Usiiharibu 'leo nzuri' kwa kuikumbuka 'jana mbaya'

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Habari!

Wewe, naam wewe ndugu msomaji ni mtu au binadamu?, kati ya hayo mawili, jibu baki nalo mwenyewe.

Lakini, ujumbe wangu kwako leo ni mfupi tu na ni huu:

Duniani kuna msemo unasema; Don't ruin a good today by thinking about a bad yesterday.

Yaani maana yake katika lugha adhimu ya Kiswahili ni maneno yaliyopo katika 'Kichwa' ama 'Title' ya uzi huu.

Kila siku ni siku mpya ya 'kujenga na kutengeneza'. Yaani kila siku mpya ni nafasi ya kila mmoja kufanya mambo mapya na hususani yenye manufaa na faida katika maisha yake na pia kwa wale wanaomzungukan na Ulimwengu kwa ujumla.

Shida zilizopita, Matatizo, Changamoto ama vyovyote vile unavyoweza kuziita ukipenda zisikufanye kulisahau ama kuliweka pembeni kusudi lako na kuhamishia fikra zako huko maana kwa kufanya hivyo kutakuondolea kama si kukupunguzia umakini ama 'Focus' katika yale ambayo umekusudia kuyatekeleza.

Peace!

Always THE GREAT
 
Back
Top Bottom