Usifanye kosa hili kwenye mapenzi, utajuta daima. Utageuka kuwa chizi uropoke peke yako barabarani

mimi nikiamua kufanya nafanya kwa akili zangu timamu,hakuna cha shetani kunipitia wala nini....mambo mengine nikujiendekeza tuu na kujihalalishia kufanya dhambi kwa kujitetea eti "binadam sio mkamilifu" lol
hizo akili timam unazokua nazo wakati wakutenda makosa ndo udhaifu wenyewe wa mwanadam ndo maana watu hujutia makosa au we hujutiagi mkuu?
 
Ukiacha Mungu na wazazi, siku zote unapendwa na watu walio chini yako... na wewe unapenda walio juu ya viwango vyako.

Umeelewa hapo!

Hii ndo sababu ya kila mtu kusaka kilicho bora kwake, kilicho juu yake... ukitaka 'wanaokupenda' basi ukubali kupokea chini ya kiwango maana ni mara chache mno aliyekuzidi akawa anakupenda bila kutia juhudi zako.
Hii nayo point,lakin mim bado npo kwa mtoa Uzi,ukitaka uishi kwa amani inabid umpende anaekupenda,usilazimishe kupendwa
Fact
 
Andikeni weeee,Ila Mimi sitokaa nimpende mwanamke,tuishie tu kwa vile tumeambiwa tuishie nao na Alie mbinguni,Ila kukolea kwa Hawa viumbe hapana kwa kihindi NEHI,NEHI.
 
Huu ushauri ni kama sehemu tu ya page 1, ya kitabu kiitwacho JINSI YA KUMWELEWA MWANAMKE, chenye page 803,000.
 
Huyo "atakayekuwa amekupenda wewe" naye atasoma uzi huu naye atataka apate wa kumpenda yeye kwanza. Hii philosophy kuna upande unauumiza bila kujua
 
Najaribu tu kuukumbusha ubongo wako kidogo, jambo dogo ila ndio source ya mambo yote mabaya katika ndoa au mapenzi.

Usiwe na mahusiano ya kimapenzi na mtu unayempenda wewe huku hujajihakikishia kuwa anakupenda pia au la.

Kuwa katika mapenzi na mwanamke au mwanaume anayekupenda na si unayempenda. Ikitokea na wewe umempenda pia itakuwa vizuri zaidi.

Usiuruhusu moyo ukutawale kwenye mapenzi, moyo utakupeleka direct kwa mtu unayempenda bila kujali anakupenda au la na mwisho wa siku utajikuta umeumia.

Kuna nyuzi nyingi za vijana kufanyiwa upumbavu na wapenzi wao humu ndani. Hii inatupa picha kuwa wamependa na hawajapendwa.

Upendo ndio utamfanya mwenzako akuonee huruma na si kukufanya ATM machine kila siku.

Upendo ndio utaleta msamaha toka kwa mwenzi wako pale utakapomkosea.

Upendo ndio utamfanya mwenzako asikucheat hovyohovyo.

Upendo ndio utamfanya mwenzako akusikilize mnapopanga mipango yenu ya kiuchumi.
Indidi

sijui kama kidhungu hicho nimekipatia si eti ndugu watanzania?
 
Back
Top Bottom