Usifanye Masters kama lengo lako sio kutafuta PHD

Habari wadau;
Wikiendi iliopita nilikuwa katika mjadala na Rafiki yangu wa siku nyingi ambaye tulipotezana zaidi ya miaka 10 iliopita.Tulikuwa tukijadili safari ya kitaaluma na swala la Masomo.Katika Mjadala tuligusia swala elimu ya Ngazi ya Masters Degree na katika mjadala nilimucha na changamoto moja kwamba,Inapendeza na ni busara zaidi unapoamua kujiunga kwa ajili ya Masomo ya Masters katika Fani yoyote basi lengo lako lisiwe kuishia kwenye Masters bali uwe unalenga kutafuta PHD.

Kwa maana hio nilimwambia ni vizuri eneo utakalochagua kulifanyia utafiti liwe ni eneo ambalo unaweza kuzama zaidi na hata kutoa andika linalofaa kwa ajili ya PHD

Nilimsisitizia kwamba ukweli ni kwamba unaposoma Masters kwa ajili ya kutafuta PHD basi unakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kupata PHD kuliko unaposoma masters kwa sababu unao uwezo wa kulipa ada au kwa sababu unafikiri utapata Mshahara Mkubwa.

Ingawa Mjadala haukufika mwisho ila nimesema niuliete hapa Jamvini kama ni busara kwa mtu kusoma Masters akiwa hana hata wazo wala mpango wa kusoma PHD.Si ni bora akasubiri mpaka ule wakati ambapo atakauwa na maono ya kupata PHD no aingie kilingeni?
Umemlisha tangopori jamaa yako.
Masters (shahada ya uzamili) inalenga kumuimarisha msomaji kwenye ubobezi wa kitu fulani kwa undani zaidi. Kwenye shahada za kwanza huwa tunasoma vitu vingi sana, huwezi kubobea katika vyote, hivyo shahada ya uzamili inakusaidia kubobea kwenye kitu kimoja ama viwili BASI. Phd (uzamivu) ni mwendelezo wa uzamili, lakini kwa undani zaidi. Kusoma masters sio lazima ulenge kusoma PhD.
 
Umemlisha tangopori jamaa yako.
Mastars (shahada ya uzamili) inalenga kumuimarisha msomaji kwenye ubobezi wa kitu fulani kwa undani zaidi. Kwenye shahada za kwanza huwa tunasoma vitu vingi sana, huwezi kubobea katika vyote, hivyo shahada ya uzamili inakusaidia kubobea kwenye kitu kimoja ama viwili BASI. Phd (uzamivu) ni mwendelezo wa uzamili, lakini kwa undani zaidi. Kusoma masters sio lazima ulenge kusoma PhD.
Ruge (Rip) alikuwa mbobezi katika kazi yake

Nafikiri kuna baadhi ya fani ndio zinahitaji masters tu zingine general skills na kuwa more flexible zinaleta more output than masters

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisoma masters na sina lengo la kufanya PhD (japo siondoi uwezekano huko mbeleni wa mimi kusoma zaidi). Kwanini nilifanya masters, na kwanini sitafanya (any time soon) PhD?.
Nilipomaliza undergraduate niliajiriwa kwenye ofisi inayojihusisha sana na tafiti. Kwa kiasi kikubwa kazi za ofisi zilifanywa kwa kandarasi (consultancy) na sie waajiriwa/ofisi tulisimamia wakandarasi kwa niaba ya serikali na taasisi zake, mashirika na watu binafsi wanaohitaji tafiti hizo. Niligundua wachukua kandarasi wengi hawana uwezo (wa kitaaluma) wala taarifa/data za tafiti wanazoomba kuzifanya na wengi wao wako bussy sana. Mara nyingi walirudi kwa mlango wa nyuma na kutulipa sisi tuwafanyie kazi hizo, kwa malipo kiduuchu huko wao wakipata hela ya maana (ujanja-ujanja na udali mwingi).
Baada ya muda niliacha kazi kwenye hii ofisi, lengo likiwa nami niwe naomba kandarasi zitakazotangazwa. Kandarasi nyingi zilitaka kigezo cha masters na zaidi. Hii ilisababisha nikose kazi hivyo nikawa natumia watu wenye masters kuombea kazi (ambapo wengi walitaka mgawo pasu-kwa-pasu japo hawashiriki kwenye kazi hata kidogo). Hii ilinisukuma kusoma masters....na kuanzia hapo mambo yamebadilika for better. My point is unaweza kusoma masters na usiwe na mpango kabisa (wala hitaji) la kusoma PhD.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom