USIHADAIKE: Hakuna uchawi wa kumfanya mtu akulipe deni

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,794
Humu mitandaoni watu wanapigwa sana. Kuna madalali humu wamejaa shuhuda za kutunga na zinavutia sana!

Kama kungekuwa na huu ushirikina wa kumfanya mtu akulipe mahakama kusingefurika kesi za madai. Ama mahakama zetu zingekuwa na afueni kubwa sana.

Sikiliza nikwambie kuna uchawi moderate tu tena wa kumfanya mtu akopesheke hata kama ananuka madeni na ukishampa pesa yako kumdai unaogopa. Hawa ndio maisha yao japo nao pesa wanayopata hawaifanyii chochote cha maana wanaishia kustarehe na kufanya mambo mengine ya kipuuzi kabisa.

Kuna makabila hutajwa kuwa ni kiboko ya wadeni, yani hao ukiwakopa tafadhali lipa, la sivyo litakupata la kukupata. Lakini nao uwezo wao ni kukuharibu na kukuumiza tu lakini sio kukufanya ulipe.

Kuna njia tano za kushughulika na mdeni sugu:

1. Kama una ushahidi wa maandishi fuata mkondo wa sheria. Lakini makinika deni lisiwe na riba kwakuwa sheria haitambui riba binafsi kama huna leseni ya kufanya biashara ya kukopesha
2. Pata mganga mwenye uwezo wa kumuangamiza. Njia rahisi zaidi ni kuua..ishu za kumpiga vimavi zina michakato mirefu
3. Malizana naye kihuni. Tafuta genge la wana wenye shughuli zao. Wape kazi wakamalizane naye kibingwa. Tit for tat is a fair deal!
4. Mwachie Mungu akupiganie. Kama ni mwamini lakini. Yeye ndio mkuu wa yote atatenda kwa wakati wake.
5. Samehe na sahau uiachie karma ifanye kazi yake! Pambana usimame tena..lakini ukiwa umepata funzo kwa njia ngumu

Usihangaike kutafuta mganga atakayemfanya mdeni/wadeni wako wakulipe. Kumbuka wakati unamtafuta mganga wa kumfanya mdeni akulipe , mdeni naye wakati huo huo anatafuta mganga amsaidie usimdai au usahau deni. Mbaya zaidi mnaweza kumtumia mganga mmoja bila kujijua wote.

Ukipigwa na waganga wa kienyeji kwenye ishu za madeni usije ukalalama hasa kama utakuwa umepitia huu uzi. Kumpeleka mdeni kwa mganga akulipe ni sawa na kupigwa mara mbili. Unaneemesha wezi wawili kwa wakati mmoja na kama kati yao kuna dalali kakutambulisha unaongeza wigo wa kupoteza.

NB: Kuna watu wana ukarimu wa kiMungu, hawajui kumnyima mtu kama wanacho na kuna watu nyuso zimeumbwa bila haya.

Kakukopa hajakulipa lakini bado anakurudia akihitaji msaada wako tena na tena. Lakini sote sie ni waja wa Mola wetu. Yeye ndie ajuaye zaidi yetu sote.
 
Juzi juzi tu mwana umetoka kimbiji, jua kali mjomba maisha yamekugonga kichizi hukukata tamaa ukasota ukachonga ofisi.

Ofisi bado haija simama umeanza kuhonga vibinti, hizo tamaa ndizo zilizonyonga machizi. Zitakuponza wewe kama zilivyomponza na fisi ukikata ringi useme umerogwa na bibi kwa ujinga wako uende kwa mganga kukoka mizizi.
 
Mkuu hili nakukatalia. kuna jamaa alikuwa anamdai mwenzake shilingi laki 8. akaenda kwa mtaalam, akaambiwa akilipwa aache laki 3 commission akakubali. Jamaa alifanyiwa fujo usiku. taa zinazimwa zinawashwa na anasikia sauti zinamwambia lipa deni la sivyo utakufa
jamaa ikabidi alipe deni.
 
Mkuu hili nakukatalia. kuna jamaa alikuwa anamdai mwenzake shilingi laki 8. akaenda kwa mtaalam, akaambiwa akilipwa aache laki 3 commission akakubali. Jamaa alifanyiwa fujo usiku. taa zinazimwa zinawashwa na anasikia sauti zinamwambia lipa deni la sivyo utakufa
jamaa ikabidi alipe deni
OK lakini ilitumika njia ya kuleta fujo na si kwa hiari
 
"uwezo wao ni kukuharibu na kukuumiza tu lakini sio kukufanya ulipe".

Ukiharibiwa na kuumizwa ni notification tosha na litalipwa kwa namna yoyote.

Upo sahihi: Hakuna uchawi unaomuingia mtu na kumshawishi kwa hiari alipe deni. Na best alternative ni kukuharibu na kukuvuruga ikiwezekana kukupoteza kabisa.
 
Mganga yupo ! Nenda ukambani huko Kenya . Mf. Siku ya kesi anaedai anapigwa kuharisha sawa na ya kipindupindu , na anashindwa kufika mahakamani . Vilevile inapigwa dawa ambayo anaedai anamfanya mdaiwa auze kila kitu ili alipe deni .

Ok ok sawa, siwezi kubisha kama kuna ushahidi
 
Back
Top Bottom