SoC01 Usikate tamaa, jenga leo kesho yako

Stories of Change - 2021 Competition
Sep 19, 2021
8
7
Najua unajihisi mkosaji au unamikosi wakatimwingine pia marafiki wanakukatisha tamaa, wanakwambi kweli wewe hunabahati hata hili pia limekupita, ngoja nikwambie hayo upitiayo kuna wanadamu wenzako yanawakuta makubwa kuliko hayo.

Najua umeshwahi kujiuliza hivi kinanini kizazi cha ukoo wangu ukapindukia nakuona labda yanayokukuta nilaana za mababu zako sasa unalipwa wewe.

Unahaki yakudhani hayo lakini tambuka kila jambo linasababu na kusudio kwako ndio kusudio lakini sio hilo unalodhani kwamba umekuja ulimwenguni kusindikiza wengine kwani hakuna msindikizaji wala muongozaji katika huu ulimwengi maana hii ni milki ya Yule aliye umba peke.

Hebu nikupe kisa cha kijana ambaye tunampa jin la kubuni ili kupoteza uhalisia wake tumuite Joseph anasema yeye nimtoto wa mwisho katika familia yake aliyelelewa na mama tu.

Joseph anasema mama yangu alinipenda sana sikuwahi kudhani kama kuna maisha bila ya yeye na sikujua pia kama yapo yanafananaje.

Mama alijitahidi kunipa kila kitu kilicho ndani ya uwezo wake japo shughuili zake zilikuwa za kilimo mkoani Tanga nilishangaa sana kuona tunaishi katika maisha magumu vile wakati kaka zangu wanaishi maisha ya kifahari jijini dar es salaam, wakati huo nikiwa shule ya msingi.

Msomaji kufika hapa unaona wazi matarajio ya Joseph nitofauti kabisa na maisha wanayo ishi na mama yake katika kijiji cha Magoroto hii inamfanya aone yeye na mama yake hawastahili kabisa kuishi hivi bila ya kujua mpangu wa mungu niupi kwake.
Joseph anasema kunasiku nilimuuliza mama mbona kaka hawaji wala hawatuletei vitu kutoka mjini mpaka mimi niende likizo huko?

Wakati wa likizo Joseph hakutamani hata kurudi lakini ilimbidi na aliona kama ananyanyaswa, basi mama yake alimtazama na kumwambia huku ndiko waliko toka kaka zako jifunze kupitia hayo wakati wako ukifika usijisahau, mwanangu sikwamba kaka zako wametutupa laah bali mji unamengi.

Anasema kufikia hapa mama yake alijitwika mzigo wakuni kichwani jembe lake mkononi akiimba wimbo ule wa karudi baba mmoja kutoka safari ya mbali alipofika sehemu ya kama mnazitaka mali kazifuateni shambani alirejea rejea mama yake Joseph.

Maana kuu ya mama huyuni kumuambia mwanawe maisha mazuri sio mjini tu.

Kunawakati kijiji hiki kiliingiwa na ukame njaa ikashika nafasi mama huyu wala hakuwatafuta wanawe bali siku moja mwanawe mmoja walikuja katika wakati ule basi alirudi mjini na kupeleka chakula cha kutosha kwa mama yake ajabu mama huyu aligawa vyakula vile nusu kwa nusu kila kilo hamsini aliigawa akabaki na 25 na kuigawa nusu hiyi kwa wanakijiji wenzake.

Hali hii ilimkera Josefu maana baada ya muda waliishiwa mama yake akamwambia unajiskiaje ukiwa umeshiba wakati mtoto wa jirani anakufa na njaa.

Kama tutawalea watoto wetu kwa moyo huu basi taifa la Tanzania halitakuwa na mafisadi wala wale wanaojilimbikizia mali, kwa ubinafsi wao.

Hatimaye msimu huu wa njaa ulipita na baada ya Joseph kumaliza elimu ya msingi nikama kaka yake mkubwa alikuja kuwachukua yeye na mama yake yeye alienda kujiandaa na masomo ya sekondari mama yake alienda kusalimia wajukuu wakati wakiwa Dar es salaama mwaka mmoja baadaye mama yake Joseph alifariki dunia, ilikundulika alikuwa na nimonia ya muda mrefu ambayo ilipasua mishipa yake ya kifua.

