Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,917
- 24,674
Jana nilikuwa na jamaa yangu flani hivi tuliosoma wote College. Naweza kusema tulikutana kama bahati tu kwa sababu tangu tumalize mafunzo yetu hatujawahi kuonana.
Ni yule kijana ambae baada ya kumaliza chuo tu wazazi wake wakaforce aingie kwenye Ndoa (kwa mujibu wa maneno yake), kwa sababu kwao wanavihela hela kidogo. Ila binafsi siamini kwa sababu namjua vyema na moja ya kauli yake kubwa wakati tulivyokuwa chuo ni kuwa kabla hajafikisha miaka 24 atakuwa tayari amefunga ndoa, na ni kweli mwaka huu yuko na 25 tayari yupo kwenye ndoa mwaka mmoja na nusu.
Jamaa ni ameoa mke mzuri kweli lakini ukimtazama tu at first unajua kabisa hiyo ndoa kwake ni ya moto,
hana nuru tena usoni kama ile niliyoizoea kuiona wakati tuko chuo tunaunga unga elimu yetu.
Wakati ule Alikuwa mchangamfu aswaa lakini kwa sasa majukumu yamechukua nuru yake.
Tuliongea sana lakini neno lake kubwa kwangu na aliliongea kama utani na mimi nimelichukulia serious ni kwamba:
"Usijaribu kuingia kwenye Ndoa kwa sababu ya Tamaa, kwa sababu hutaki kumpoteza mpenzi wako kwa sababu ya ule uzuri wake, kwa sababu ya kufanya mapenzi kila unapohitaji au kwa sababu umeona flani anaishi kwa furaha na mkewe ukadhani ukioa na wewe utaishi kama wao. Ndoa ina mambo mengi na jambo kubwa usijaribu kufunga ndoa kabla mwili na akili yako haijakomaa.
Namnukuu "Natamani siku zirudi nyuma niache yale mawazo ya mimi kuoa ili nitafute maisha kwanza, nijipange nikiwa mwenyewe nikomae kimwili, kifikra na kiakili ndiyo nije na wazo la kuoa. Nioe kwa sababu ya kuanzisha familia na sio kwa sababu ya uzuri wa mwanamke, nioe kutafuta msaidizi wangu na sio kuoa kwa sababu ya kutaka kufanya mapenzi"
Mwisho wa kumnukuuu.
Vijana wenzangu wa kiume huo siyo utani, sisi tunatofauti kubwa sana na vijana wenzetu wa kike,
mwanamke anaweza kuolewa akiwa kwenye umri wowote kuanzia miaka 18 na akaishi vizuri kwenye ndoa,
lakini sisi wanaume kuoa na umri wa miaka 18-30 ni kujiongopea.
Miaka hiyo hapo kati ndio miaka ambayo kwa mwanaume ni ya kujipanga at least tufikilie kuoa tukiwa tayari tumefika miaka 30 plus.
Kwa sababu hata akili, mwili na matendo vitakuwa vimefika mahala.
Cc Zero IQ