Usijilaumu kwa makosa uliyokwishafanya hakutakusaidia ilaa..

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
USIJILAUMU KWA MAKOSA ULIYOKWISHAFANYA HAKUTAKUSAIDIA KWA NAMNA YOYOTE ILE ZAIDI YA KUKURUDISHA NYUMA.

Moja ya hatua muhimu sana unazotakiwa kupiga ili kuweza kufikia mafanikio makubwa ni kuacha kulalamika au kulaumu wengine. Haijalishi ni nani au nini kimefanya nini, haijalishi ndugu zako wamekufanyia nini, haijalishi serikali imefanya nini, utakapoanza tu kulaumu na kulalamika, umejiondoa kwenye njia ya mafanikio.

Hivyo kila linalotokea unapaswa kulibeba na wewe mwenyewe kuchukua hatua ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.Sasa kuna kitu kingine kibaya sana watu wamekuwa wanafanya na kinawazuia kufikia mafanikio. Kitu hiki ni kujilaumu sana wao wenyewe, kujisema na kujishusha mpaka kufikia hatua ya kujiona hufai.

Kama utakuwa mtu wa kujilaumu kila mara, kwa kujiona huwezi, kwa kujiona hufai, kwa kitu kutokea na kusema nilijua tu sitaweza, kwa kujiona una kisirani, ni vigumu sana kufikia mafanikio makubwa.

Kila mmoja wetu anapitia changamoto mbalimbali kwenye maisha, usikubali changamoto unazopitia zikugeuze wewe kujiona ni mtu wa hovyo sana. Hata kama umefanya kosa kubwa, jifunze kupitia kosa lile na songa mbele.

Kukaa kujilaumu kwa makosa ambayo umeshafanya hakutakusaidia kwa namna yoyote zaidi ya kukuondolea kujiamini na kukuzuia kufikia mafanikio.
 
Well said mkuu....Unaweza ungana na Makirita kutoa semina ya jinsi ya kufanikiwa katika maisha.
 
wakati mwingine mwanadamu unayapitia yalio magumu mno tena mfululizo, wakati huohuo wanzako wanafanikiwa.na ndani mwako uko na dhamiri njema na unamcha Mungu.lkn unadanganywa unadhulumiwa unasalitiwa unakataliiwa na jamii na megineyo kama hayo mengi. unadhani ni moyo wa namna gani utampa mtu huyu.
 
Mtangulize Mungu mbele na ujiamini. Sahau yote ya nyuma. Uwezi ishi maisha ya nyuma. Maisha ni haya sasa hivi ukiwaza na kesho. Usikubali ya nyuma yaingiliane na haya ya mbele yako.
 
Mh!, ni vzr kubaki na mawazo chanya japo si muda wote akili itasoma hivyo.. Sema mambo mengine ni ngumu kumeza,pamoja na kumtegemea Mungu ruhusu hisia zako kupona hata kama ni kwa kujutia nafsi.. Muda unavyokwenda jambo litapunguza makali ya maumivu na Mungu atakuonyesha njia sahihi
 
Asante kwa Kuamia Mungu.
 
Back
Top Bottom