Usifanye Masters kama lengo lako sio kutafuta PHD

... tatizo watu wengi ni malimbukeni WA hayo mambo
Mimi ninawatazama kama watu wanaotafuta mafanikio kitaaluma na siyo kifedha na wala si malimbukeni kama ulivyowaita. Wako sawa wacha wasongoke hadi u-prof waendelee kufanya tafiti ziwasaidie watunga sera, watawala, wajasiriamali na wafanyabiashara; ili nao wafanikiwe katika eneo lao hili.
 
MBA ni nzuri mbali na 'status' inaweza kukupatia 'inputs' za kusimamia biashara zako kama hukuajiriwa.
Mimi ninawatazama kama watu wanaotafuta mafanikio kitaaluma na siyo kifedha na wala si malimbukeni kama ulivyowaita. Wako sawa wacha wasongoke hadi u-prof waendelee kufanya tafiti ziwasaidie watunga sera, watawala, wajasiriamali na wafanyabiashara; ili nao wafanikiwe katika eneo lao hili.
Ok hongera mkuu
 
Habari wadau;
Wikiendi iliopita nilikuwa katika mjadala na Rafiki yangu wa siku nyingi ambaye tulipotezana zaidi ya miaka 10 iliopita.Tulikuwa tukijadili safari ya kitaaluma na swala la Masomo.Katika Mjadala tuligusia swala elimu ya Ngazi ya Masters Degree na katika mjadala nilimucha na changamoto moja kwamba,Inapendeza na ni busara zaidi unapoamua kujiunga kwa ajili ya Masomo ya Masters katika Fani yoyote basi lengo lako lisiwe kuishia kwenye Masters bali uwe unalenga kutafuta PHD.

Kwa maana hio nilimwambia ni vizuri eneo utakalochagua kulifanyia utafiti liwe ni eneo ambalo unaweza kuzama zaidi na hata kutoa andika linalofaa kwa ajili ya PHD

Nilimsisitizia kwamba ukweli ni kwamba unaposoma Masters kwa ajili ya kutafuta PHD basi unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata PHD kuliko unaposoma masters kwa sababu unao uwezo wa kulipa ada au kwa sababu unafikiri utapata Mshahara Mkubwa.

Ingawa Mjadala haukufika mwisho ila nimesema niuliete hapa Jamvini kama ni busara kwa mtu kusoma Masters akiwa hana hata wazo wala mpango wa kusoma PHD.Si ni bora akasubiri mpaka ule wakati ambapo atakauwa na maono ya kupata PHD no aingie kilingeni?
Habari Brother. Tafsiri ya "Masters Degree" ni Shahada ya Umahiri/Uzamili,hivyo basi ngazi hii ya Elimu huandaa zaidi Wataalamu waliobobea ktk fani husika ili kuwa Leaders/Viongoz ktk utendaji wa kitaalamu..Planners and Project Decision makers wengi hutokea hapa kwenye Level ya Masters..PHD ni Shahada ya Uzamivu,hii humuandaa zaidi mtu kuwa Reseacher au ktk Academic issues Vyuoni.!.Hivyo unaweza kusoma Masters kwa lengo la kuwa Leader in your area of expertise ,and ts not that necessary kuwa na mlengo wa kusoma Masters kwa ajili ya PhD.
 
Yan unakuta mtu anamiaka 40 bado anangangana kutafta ma PHD, kiatu anatembelea mpaka sole inaisha. Kichwani ana ndoto ya kuwa boss. Mwisho wa siku anaishia kuwa muuza duka. Sasa iyo pesa ya kusoma kuto uko ukipiga hesabu unaweza fungua hata kiwanda kidogo cha kutengeneza sabuni za kogomq.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengine kusoma ni hobi, sio mpaka pesa... Wengine wanasoma for personal safisfaction and self esteem.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine wameridhika na maisha yao waliyonayo.... Kama wazaramo, anakula mara Moja, nguo yake msuri, nyumba ya makuti lakini ana furaha na maisha yake. Alafu kusoma ni talent wengine mnadis wanasoma kwasababu uwezo kichwani hamna. Binafsi napenda kila mtu afanye kile serikali yake ya kichwa inavyomtuma, tusipangiane maisha. Mind your own business.
Kusoma mwisho degree huko mnakoenda nyie ni uoga wenu wa maisha maliza degree kama una kazi yako tayar anza kufanya biashara

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kuna wapumbavu wanawachuuza sana wenzao humu.

we ni mzembe! Masters ni kwa ajili ya SPECIALIZATION au kumwandaa mtu kwa Managerial Levels! PhD kwa ajili ya ku oversee mambo yote hayo niliyosema kama yanaenda inavotakiwa kwa kucheza na policies! PhD ni level za matumizi ya nchi kwa kurekebisha panapoleta shida kwa kila nyanja!
tatizo Masters zetu ufundishaj wake inakuwa kama undergraduate
 
Umegonga penyewe! Kiukweli Masters degree labda kwa mtu anayetaka knowledge mpya ili imuongezee ufanisi zaidi kazini mfano umesoma degree ya BBA ile general alafu umefanya kazi accounts muda mrefu ingawa kwenye degree yako hukuzama na unataka position kubwa zaidi, then unaamua kufanya Masters ya Accounting kuepusha mlolongo wa CPA/ACCA professional exams.

Lakini wengi wanasoma tu ili waipate na kimbilio kubwa ni MBA bila kujua ume target nini. Walau ukiwa na target kuitumia kwa mfano kwenye biashara zako utajua area of concentration ili uende extra miles kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuliko kusoma masters ya accounting bora ukasome CPA au ACCA itakusaidia zaidi.
 
PHD inategemea na spidi yako ya kuleta jambo jipya na la kipekee.Unaweza tafuta PHD hata kwa Miaka 15.Ndio maana nimeshauri kwamba mtu anayeanya Masters alenge PHD ili awe na mchango mzuri katika taaluma yake badala ya kusoma Masters halafu unaendelea kufanya kazi za undergrad.
Mzee Machache alisomea yake wapi? Maana imevuma sana hapa mwishoni
 
First degree ni basic and essential kwa ajira.Makampuni mengi ya private hayatofautishi mwenye bachelor na masters.
Na tena ukimkuta mwenye bachelor amekaa muda mrefu anakuzidi cheo na mshahara unayekuja na masters.
Kusoma ni muhimu hata hivyo ukiweza unganisha umalize yaishe.Wakati mwingine kujiendeleza inategemea na speciality au aina ya kazi unayofanya.
Mfano huwezi kuwa academician au researcher au mwalimu wa chuo kikuu na degree moja au masters lazima utapata challenge inabidi utoboe hadi PhD.
Ukiwa daktari wa degree moja fine ukiamua kuwa bingwa ongeza masters.
Sometimes tusome kwa malengo sio tu just prestige ya sifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko sahihi ,kila fani inanamna inavyotaka kulingana na mahitaji yako...Mfano ukisomea udaktari degree moja unakua kiraka yani kwa wenzetu unakua bado hujakua na kitengo chochote...sasa hapo ili ufanye kazi kwa amani inakubidi ukasome masters,unaspecialize katika eneo moja unapunguza mizigo mingi !!ukiwa daktari wa watoto inakua rahisi kwako hata kujitambulisha ,ukisema wewe ni daktari mtu akakuuliza daktari wa nn kama Ni M.D. lazima kikugumizi kije! !
 
Back
Top Bottom