasi cha kusababisha wapinzani kutoka nje huku upande mwingine ukizomea. Hata hivyo, hatua hii haikuwa na tija kwa Watanzania ambao wana uchu na katiba mpya.
  Viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kinachoongoza Kambi ya Rasmi ya Upinzani bungeni, kutokana na kuona umuhimu wa katiba hiyo mpya, wakachukua jukumu la kuomba kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Kikwete ili waweze kuwasilisha yale ambayo wanayaona yanahitaji ama kurekebishwa au kuingizwa kwenye muswada huo wa sheria ya kuundwa Tume ya kukusanya maoni.
  Kutokana na dhamira njema aliyokuwa nayo Rais wetu tangu kutolewa kwa hoja hiyo, taarifa kupitia vituo vya ITV na TBC zikaeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete amepokea kwa furaha ombi la viongozi wa CHADEMA la kutaka kuonana naye ili kuzungumzia sheria ya mchakato wa uandaaji wa katiba. Aidha taarifa ikaongeza kuwa Rais amewaagiza maafisa wake kuandaa mkutano huo.
  Hii ilikuwa ni busara kubwa ambayo Rais alionesha tofauti na baadhi ya watu ambao walipenda Rais aikatae. Sio ajabu walikuwepo pia ambao hawakupenda viongozi wa CHADEMA kutoa ombi hilo kwa Rais, na badala yake waone maandamano pasipo fursa yoyote ya kufanya mazungumzo kuhusu suala hilo muhimu.
  Kikao cha kwanza kikafanyika Novemba, mwaka jana, kikafuatiwa na kingine na viongozi wa Chadema, Januari 21, mwaka huu, safari hii akiwemo Dk.Wilbrod Slaa ambaye alikutana na Dk. JK kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2010 ambapo JK alimshinda Slaa katika nafasi ya urasi wa nchi yetu.
  Siku hiyo hiyo baada ya kukutana na viongozi wa Chadema pia Rais JK alikutana na viongozi wa NCCR-Mageuzi wakiongozwa na Mwenyekiti James Mbatia. Alishakutana pia na viongozi wa Chama cha CUF.
  Mazungumzo yale kati ya Rais na upande wa upinzani, yalifanikiwa kutokana na usikivu ulio dhahiri wa serikali yetu, kwani marekebisho ambayo ulitaka yafanyike yalikubaliwa na hata muswada huo ulipowasilishwa juzi bungeni mjini Dodoma haukupata pingamizi kama ilivyotarajiwa.
  Katika kuonyesha dhamira ya dhati ya kuungana na serikali katika kupata katiba mpya, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ilimwagia sifa za busara na hekima Rais JK na kuikubali hoja ya serikali.
  Muswada huo una lengo la kufanyia marekebisho vifungu sita vya sheria ya sasa ili kuiboresha na kupata mwafaka wa kitaifa wa kumpa Rais nafasi kuunda Tume ya kuratibu mchakato huo.

  Katika mchakato huu, dalili njema zimeanza kuonekana ambapo kwa mara ya kwanza, Msemaji wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu juzi aliunga mkono hoja ya Serikali. Akasema usikivu ulioonyeshwa na Rais Kikwete hauna mfano na kutaka Watanzania wote wawe wamoja katika kushughulikia mustakabali wa taifa letu.
  Kwa msisitizo akasema, “Bunge hili tukufu lina wajibu mbele ya historia na vizazi vya sasa na vijavyo, kuhakikisha tunapata muafaka wa kitaifa juu ya Tanzania tunayoitaka”. Alieleza hayo huku akitumia muda mwingi kuelezea kwanini kambi ya upinzani inakubaliana na mapendekezo yote ya serikali.
  Tuchukue fursa hii kwanza kumpongeza Rais kwa dhamira yake safi na pia kuipongeza kambi hiyo ya upinzani kwa namna walivyomwelewa Rais wetu kuhusu suala hilo muhimu kwa sasa na baadaye. Pia pongezi kwa wadau wote waliounga mkono muswada huo wakiwemo wabunge wetu ili tuweze kusonga mbele kwa yote tuliyokusudia.
  Ni ishara njema kwa ustawi wa demokrasia ya nchi yetu watu kukubaliana kwa pamoja katika masuala ya msingi kamahili la Katiba.
  Kwa mantiki hii, mwelekeo ni mzuri katika kupata Katiba Mpya mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.
  Kambi ya upinzani imeonesha ukomavu wa kisiasa katika kuunga mkono marekebisho hayo ya muswada na tunaamini katika mchakato mzima mshikamano zaidi utaimarishwa ili taifa lisonge mbele. Kama alivyosema Spika Anne Makinda, sasa wabunge wabishane kwa hoja, kwani uwanja wa ushindani sasa unaonekana ku-balance(uwiano sawa).
  Mungu ibariki nchi yetu Tanzania.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  haya tumesikia JK msikivu!!

  cjui statement hii pro-chadema wanaipokeaje!

  All I can say is, all these are VANITY!
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Amekuwa msikivu baada ya kugundua nini watanzania wanakihitaji na si nini ccm inataka, ndiyo maana kuna mgawanyiko wa mawazo ndani ya ccm kuhusu uamuzi wake.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Heading inasema WAPINZANI na si pro-cdm....tufute dhana ya kuwa upinzani ni cdm!
   
 5. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  PJ hawa cdm itawaua kwa presha,post haiwagusi cdm lkn mtu anailink na cdm...............Nonsense!!!!!
   
 6. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kaka kwenye red unaniangusha. Wewe tunakutegemea humu, uandishi wa kisekondari achananao!
   
Loading...