Ilikuwa huzuni kubwa sana katika familia hii siku tatu kabla ya kukutwa na umauti mama huyu Joseph anasema siku hiyo tulikaa nnje akanitazama kasema umefurahi sasa tupo mjini hapa na pale unaenda kwa gari tulifurahi tuka cheka kwa pamoja baada ya kucheka alinilaza miguuni nakumbuka ulikuwa mwaka 2000 akasema mwanangu nikiondoka katika ulimwengu huu tambua siku nilikuzaa nilikuzaa peke yako japo wapo walio kutangulia.

Kumbuka asili yetu ni umasikini hivyo maisha haya ya raha yakikutupa mkono nisawa na kurudi katika asili yako maana ulikuja ulimwenguni mikono mitupu nautaondoka mikono mitupu, nitakuwacha na wakati mgumu sana lakini ngoja nikwambie kitu mara zote ulipouliza kuhusu baba yako nilikwambia kafa hapana nimzima wa afya ila tuliachana nilishindwa na uke wenza alitaka sana kubaki na wewe na alijitahidi sana kukuhudumia lakini nilikataa msaada wake kwa machungu.

Ugomvi wetu uwache ubaki kwetu usiache kwenda kumtembelea.

Haya yalikuwa maneno ya mwisho kabisa kabla ya mama huyu uondoka katika hii dunia Joseph anasema walisafirisha maiti na kuzika kijijini kwao Magoroto baada ya miaka miwili kupita Joseph anasema wakati huo nilikuwa kidato cha pili hapo nikaanza kuambiwa sina akili napoteza pesa bure, lakini kaka hakusikiliza.

Waswahili wanasema wimbo mbaya uimbe mara kwa mara mwisho utakuwa mzuri.

Siku moja nilienda kumtembelea dada yangu shangazi kwa mjomba niliondoka kifua kinaniuma sana nilipo rudi niliambiwa nichote maji nikasema siwezi kifua kinanibana na yalikuwa masafa marefu kidogo sehemu aliyofikia Joseph Dare s salaam ameomba tuifiche kulinda familia yake na utambulisho wake.

Basi aliposema hayo hayakumpendeza shemeji yake lakini hakuwa na jinsi maana asinge weza anasema anachokumbuka zaidi nikauli ya utaona aliporudi kaka yake hajui nini kilizungumzwa chumbani lakini aliamuliwa kuondoka katika nyumba usiku wa saa mbili hiyo tena akinyang’anywa kila kitu alicho wahi kununuliwa "iliniuma sana niliondoka na nguo mbili tu nilizo vaa na nyingine katika mfuko wa ramba, nilihisi dunia imenielemea namkumbuka mama yangu sasa nashindwa kujua naelekea wapi kwa takribani saa tatu nilielekea kwa kaka yangu mdogo alisikitika sana hali yake haikuwa ya kunisomesha mimi na watoto wake"

Nilihama Dar nikatokomea mbali sitakutaja jina nilipofika huko niliishi na mtu aliyekuwa akijuana na kaka Dar nikaanza kujishuhulisha na kazi ya kunyoa Saluni nikijiendeleza kimasomo mpaka nika maliza kidato cha nne kila siku nilikuwa nikisema mama uliniandaa kupambana naelewa sasa uliposema siku unanizaa nilikuja peke yangu.

Stori ya kijana huyu nindefu sana lakini kwa ufupi umetambua yale yote aliopitia kijijini yalikuwa na makusudia japo hakuyaona haya yalikuwa nimaanalizi kwake ya kuja kuyakamilisha maisha haya kila alilomueleza mama yake ilikuwa nikumuandaa japo hata mama yake hakujua kwamba mwanawe atapitia haya.

Huu ndio ukubwa wa yule aliye kuumba yule aliye umba mbingu na ardhi.

Leo hii Joseph ni muandishi mkubwa tu hapa Tanzania na yuko mbioni kuanzisha taasisi yake ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wazo hili linamjia kila akikumbuka kauli ya mama yake "unajisikiaje ukishiba wakati mtoto wa jirani yako anakufa njaa" tuishi kwa upendo usikate tamaa walausidhani kukatishwa masomo ni mwisho wa maisha au kutosimama tena baada ya kudondoka ndio njia ya kutatua matatizo yako baada ya maisha ya dunia yapo maisha ya akhera kila shida ya dunia nindogo kama punje ya ngano ukilinganisha na adhabu ya akhera
Kutoka sasa simama sema nasonga tena sikati tamaaaa

Mwandishi Mwenenu Binnassib
Jina la mwanzo Mwenenu ni la kubuni
new1.jpg
 
Jina la mwanzo Mwenenu ni la kubuniView attachment 1946013
Sawa
 
Back
Top Bottom